Mwanamama ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja akifanya biashara ya kuchoma mahindi katika barabara ya Nairobi,Jijini Arusha.Wakina mama wengi jijini humu hujishughulisha na biashara mbali mbali hata zile ambazo hapo awali zilikuwa zikifanywa na kina baba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Haya waosha vinywa ambao kila siku mnasifia kuwa nchi inaendelea kwa kuangalia mjini pekeyake

    muoneni dada yetu anavyotafuta riziki kwa njia kama hiyo hapo utakuta ana watoto na inabidi awasomeshe na chakula juu

    tanzania bado sana maendeleo sio mjini tu mkiona majumba marefu

    swagga lipo vijijini

    ReplyDelete
  2. Utamu wa mahindi ya kuchoma mchomaji awe na mafua makali!!!

    ReplyDelete
  3. Anony Wed Mar 21, 11:35:00 AM 2012"Utamu wa mahindi ya kuchoma mchomaji awe na mafua makali!!"
    Duh! Ama kweli kuna watu wana mineno sijawahi ona lol!!

    ReplyDelete
  4. Ujerumani wauza vyakula huvibeba mgongoni. UK omba omba wanapewa magazeti wauze "Big Issue" na kila gazeti wanapewa 50%. Dunia nzima wajasiriamali wapo na ndio maisha. Tumpe heshima yake kwa kununua mahindi na pia awezeshwe kwa kupatiwa kibaiskeli cha maringi manne.

    ReplyDelete
  5. Shida haina adabu:

    Hadi Dada Mchoma mahindi anaficha uso kupigwa picha akijisikia vibaya na kuwa na haya!

    Jitihada inahitajika kuwaondoa wananchi wa Tanzania na Dunia nzima ktk ajira zisizokuwa rasmi kama huu uchomaji wa mahindi, hapa ina maana:

    1.Uwezeshaji haujawafikia walengwa licha ya sehemu kama Arusha kubarikiwa kwa ardhi iliyo na rutuba na masoko ya bidhaa yaliyoimarika na ya hali ya juu.

    Hili sio tatizo la Tanzania peke yake, isipokuwa ni nchi nyingi sana Duniani mfano taasisi za Uwezeshaji wa Kifedha kama Ma Benki na Asasi mbali mbali zimekuwa ziki sisitizwa na Mashirikisho ya Kimataifa kama WORLD BANK na IMF kuwa na urafiki wa karibu na Wahitaji kwa maana ya kupunguza Mashariti ya utoaji Mikopo na Uwezeshaji na kujenga auaminifu au kutafuta njia mbadala za kuwaamini Wateja kwa njia kama 'Credit Data Bank Refference'

    2.Sera hazijatekelezeka kama zinavyonadiwa na upande wa Siasa za Kidunia na uenezi wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...