Mzee mwenye umri wa miaka 120 katika Kijiji cha Ngongongare, Kata ya Maji ya Chai, IbrahimMbise (kushoto) akimuombea baraka kimila mgombea wa CCM jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, uliofanyika katika kijiji hicho, jana.
Kinamama wakimshangilia Sioi baada ya msafara wake wa kampeni kuwasili kijiji cha Ngongongare,Maji ya Chai, jana.
Mfuasi wa CCM akishangilia 'kwa raha zake' kwenye mkutano wa kampeni za CCM katika kijiji cha Ngongongare. Kulia ni mmoja wa polisi ambao huwepo kuimarisha ulinzi kila mikutano ya kampeni ya vyama vinavyoshiriki uchaguzimdogo jimboni humo.
Uhaba wa maji katika maeneo kadhaa katika jimbo la Arumeru Mashariki ni miongoni mwa kero ambazo wagombea wa vyama mbalimbali vinavyoshiriki kampeni za uchaguzi mdogo jimboni humo,wamekuwa wakiahidi kuupatia ufumbuzi. Pichani, watoto wakisafiri kwa punda kutafuta maji katika kijiji cha Ngongongare, jimboni humo,jana.
Mwanafunzi wa shule ya sekondari Ngongongare, Maji ya Chai, akiwa kwenye dirisha la shule hiyo wakati akifuatilia mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji hicho jana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nimependa hiyo five spokes rimz kitu Arumeru green car!

    ReplyDelete
  2. Kazi iliyopo kwa MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI:

    1.Kuondokana na Usafiri huo wa Ujima wa kutumia Mnyama, kwa kuwa Wanaharakati wa Wanyama wanakuja juu sana kwa matumizi ya viumbe ktk utaratibu huu.

    2.Hii adha ya kutumia muda mrefu wa kutafuta maji badala ya kufanya kazi ili kuazalisha mali na kujenga taifa inatakiwa iangaliwe.

    3.Matumaini yarejeshwe kwa Wananchi kama inavyoonekana Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari hapo chini ameshika shavu kwa kupigwa na butwaa,,,ili watu waweze kuishi maisha marefu kama Mzee Ibrahimu Mbise (Miaka 120) hapo picha ya kwanza juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...