Mama anayejishughulisha na kuuza samaki pembezoni mwa lango kuu la kuingilia katika soko kuu la manispaa ya Songea (kushoto) akimfungia mteja wake kitoweo hicho kama alivyonaswa na kamera yetu mjini Songea.
Mchuuzi wa vitunguu katika soko la kuu la Songea mkoani Ruvuma Bw Mkuya Omari, akipanga vitunguu hivyo chini huku maji machafu yanayotoka kwenye mabucha yaliyopo sokoni humo yakitiririka bila kuzingatia kanuni za afya,uuzaji wa vyakula wa aina hii ni hatari kwa walaji.
Muuza chumvi Ramadhan Said akisubiri wateja kando kando ya mtaa wa mkwepu mjini songea ambapo huuza kila kopo moja kwa shilingi 300,chumvi ya aina hii isiyokuwa na madini joto haifai kwa matumizi ya binadamu.
PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII,RUVUMA.
PICHA NA MUHIDIN AMRI WA GLOBU YA JAMII,RUVUMA.
hii chumvi ndo nzuri iliyowafanya wazee wetu waishi miaka mingi.wamekuja wajanja wanataka kuuza madini yao wamelazimisha tuwekewe kwenye chumvi hamna lolote zaidi ya kutupunguza nguvu za kiume tu na kutupunguzia umri.kula kitu natural hicho walichokuwa wanakula mababu.
ReplyDelete