Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Adam Malima
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphina Chialo amesema kuwa aliyemwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima vitu mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni katika hoteli ya Nashera mkoani Morogoro sio mwanamke.

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa aliyekamatwa na polisi alipohojiwa alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi nyumbani kwa mama yake mdogo na kwamba waziri Malima hakuwa na bunduki aina ya SMG, kama inavyodaiwa na baadhi ya watu.

Naibu Waziri Malima alikumbwa na mkasa huo uliozua maswali mengi saa 10 alfajiri ya kuamkia Machi 9, mwaka huu baada ya watu kueleza sababu tofauti za wizi huo.Baadhi ya watu walidai kuwa Waziri huyo alikuwa na mtu chumbani anayesaidikiwa alitoroka na vitu hivyo na wengine walidai kuwa aliibiwa na mtu aliyepitia dirishani baada ya kufungua dirisha.

Chialo aliliambia Mwananchi kuwa mmoja wa watuhuniwa wa tukio hilo alipobanwa alieleza wazi kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo.“Unajua haya mambo yanakuzwa lakini hayana ukweli wowote, yupo mtu mmoja ambaye baada ya kumbana alieleza kuwa vitu alivyoiba alivihifadhi kwa mama yake mdogo,” alisema Chialo.

Akizungumzia taarifa kuwa Waziri Malima alikuwa na SMG katika chumba chake alisema “Hakuwa na SMG alikuwa na bastola, SMG ni silaha ambayo hata mimi Kamanda wa polisi siwezi kutembea nayo”Alifafanua kuwa silaha hiyo ya kivita humilikiwa kwa kibali maalumu na kwamba si rahisi kwa mtu kuwa nayo kienyeji.

“Hata silaha ambazo alikuwa nazo Waziri Malima ni za kawaida na anazimiliki kihalali” alisema Chialo.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo, Machi 9 mwaka huu Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Hamisi Seleman alisema ingawa uchunguzi unaendelea kufanyika, taarifa za awali zilieleza kuwa mtu asiyejulikana alivunja dirisha la chumba namba 125 alichopanga Naibu Waziri huyo kisha kuingia ndani na kuiba vitu hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh23.25 milioni.

"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni.

Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh 1 milioni na simu tatu aina ya Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry zenye thamani ya Sh5.5 milioni," alisema kamanda huyo na kuongeza:

"Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola 4,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.

"Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.Kaimu kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema kuwa hata hivyo, mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu iliyowazi.

Katika hatua nyingine, polisi mkoani Morogoro, wanawashikilia watu watano wanaotuhumiwa kumwibia Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Malima katika Hoteli ya Nashera wiki iliyopita huku asilimia 90 ya vitu vilivyoibiwa vikipatikana kutoka kwa watuhumiwa hao.

Kamanda Chialo alisema waliokamatwa kuwa mmoja ni mkazi wa Chamwino kwa Mgulasi na wengine ni wakazi wa Mafiga Manispaa ya Morogoro ambao kwa pamoja wanadaiwa kushiriki katika tukio hilo la wizi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Huyu mheshimiwa alikuwa kwenye ziara ya kiserikali au binafsi, ama alikuwa kibiashara maana bado hii issue bado mimi naona ina mkanganyiko otherwise mwandishi ndo kakosea baadhi ya paragraph,hebu tembelea para no mbili halafu uje uangalie ya tatu toka mwisho. laptop tatu,vinasa sauti sauti,simu, dola.

    ReplyDelete
  2. Hivi kweli kuna haja kwa kiongozi wa serikali kutembea mikoani na mali zote hizo? Laptop 2, silaha za moto 2, simu 3, dola 5,000, madafu milioni 2.5!!!

    Nasikia kama harufu ya ufisadi vile!!!

    ReplyDelete
  3. Ankal huyu Mheshimiwa atakuja kuibika bure hapo baadae. Kama alikuwa na washauri wazuri wangemshauri tokea mapema kuwa asikutane na waandishi wa habari na hata kuwapeleka hotelini kufafanua kilichompata. Angekaa kimya tuu polise "wafanye uchunguzi" wao.

    Hii biashara ya kutapatapa kwenye vyombo vya habari kujaribu kujisafisha (sijui anajisafisha kwa umma au kwa mkewe) itakuja kutokea puani. Wanasema hakuna siri ya watu wawili na ukweli utakuja kujulikana tuu. Yeye angejikalia zake kimya. Yaliyompata yamewapata wanaume wengi tuu tena uswahili kweupeeee.

