Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Abdalla Mwinyi akitoa hotuba katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar  katika Ukumbi wa Eacrotanal mjini Zanzibar. Kushoto yake ni Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo wa Zanzibar Bihindi Hamadi Khamis na kulia kwake ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA)Sudi Mohd Masoud
Wanafunzi kutoka katika Skuli ya Uroa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja wakitoa burudani katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar 
 Mwanafunzi kutoka skuli ya Vikokotoni Machano Bakari Hussen akipokea zawadi na Kumshukuru Mungu baada ya Kushinda katika chemsha Bongo ya Maswali ya papo kwa papo huko katika Maadhimisho ya siku ya Kiswahili Zanzibar .Picha na Yussuf Simai Ali-Maelezo Zanzibar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Michuzi inaonekana unaipenda sana zanzibar

    ReplyDelete
  2. Kwakweli hii imenifurahisha sana na sijajua kama Tanzania ina siku ya Kiswahili nje ya hii ya Zanzibar.

    ReplyDelete
  3. Duh watu kwa kupenda sherehe kesho kutwa kutakua na sherehe ya kuvaa kanga-

    Ok hii shule ya VIKOKOTONI zamani ni wanafunzi wa town tu lakini siku hizi haya majina unajua wanatokea mikoa ya kaskazini na kusini-

    hivi huyo bi hindi mbona simuoni naona wote waswahili humu

    ReplyDelete
  4. Mdau wa tatu kazi huna jema kazi lawama tu.

    Shule ya Vikokoni eti ya wanafunzi wa town, kwani huo mji ulikuwa na watu wenye majina maalumu - akina bin Kinana bin Khuzaymata?

    Na wewe jinsi ulivyogubikwa na kiza cha ubaguzi unalalamika eti Bihindi humuoni na unaona waswahili kwani umeambiwa Bihindi ni muhindi?

    Watu wengine wanapenda sana kuonyesha kiwango chao cha ujinga katika jamii.

    Samahani lakini umenikera sana kwa dharau zako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...