Afisa Habari wa kampuni ya Push Mobile, Sarah Richard akionyesha jezi zitakazoshindniwa katika shindano la Ruka kwa ajili ya mashabiki wa soka wa Uingereza na Hispania.
Meneja wa kampeni ya Ruka ya kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney akionyesha moja ya zawadi ya mpira utakaotolewa kama zawadi katika shindano la la Ruka ambapo washindi wake watapata fursa ya kuona mechi moja za timu sita maarufu bara la Ulaya.
Meneja wa kampeni ya Ruka ya kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney na Afisa Habari wa kampuni ya Push Mobile, Sarah Richard wakionyesha jezi zitakazoshindniwa katika shindano la Ruka kwa ajili ya mashabiki wa soka wa Uingereza na Hispania.


Mashabiki mbali mbali wa soka nchini watapata fursa ya kuona mechi mbali mbali za Ligi Kuu ya Uingereza na ile ya Hispania (La Liga) kwa kwa kushiriki katika shindano maalum lililoandaliwa na kampuni ya Push Mobile lijulikanalo kwa jina la RUKA.
 
Akizungumza katika uzinduzi wa shindano hilo, Kampeni Meneja wa kampuni ya Push Mobile, Rugambo Rodney alisema kuwa mashabiki wanaotaka kwenda kushuhudia zawadi kubwa ya shindano hilo wanatakiwa kutuma ujumbe wa neon “RUKA” kwenda kwenye namba 15555.
 
Rodney alisema kuwa washindi watakaopatikana watapara fursa ya kusafiri kwenda Uingereza na kuona mechi moja kati ya timu nne za huko ambazo ni Arsenal, Manchester City, Chelsea na Livapool na nchini Hispania kuona mechi za timu za Real Madrid na FC Barcelona.
 
“Hii ni fursa pekee kwa watanzania kwenda kuona mechi kubwa zitakazochezwa nyumbani za timu hizo kubwa duniani, tumechagua mechi za nyumbani kwa sababu tunataka kuwapa nafasi washindi waone hamasa za mashabiki wakiwa katika mechi za nyumbani,” alisema Rodney.
 
Alisema kuwa mbali ya zawadi hiyo kubwa ambayo zitahusisha mechi zinazochezwa uwanja wa nyumbani, pia washindi watapata zawadi  mbali mbali kama jezi za timu za Chelsea na Real Madrid zilizosainiwa na wachezaji nyota wa timu hizo kama Cristiano Ronaldo na Fernando Torres na mpira iliyosainiwa na nyota hao.
 
Mbali ya zawadi hizo, pia kutakuwa na zawadi ya fedha taslim shs 60,000 kwa kila siku ya mashindano hayo kwa msimu mzima. Mashindano hayo mbali ya kusimamiwa na Bodi ya michezo ya kubahatisha Tanzania. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. BONGO tambarare badala ya kukuza ushabiki wenye maendeleo bongo,tutakalia hayahaya,Kasumbaaaa !!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...