    ReplyDelete
  4. Mh.Malima alikua ziarani au matembezi ya kawaida? Laptop 3 za nini????????? Simu sawa kama ana mitandao mingi. Dollar 4000 ndani ya nchi??? Kuna maswali mengi. Alipoibiwa alikua amelala au nje ya chumba?

    ReplyDelete
  5. wewe unaesema unasikia harufu ya ufisadi labda hujui mafisadi

    mtu kama mh malima kuwa na vitu au pesa kiasi cha milioni 23 au hata 50 sio kitu cha kumuita fisadi

    pesa hizo ni pesa kidogo sana ambazo mfanya biashara mdogo anaweza kuwanazo sembuse mtu kama malima ambae ni kiongozi na pia ni mfanya biashara acha ujinga wewe

    mafisadi wanajulikana wanaochota mabilioni ya hela na sio milioni 23 hata mimi ninaeandika huu ujumbe hazinishindi hizo sasa nikipata kazi ya ujumbe wa nyumba kumi na ninamiliki milioni 50 zangu utaniita fisadi?

    pambaaaaaaaaaaaff

    pole sana mh malima

    ReplyDelete
  6. Yale yaleee....Mdau-NYC, USA

    ReplyDelete
  7. Hata mzungu akija kwa utalii habebi vitu kama hivyo,hii yako muheshimiwa imekuwa too much.Yaani watu kama sisi choka mbaya,unazidi kutuumiza kiongozi kuwa na mali yote hiyo,,just Dar to Moro,,na ikiwa nje ya nchi unakwenda na milioni ngapi?,kweli hii ni hatari,,otherwise ulikuwa unampelekea mtu kumuuzia hiyo mali.

    Mtanzania muathirika wa Mafisadi

    ReplyDelete
  8. Kwa nchi za wenzetu kama huku UK, kwa mtu kutembea na mali nyingi kiasi hiko, maswali huanza e.g is it miney laundering? drugs? etc. na lazima watakufuatilia, whether kigogo or not

    ReplyDelete
  9. Kwa nchi za wenzetu kama huku UK, kwa mtu kutembea na mali nyingi kiasi hiko, maswali huanza e.g is it miney laundering? drugs? etc. na lazima watakufuatilia, whether kigogo or not

    ReplyDelete
  10. Kuna kitu kimejificha ni vile tu taasisi zetu zinatumiwa vibaya kisiasa. Ukweli haujasemwa kabisa. Haiingii akilini jambazi aingie sehemu kama hiyo na kufanya yaliyofanyika hapo!
    Cha zaidi ni jambazi gani ataacha mtaji(bunduki) aliyoikuta ipo tu wakati huwa wanateka hata askari na kuwanyanga'nya? Hii nchi inazidi kuwa corrupt na bahati mbaya jeshi la polisi linatumika kuficha huo uozo bila kujua wanazidi kupoteza uaminifu kwa jamii ambayo ndiyo waajiri wao na kucover up kwa hawa watu wanaofanya mambo machafu.

    Uwezekano mkubwa kwamba waliokamatwa wanabambikiwa kesi tu ili mheshimiwa asafishwe kwani wizi uliofanyika moja kwa moja una dalili zote kwamba ulifanywa na changudoa aliyeingizwa kwenye hicho chumba na mambo yote ya kuvunja madirisha ni fixture tu ili tuamini kuwa wameingia watu.

    ReplyDelete
  11. Jamaa naona alikuwa mkao wa kukimbia nchi nini? Kila kitu alikuwa nacho mpaka silaha za kutosha au alikuwa mwindaji?

    ReplyDelete
  12. Jamani vitu vyote hivyo vya nini hapo morogoro tuu!!!!!!!mambo mengine kweli hayaeleweki kwa mtu mwenye akili timamu.

    ReplyDelete
  13. Mimi pia nasikia harufu ya ufisadi...eti hakuwa na SMG, wanamaanisha kwamba alikuwa na mchine ya kuulia(bastola, bunduki, n.k).
    Huyu ni kweli alikuwa anafanya mambo na mwanamke na huyo mwanamke ndio amefanya mpango vitu vimeibiwa vikapelekwa kwake. Ila kama kawaida viongozi wabongo wanataka kuficha ukweli. Wewe waziri tu kubali kwamba ni mdhidhi(sio mwaminifu kwa mkeo kama umeoa)ndio maana una simu nyingi...alafu laptop 3 jamani du kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  14. Kaka Michu, mbona mie sielewi? unajua angekuwa mwizi mzoefu hawezi kupeleka vitu kuhifadhi kwa mwanamke! inaonekana 'aliyeiba' vitu hivi ni Mwanamke mndio maana akapeleka kwa mmwanamke. Tuweke sawa Mkuu.

