Mwenyekiti wa TLP,Mh. Agustino Mrema akihutubia wananchi katika kiwanja cha Tengeru leo wakati wa uzinduzi wa kampeni wa chama hicho uliofanyika katika uwanja huo na kumnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya chama hicho,Bw. Alesanda Abrahamu.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP,Mh. Agustino Mrema akimnadi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa tiketi ya chama cha TLP,Bw. Alexanda Abrahamu kwa wananchi walioudhuria katika mkutano huo huku akiwaambia wampe kura kama yeye alivyowasaidia kuwasuluisha kipindi cha vita ya mwaka 1993.Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii,Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. jamani huyu ndie mrema tunajemjua au sie...si alisema babu amemponya au...wanasiasa wetu bwana.

    ReplyDelete
  2. Yaani ndio Mrema kaisha hivi, alikuwa najaza Kirumba enzi zake leo hii ana watu 15! maajabu ya Musa.

    ReplyDelete
  3. HAWA WAZEE NAONA WAMEKUWA KAMA WAKINA MPOKI ! WATU WANAENDA KWENYE MIKUTANO YAKO KUCHEKA TU , AWANA SUMU KABISA , NAZANI NI MUDA WA MREMA KUTULIA KWENYE NYUMBA ZA KULELEWA WAZEE!

    MDAU PARIS

    ReplyDelete
  4. Kafara la waislam pale msikiti wa mtoro kariakoo kisomo kilichoongozwa na sheikh imam kassim bin jumaa kimemtengeneza cheza na waislam

    ReplyDelete
  5. Aikambe Meku, Msee na mimi Mangi nipeni Kura sangu!

    ReplyDelete
  6. Kweli Mdau wa PARIS nakuunga mkono!

    Ni wakati muafaka 'Sheikh Mrema' akatulia Mjengoni mustarehe akaanza kula Kodi ya Wananchi kutokana na Utumishi wake kwetu!

    ReplyDelete
  7. Naam, Kisimamo cha waislamu na hasa pale alipokhutubia Mbagara kusema kuwa akipata urais atakomesha adhana zote maana zinapiga kelele! wakome

    ReplyDelete
  8. Tuache mzaha wakati wa kazi. Demokrasia hii 2nai2 100(tunaitumia)vibaya.Mrema weka damu changa halafu ukae kando na kuwashauri. Unamjua Edwi Mtei?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...