Mama aliekuwa na watoto wake wawili,Mmoja akiwa amembeba mgongoni na mwingine akiwa amemshika mkono huku akiwa na mzigo kichwani na mwingine mkononi akielekea nyumbani wakati akitokea mahala anakofanya shughuli zake kama alivyonaswa na Kamera Man wa Globu ya Jamii leo,Mkoani Morogoro.
Watoto ambao umri wao ni wa kuwa shuleni hivi sasa,wakifanya biashara ya kuuza ndizi pembezoni kwa barabara ielekeayo Morogoro Mjini.

Wakazi wa Mji wa Morogoro wakitoka sokoni kununua bidhaa mbali mbali.
Mkaa ukipelekwa sokoni.
Abirira wa Basi la Champion lifanyalo safari zake kati ya Dar-Dodoma wakiwa wamesimama huku wakitafakali la kufanya mara baada ya basi hilo walilokuwa wakisafiria kuharibika wakati likiwa safarini,mapema leo asubuhi nje kidogo ya mji wa Morogoro.
Wanafunzi wakitoka kuteka maji mali na shule wasomayo kwa ajili ya matumizi mbali mbali shuleni kwao.
Safari ni hatua na kina Mama hawa wanalidhihirisha hilo.









What will we do without women. My mothers, grandmothers,sisters and daughters you rock. Ukiangalia hizi picha za Morogoro karibu kila mwanamke anaonekana akifanya kazi ya watu wawili. Mungu wabariki wanawake bila ya wao tusingepata malezi mazuri na maendeleo tuliyo nayo.
ReplyDeleteI agree with the recent comment. Now,the question is, where are the men - or rather, what are they doing while these women are working???
ReplyDelete@anonymous 1. kama ulikuepo ndgu yangu wazazi wetu wanapata tabu sana, alafu sie tukishakua maboss makazini tunawatelekeza.
ReplyDeleteMpiga picha tafadhali nipatie jinsi ya kumpata mama mwenye mtoto mgongoni..
ReplyDeleteUkipanda basi la Champion ukafika bila shida yoyote shukuru. Ni mabovu kila sehemu, viti injini, bodi. lakini bado watu wayapanda tu. Wapiga debe wanatuponza sana
ReplyDeleteUkiona Wanawake Vijini wanafanya kazi ujue Wanaume wapo Vilabuni wanalewa Pombe!
ReplyDeleteMwanamke popote alipo, ni mke, mpishi, mtumishi wa nyumbani, mlezi wa watoto, ofisini ni Manager, au Secretary au accountant lakini nyumbani hizi zote ziko combined, including being a doctor and nurse, orderly (maana saa nyingie inabidi azoe matapishi ya baba anapokuwa amelewa sana) a teacher counsellor, mwamuzi wa masumbwi ya watoto akiwa na watoto wakiume watupu. Strategic Planner/cum financial plannner (ingawa safe analo mwenyewe) of all family including extended family, ie. if the husband is the only well-to-do individual in the clan. Na ole wako ukiwa unafanya kazi na kipato kizuri, pesa ya mwenzako huioni kila kitu nenda kwa mama. Halafu in the end hata ile heshima huwekewi na baba wala watoto.
ReplyDeleteChampion?? hapana... gari zao karibu zote mbovu, waendeshaji vichaa mwendo kasi ajabu, kituo kila mahali kama daladala.. Nilishaapa sitapanda champion tena...
ReplyDeleteswagga la vijijini mnaliona hilo? waosha vinywa mpooooo?
ReplyDeletesio kusifia maendeleo eti tanzania inaendelea sana wacheni kuangalia mjini maisha ya hali halisi ya mtanzania yapo vijijini na sio mjini
Mwanamme pekee ambaye yupo hapo ni huyo dogo ambaye hajabeba kitu chochote. Hii ni halisia sana!!
ReplyDeletewanawake ni kila kituu.
ReplyDeleteNINGEAMRIWA NIMWABUDIE MTU HAPA DUNIANI NINGEMWABUDIA MAMA.
GOD BLESS THE WOMAN.
Du, Kwa kweli bongo bado saaana!
ReplyDeleteBARUA KWENDA MOROGORO:
ReplyDeleteAhhh,
Mjini nimehangaika nimepoteza muda wangu Babdari salama nimekaa sijaona kitu kwangu makini.
Nafungua Blogu ya Jamiii leo hii katika makala hii anona picha ya tatu kutoka juu namuona Binti kabeba pakacha akiwa na wenzie ktk msafara.
Binti huyu ana bashasha ingawa ni ktk picha amevaa siketi nyeusi na blauzi ya kijivu kati kifuani kipo cha mduara kifungo.
ANKAL BINTI WA PICHA YA TATU KUTOKA JUU MWENYE SIKETI NYEUSI NA BILAUZI YA KIJIVU YENYE KIFUNGO CHA MDUARA KIFUANI AMEIJERUHI NAFSI YANGU.
DUH HAZINA IMEFICHIKA VIJIJINI NA MIKOANI!
AMA KWELI MJINI TUNAHANGAIKA BUREEE MAMBO YAPO MKOA NA VIJIJINI!
NAOMBA CONTACTS ZAKE TAFADHALI!
Mdau hapo juu wa BARUA KWENDA MOROGORO,
ReplyDeleteHata mimi Binti amenigusa na mimi nataka nipewe Kontakti zake!
Naahidi kuyatuwa chini mapakacha hayo mawili aliyobeba kichwani nitamwezesha kwa Mtaji hata ikiwezekana kumfungulia Duka la bidhaa.
Binti anapata tabu bure Kijijini kwao mimi naahidi kuzimaliza shida zake ili tuanze maisha mapya naye kama Mke na Mume!