Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shairif Hamadi alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala mazima ya Utendaji wa Kazi zao na matatizo wanayokumbana nayo,hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar,hii ni baada ya kumaliza kwa Ziara yake ya Kuzitembelea Idara mbalimbali za Wizara hio.
Wafanyakazi mbalimbali wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shairif Hamadi alipokutana nao
Mfanyakazi wa Kamisheni yaMichezo na Utamaduni Othman Mohd (Makombora)akifafanua jambo katika Mkutano wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,uliofanyika hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Mjini Zanzibar.
Mfanyakazi wa Kamisheni ya Michezo na Utamaduni Fatma Issa Juma akifafanua jambo katika Mkutano wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo,uliofanyika hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Mjini Zanzibar
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamadi akifafanua jambo katika mkutano wake na Wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utamaduni Utalii na Michezo alipokutana nao na kuzungumza nao kuhusiana na masuala mazima ya Utendaji wa Kazi zao na matatizo wanayokumbana nayo,hapo katika ukumbi wa Salama Holl Bwawani Zanzibar,hii ni baada ya kumaliza kwa Ziara yake ya Kuzitembelea Idara mbalimbali za Wizara hio.Kushoto yake ni Waziri wa Habari Umaduni Utalii na Michezo Zanzibar Abdillah Jihad Hassan.
PICHA ZOTE NA YUSSUF SIMAI ALI MAELEZO ZANZIBAR
Unguja acheni masihara, yaani mfanyakazi wa wizara anavaa makatambuga ya choo kwenye mkutano. Je, mkutano ulifanyika baada ya kazi, au muda wa kazi? Guys, be serious!
ReplyDeletemdau wa kwanza una point nzuri lakini wakati huo huo kumbuka kuwa wenzenu sisi hali zetu ni mbaya kimshahara. Hatuni sababu yaaki kudanganya kwa kuvaa uzuri ilhali ukweli ni kuwa mifuko imetoboka.
ReplyDeleteNi vizuri tuvae kanda mbili na nguo zilizochaa ili viongozi waone na kujua ukweli kuwa mishahara yetu ni midogo na tunastahili kuwa katika mfumo sawa na wa tanzania bara, angalau hapo tutaweza nasi kununua buti za seconda hand.
Kama anaumwa miguu na daktari wake amemwambia avae makubazi?
ReplyDelete