    ReplyDelete
  15. Sina uhakika kama nyie mnaouliza ni watanzania na mmeishi Tanzania kwa kipindi cha karibuni. Simu tatu ni kawaida sana, maana kulingana na gharama za kupiga simu kuwa juu, mtu anakuwa na simu kulingana na idadi ya line za simu alizo nazo. Laptop mbili ni kawaida pia. Maana mwendo huu wa mchina china, hauwezi kuamini laptop moja. Lazima uwe na mbili ili moja ikikwama njiani, nyingine ikukwamue. Silaha za moto, kama kweli anazimiliki kihalali, inafaa awe nazo muda wote. Maana kama akimwachia mtu, na bahati mbaya zikatumika ktk uarifu, yeye ndiye atawajibishwa. Suala la pesa, bado naona si nyingi sana, maana hatujui sababu hasa iliyomfanya kuwa hotelini. Mmeshaambiwa hotel ya kitalii, kutumia dola 300 kwa siku kwa hotel za namna hiyo si ajabu. Naomba kuwasilisha

    ReplyDelete
  16. Hapa ni au waandishi wnatuchnganya,au Polisi anatuchanganya kwa kutetea.Huwezi kuamini huyu waziri kuwa kweli alikuwa hotelini kwa vitu vyote hivyo.

    Nadhani hayo ni mzingira ya nyumbani si hotelini.Vitu vyote hivyo utakuwaje navyo hotelin!Hata tajiri wa kupindukia huwezi kumkuta na vitu hivyo hotelini.Laptop tatu!bunduki mbili!Ni mtalii au kenda kuuza,au alikuwa nyumbani?

    ReplyDelete
  17. Haiji akilini jamani du!! Laptop tatu alikuwa anafanyia nini huko hotelini? Simu tatu za nini?Bastola mbili za nini zote? na pesa zote hizo za nini kutembea nazo wakati ana kadi za bank?

    Sidhani kama alikuwa kikazi zaidi ya kibiashara na kifisadi.

    ReplyDelete
  18. Something fish kwenye hii habari. Safari ya kikazi kutoka Dar kwenda Morogoro mabegi matatu ya nguo, silaa mbili, fedha kama unahama nchi, na pete ngapi za dhahabu?

    ??????????????????

    ReplyDelete
  19. mh! hapa inaonekana sanaa tupu! mwizi huyo ni wa aina gani akabeba mabegi yote na vifaa vyote bila walinzi au watumishi wa hoteli kufahamu.
    pia waziri vitu vyote hivyo alivyokuwa anavyo alikuwa anahama au anapeleka zawadi mahali. anyway!

    ReplyDelete
  20. Vimepatikana kwa bi mdogo

    ReplyDelete
  21. watu wametetea simu tatu bongo kawaida haya tukubali laptop 3!!!!! kwani hata kama unatumia moddem si unabadilisha tu? dah nadhani muheshimiwa anajua alikuwa anfanya nini but sidhani kama marehemu muheshimiwa kighoma ali malima angeaprove!!!!

    ReplyDelete
  22. Kwani la ajabu gani akiwa na bi mdogo. Pili kama mtu anaunganisha safari kwa nini asitembee na nguo nyingi, kwanza kufua kwenyewe huko mbali maji ya tabu. Huyu Baba ake alifuatwa sana kwa sababu ya jina lake. By the way huyu kwa mama yake ni Iringa hata kama mnafikiria kwamba Baba yake ni Malima. Mwacheni mtoto, wangapi wana mabibi humu. Hata padri fulani ana bibi badala ya mke. Hilo suala ni baina ya yeye na mkewe.

    ReplyDelete
  23. Ingekuwa jimboni kwake tungesema aanwapelekea watu wake,lakini jimbo lingine kabisa!

    Huyu alikuwa nyumba ndogo na baada ya mbao kuharibika kasingizia kuibiwa danganya toto.

    Mtu si alilala kwa hawala,akaenda kituo cha polisi awekwe ili singizie alikatwa na kushikiliwa usiku kucha.

    Malima acha janja ya nyani,tuache tufikirie mambo mengine kuliko kutolea usanii huu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...