Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mambo ya Ndani Bw.  Mbarak Abdulwakil pamoja na Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi inayotengeneza vifaa vya kuzimia moto vyenye teknolojia ya kisasa vinavyoitwa DSPA 5, wakikiandaa kifaa hicho kwa ajili ya kukirusha ndani ya kontena lililowashwa moto, ili kufunga mlango na kuruhusu kifaa hicho kufungua gesi ya Oxgen baada ya sekunde sita tayari  kuzima moto huo ndani ya kontena hilo, tukio hilo lilikuwa ni uzinduzi wa vifaa hivyo hapa nchini, uliofanyika katika viwanja vya Kikosi cha kuzima moto Fire jijini Dar es salaam leo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Mbarak Abdulwakil kulia  akipokea moja ya vifaa hivyo DSPA 5 kutoka kwa  Damian George kushoto Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya  Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini , wa pili kutoka kulia ni Kamishna wa kikosi cha Zimamoto  Kamanda Pius Nyambacha na anayefuatia ni Frans Vogelzangs Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi. 
 Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi,Frans Vogelzangs akimwelekeza katibu mkuu Mbarak Abdulwakil katikati jinsi ya kuuweka ufunguo wa kifaa hicho kabla ya kukirusha ndani ya kontena lenye moto, Kushoto ni Damian George Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Your Solution Limited inayosambaza vifaa hivyo hapa nchini.
 Meneja Mkuu wa kampuni ya AFG Group ya Uholanzi,Frans Vogelzangs akiwaelezea wageni waalikwa mbalimbali pamoja na waandishi wa habari jinsi kifaa hicho kinavyofanya kazi.
 Askari wa Kikosi cha kuzima mto wakiwa tayari kwa kuzima masalia madogo madogo ya moto baada ya kifaa hicho kufanya kazi yake kikamilifu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. sasa masalia ya moto yanatoka wapi kama kimetenda kikamilifu.Bongo bwana kuvamia mambo harakaharaka hatujambo.Haya twendage wandugu.Mtaniambia siendi na wakati hata mie mfuasi mzuri tu wa teknohama lakini yako mengine yanahusu hata afya zetu na mbinu za kawaida ambazo ni madhubuti tunapuuza na vilevile uvivu ndo maana tunarukia mambo rahisi rahisi.Utaona kujaza maji ya dawa tu kwenye gari la fire ni ishu mpaka moto utokee ndo heka heka ianze.

    ReplyDelete
  2. Really? Jamani tuwe serious. Yaani kidubwesho hicho kiwatoe watu kwenye shughuli zao? Why is this even news? Pipo tuwe serious.

    ReplyDelete
  3. I feel sorry for africans...i real do....

    ReplyDelete
  4. Kufungu gesi ya Oxygen???????

    ReplyDelete
  5. mdau wa mwanzo nimeshindwa kufahamu point yako. kwanza ni nini masalia ya moto? Na kama umekusudia moshi kwani hujui kuwa hata moto ukiwa umezimika, moshi takriban huwepo?

    ReplyDelete
  6. Vifaa vyetu hivo watu wa uholanzi tunatesa lol

    ReplyDelete
  7. moto mara nyingi unatokea kwenye makazi ya watu na ofisini,huo mfano wa kuzima moto ndani ya kontena ni mfano mfu.Zimamoto wanahitaji vitendea kazi kwa mfano,mabomba yasiyovuja,maji kwa urahisi,gari imara, mavazi sahihi,na mwisho vituo zaidi vya zimamoto.kukitimiza haya hatuna haja ya mtu kutufundisha jinsi ya kuzima moto kwenye mazingira ya kitanzania.hipo siku tutafundishwa hata jinsi ya kwenda aja kubwa na ndogo kwenye vyoo vya kukaa!!!!

    ReplyDelete
  8. Waafrika tutauziwa hata kinyesi cha mbwa tukiambiwa kina zima moto ili mradi ni mzungu anayekiuza.. jamani hata primary tulifundishwa Oxygen gas inasababisha kuwasha moto, hauhitaji kwenda secondary wala university kugundua huu ni wizi wa kimachomacho... Since when Oxygen is used to fight fire? I've never heard that crap anywhere.... Afu ajabu Angekuja mweusi mwenzetu na huu uongo tungegundua lakini kwa vile ni mzungu nope we are freaking blinds.

    ReplyDelete
  9. Sasa zoezi la kuzima moto hiyo Laptop inakuwa vipi hapo?

    ReplyDelete
  10. May be huyo mzungu alisema "Carbon-dioxide" afu repoter akachanganya habari.., hahaha

    ReplyDelete
  11. HICHO KIFAA KINAITWA DSPA-5,NA KINATOA AEROSOL,MWANZO KWA WATU WA NJE WALIKUWA WANAKITUMIA KUZIMIA MOTO WA KWENYE NYAMBIZI,NA AEROSOL INAFANYA KAZI SAWA NA GESI YA KAWAIDA HUTANUKA NA KUJAA CHUMBA,TOFAUTI YA KABONI NA AEROSOL NI,KABON NI HEWA YA UKAA,NA AEROSOL KAZI YAKE NI KUNYONYA HEAT,NA AINA MADHARA KWA BINADAMU NA HATA MIMEA/WANYAMA.
    IF U WANT TO KNOW MORE CONTACT THE OWNER OF THIS BLOG,HE WILL SHOW U TO US.THANK U

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...