Hasheem Thabeet katikati na jezi ya timu yake mpya
Na Dina Ismail Blog
MCHEZAJI wa kulipwa wa mpira wa kikapu wa Tanzania, Hasheem Thabeet amechukuliwa na klabu ya Portland Trail Blazers inayoshiriki kwenye Ligi ya Mpira wa Kikapu nchini Marekani (NBA) kutoka klabu ya Houston Rockets.

Kwa mujibu wa taarifa za kwenye mitandao mbalimbali ya intaneti, Portland Trail Blazers imefanikiwa kumnyakua Mtanzania huyo kutoka Rockets kwa kubadilishana na mchezaji mwingine Marcus Camby, jana ambayo ilikuwa siku ya mwisho iliyowekwa na NBA kwa ajili ya klabu zinazocheza ligi hiyo kufanya utaratibu huo wa kubadilishana wachezaji.

Mlinzi Jonny Flynn, pia amejiunga na klabu ya Portland Trail Blazers kama sehemu ya utaratibu huo, Thabeet ambaye sasa amechukuliwa na Blazers kabla alichukuliwa na Houston Februari mwaka jana, akitokea Memphis na alifanikiwa kuichezea Rockets mechi tano pekee katika msimu huu wa ligi.

“Tunatazamia kuwa yale yatakayofanywa na Jonny pamoja na Thabeet yanaweza kuleta mafanikio katika timu yetu na pia tunamshukuru Marcus kwa mchango alioutoa kwa kipindi cha misimu mitatu aliyokuwa nasi na tunamtakia kila la heri huko alikoenda,” alisema Kaimu Meneja Mkuu wa Blazers Chad Buchanan.

Katika michezo 120 ya misimu mitatu akiwa na klabu za Memphis na Houston, Thabeet mwenye umri wa miaka 25, ana wastani wa pointi 2.2, na jumla ya dakika 10.7 pamoja na rebaundi 2.7.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. BIG UP TANZANIA AHSANTE UPER STAR THABET UMETUFUNGUA MACHO WA TZ KAONYESHE GEMU KALI BLAZER LAKINI TUTA KUMISS BIG TYME HTOWN

    ReplyDelete
  2. Kijana Thabeet Carroll

    ReplyDelete
  3. Huyu jamaa ana matatizo na hapo Portland ataendelea kukaa benchi tu. Ni haibu lakini jamaa hajitumi hata kidogo na anaonekana ni muoga wa kucheza.

    ReplyDelete
  4. Kila la Kheri Mwanandugu Big Super Star Hasheem Thabit!

    Mungu akupe uwezo!

    Jitahidi, Jirekebishe na Ujitume,,,nduguzo tunakutegemea!

    ReplyDelete
  5. Hasheem Thabit

    Inshallah Mwenyezi Mungu akuwezeshe na kukufungulia zaidi!

    AMIIIIIIIIIINNNNNNNNN!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...