Uncle samahani , kwanza pole na pia pongezi nyingi kwa kuuunganisha Uma .
Nimetazama Video ya Young Africa na Azam na kuachwa na Majonzi makubwa . Amini usiamini nilishindwa hata kupata usingizi . Ningefurahi sana kama jambo hili wadau tungelijadili kwa kina haswa kwa sisi wadau wa soka.

Swala hili ni Doa kwetu na aibu kubwa kwa nchi Yetu vile vile kwa Wana Young Africa damu ulimwenguni kote . Hawa ma bwana wadoogo hawafahamu kuwa wao ni mabalozi wa mamilioni ya Wana Yanga Ulimwenguni . vile vile ni vioo vya watoto wanaochipukia , sasa kama baba anakojoa kitandani , mtoto naye afanye nini ?

Bila kukimbilia kutupia lawama kwa TFF au Polisi , kwanza ni kwa hao wachezaji waliotuchafulia jina wana Young Africa , enzi zile kuichezea yanga ni fahari kubwa hata kama haupati kitu haswa ..
Ndio Maana hata Africa Nation Cup inabidi tuchague Timu ya kushangilia ,Tazama majirani zetu Zambia , Kongo - TP Mazembe , siye tunaishia kufanya ujinga tu .

Tafadhali Mjomba tubandikie kibao cha gwiji PEPE KALE.... " Young Africa `` ,angalau kitupoze Roho , enzi zile Yanga ikicheza mtoto hatumwi dukani . Haya mambo ya masumbwi walikua nayo Simba sio sie.

Inapaswa wachezaji wetu wa sasa kupata elimu ya kujielewa pia , jambo kama hilo lingetokea simba na yanga , mashabiki si tungekamatana pia ? yale yale ya Misri ? , Mchezaji Huwezi tu kukurupuka kama kichaa na kufanya ujinga wako kiwanjani , alafu bado unataka kucheza professional Ulaya , Mnawachafua majina ya watanzaia wachache wanajaribu kivyao ughaibuni .

mbona mkipelekwa ulingoni kamasi zinawatoka .
Roho inauma.
Mdau .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Hili swala inabidi lipelekwe mahakamani. Polisi walikuwas wapi wakati mtu anapigwa. Acha mpira, hiyo ilikuwa kumpiga mtu akiwa kazini, ni swalla zito sana. Polisi wanalipwa kulinda umma, nao walikuwa wanaangalia tu.

    ReplyDelete
  2. Shida ni moja tu hapa kwetu mpira unachezwa na watoto ambao wengi wao darasani hawakufanya vizuri. Na hicho walichoonesha hao vijana ndiyo hulka na tabia zao wachezaji wetu walio wengi oneni aliyofanya Haruna Moshi alipokwenda Ulaya si alirudi na visingizio kibao!

    Ukweli ni kwanza wachezaji wetu hawajui hata kwa nini wanacheza mpira na ndiyo maana Taifa hili kutoka hapa tulipo upande wa michezo ni kazi kubwa sana.

    Tutilie sana mkazo kwenye shule za michezo zitakazotumika kulea vipaji na kuwalea watoto tangu wakiwa wadogo wajue mpira ni nini na wao kama wachezaji wana nafasi gani.

    Pole sana mwana Yanga wewe uliyeumizwa na hilo hata ukaleta hoja hii. NAKUPONGEZA Lakini ndugu yangu tuna kazi kubwa sana.

    ReplyDelete
  3. nakumbuka sana yanga ya enzi zile nilikuwa mdogo basi kijijini kwetu watu wengi hufika nyumbani kwetu ili kusikiliza radio

    nyumba yetu iligeuka kama tawi la yanga kila siku yanga inapocheza baba ananipa kazi ya kupanda juu ya paa la nyumba na kutundika bendera ya rangi ya kijani na njano

    miaka hiyo ilikuwa yanga yanga ya ukweli na wachezaji walikuwa wanajituma kikweli sio mambo ya posho

    inasikitisha sana mpira wetu watanzania unazidi kushuka na matokeo yake hatufiki popote zaidi ya kubaki nyumbani.

    ReplyDelete
  4. POLE MDAU. HAO VIJANA WANGETIMULIWA KABISA KLABUNI KWETU!

