Meneja wa Bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizngumza na waandishi wa vyombo mbali mbali vya habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa kuzungumzia mchakato mzima wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 zinazoendelea hivi sasa nchini na kuwataka wanahabari kutoa somo kwa wasanii wanaozibeza Tuzo hizo na wale wanaojitoa kwenye mchakato bila sababu za msingi,Mkutano huo umefanyika katika hoteli ya Double Tree,Jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya 1Plus Communications,Fina Mango akitoa muongozo kwa waandishi wa habari namna mchakato wa Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 unavyoendelea na ufafanuzi wa namna mchakato mzima upigaji wa kura kwa wasanii wanaowania Tuzo hizo zinavyoendelea kupigwa,wakati wa mkutano uliofanyika leo kwenye hoteli ya Double Tree,Jijini Dar es Salaam leo.
Mratibu wa Tuzo Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2012 na Muwakilishi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA),Angelo Luhala akionyesha karatasi yenye historia ya tangu kuanzishwa kwa Tuzo hizo mnamo mwaka 1999,wakati akizungumza na kutoa ufafanuzi wa namna Tuzo hizo zilivyokuwa zikiendeshwa na makampuni mbali mbali kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhulia mkutano huo leo kwenye hoteli ya Double Tree,Jijini Dar es Salaam.
Meneja Miradi wa Kampuni ya Inovex,Lloyd Zhungu akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusina na namna kura zinavyotakiwa kupigwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...