    ReplyDelete
  5. Kwa taarifa yako mtaani hakuna Yanga Damu hata mmoja anayesikitika zaidi ya kuwaona ni mashujaa kwakuwa tatizo ni refa na ninyi hamtaki kuweka clip ya madudu aliyofanya refa. Yanga wee ee Yanga weee...I love you!! Yanga Hoyee, ila ngumi noma.

    ReplyDelete
  6. YANGA siku zote ni watu wasio na maaadili, tangu lini mtu wa Uswazi akawa muungwana.

    Sasa mbona mpaka leo club haijatoa adhabu yoyote kwa hao unao waita wahuni. Maana nake wachezaji=viongozi=mashabiki.

    Yeboyebo wahid!

    ujadili na nani na we muhuni.

    ReplyDelete
  7. Huyu mdau mwanzo niliona anaongea mambo ya maana,lakini anamliza vibaya.Anasema haya mambo walikuwa nayo Simba!Kupigana wapigane Yanga wewe unaanza kuongelea ya Simba!Wee kichwa boga kabisa.

    Hukumbuki mamabo ya mpira kabisa wewe au unaoongea mambo usoyajua.Yanga ni watu wa vurugu siku zote,wanapenda mabavu na maguvu kuliko akili.Hii ni tabia yao.

    Yanga wametia aibu sana na wanastahili hiyo adhabu.Mkishindwa mpira mnaanza kupigana,halafu na viti mwang`oa vya nini?Chezeni mpira mshinde msitafute kushinda kwa vita.Hamna mpira pale manwaonea vijana wa Azam wanapolisakata soka mwaona aibu halafu mnapigana.

    Badala ya kuomba msamaha mnaanza kusema hayo mambo ya Simba.Ebo!

    ReplyDelete
  8. Viongozi wa Yanga na wachezaji wao wajue vitendo walivyo fanya kwa mwamuzi sio aibu kwao tu ni kwa nchi nzima. Kitendo walichokifanya kimeonekana dunia nzima hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu. Huu ni ushamba wa kutokujuwa mpira maana yake ni nini na wala si uhodari wa kujionyesha umwamba bora waungane na akina Matumla wafanye mazoezi ya masumbwi badala ya mpira. FAT nayo inatakiwa kutoa adhabu kali sio kumfungia mchezaji mwaka mmoja this is criminal case ( in case mwamuzi angeumia au kanguka na kufariki). Mujifunze sio muige musione wenzenu kina Drogba au Weah wanacheza mpira wa kulipwa mkadhani walikuwa wababe huko walikotoka

    ReplyDelete
  9. Pale Yanga kwa sasa hamna wachezaji, wale wote waliomo ndani ya ile timu ni wachawi kwani hawana vipaji vya uchezaji na ndiyo maana wakifungwa wanajihami kwa makonde. Uyanga na Usimba kwishney.

    ReplyDelete
  10. Mdau ametamka kwamba amekosa usingizi. Bila shaka ndio sababu anachachawa na kuanza kuzungumzia mambo ya Simba. Wakati wa varangati hilo kuna mchezaji wa Simba alikuwepo uwanjani?

    Ukweli ni kwamba Yanga wamezoea marefa wa mechi kuingia uwanjani na mbeleko. Kwenye mechi na Azam walikutana na refa anayechezesha kwa haki wakaona wanaonewa. Nani alikuwa anaongoza mechi mpaka wakati vurugu inaanza? Yanga walifunga magoli mangapi yakakataliwa? Jitazameni kwenye kioo. Mnacheza mpira wa gazetini badala ya mpira wa kitabuni ndio maana hata Zamalek chovu ikawashinda kuing'oa.
    Kwa wale wanaotaka kubisha kwamba Yanga hawajazoea mbeleko nawashauri wapekue vitabu vya historia. Yanga waliwahi kufungiwa kushiriki michuano ya Afrika kutokana na kujaribu kumlisha refa mlungura. Hata kipa wao (nimtambulishe kama I.M.) akiwa anachezea timu ya taifa alipata kushauri kwamba timu ya taifa iwe inawashikisha marefa chochote ili kurahisisha kazi uwanjani. Mnadhani atakuwa alijifunzia wapi hii tabia kama sio klabuni kwake?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...