Salaam Kaka Issa.
naomba mchango huu uunakirishe kwenye blogi yetu hili,na pengine madaktari wetu wakapitia hapa na kuelewa taratibu zilivyo linapokuja suala la madai ya waajiriwa kwa mwajiri sehemu yeyote ile hapa ulimwenguni.
Kaka Issa,katika kutoa mchango wangu hapa kama mtaalam wa mambo ya utumishi na utawala,sitaegemea upande wowote ule uwe wa serikali ama wa madaktari.
Kwanza naomba madaktari wetu wafahamu kwamba palipo na mwajiriwa kuna mwajiri bila kujali kama ujira unaolipwa kama fidia ya kazi aliyoifanya mwajiriwa unalipwa kwa masaa(hourly pay wage) ama kwa mwezi(monthly base pay).
Kwa mantiki hiyo hapo juu ni wazi kwamba kila mwajiriwa anapokubali ajira au anapokubaliwa na mwajiriwa kuwa maombi yake ya kazi yamekubaliwa ni lazima asaini mkataba wa ajira bila kujali kama ni kibarua(cheap labour) ama mwajiriwa chini ya masharti ya kudumu(permanent terms employment)
Nanacho taka kukizungumzia hapa ni makubaliano na masharti ya mkataba unless mkataba uwe haujakidhi kiwango chini ya Labour Laws and Employee Relations ya nchi husika.
Katika sheria hii kuna mambo mawili yaliyoanishwa ama kuelezwa bayana juu ya nini na kipi kifanyike kwenye terms na conditions za ajira baina ya mwajiriwa na mwajiri.
Mambo haya mawili yanagusa na kulenga benefits mbalimbali ambazo ni haki ya mwajiriwa kuzipata kutoka kwa mwajiri wake bila kujali kama masharti ya ajira ni ya labour pay bases ama permanent pay bases.
Mambo haya mawili ni :
1.Faida,ujira ama (fidia)zinazostahili kutolewa kwa mwajiriwa kisheria(legally required benefits) na mwajiri.Zaweza kuwa pesa ama huduma.
Hizi zinashirikisha benefits zote chini ya sheria ya Social Security Fund Act ya Tanzania(1997),Workers compensation Act ya (2008), na Family and leave Act(hapa kwetu vifungu vyake vipo kwenye sheria ya Employment and Labour Relations Act ya 2004.Katika mfumo wa ajira ndani ya nchi yetu benefts zote zilizo chini ya sheria hizo 3 ni za lazima kisheria kutolewa na kutekelezwa na mwajiri kwa mwajiriwa.
Pasipo kufanya hivyo mwajiriwa kupitia vyama vya waajiriwa (Trade unions) wanaweza kumshitaki mwajiri kwenye Mahakama ya Kazi ama Tribunal yeyote inayo husika na usuruhishaji wa migogoro baina ya hizi pande mbili ama sivyo kuanzisha migomo hili kumshinikiza mwajiri,atimize kile kinachodaiwa na waajiriwa au madai yao kwa ujumla ya kipengele hiki.
2.Faida,ujira ama fidia zinazotolewa kwa mwajiriwa kama kipenda roho cha mwajiri(Discretionary Core Fringe Benefits)Hizi ni fidia ama ujira unaotolewa kwa mwajiriwa kama kipenda roho tu cha mwajiri, kumfanya mwajiriwa ajisikie vizuri kiroho,kumuongezea motisha ama kumfanya akabiliane na ugumu wa gharama za maisha.
Hizi zinashirikisha: program za kumlinda mtumishi kama matibabu,anapokoswa ajira,kutojiweza,ulemavu,ajali nk.
Malipo ama ujira wa kutokufanya kazi-Paid Time Off ambao mwajiriwa hulipwa anapokwenda mapumziko,likizo ya ugonjwa ama masomoni nk.
Huduma-hizi ni huduma anazozipata mwajiriwa kama kupata msaada wa chakula cha mchana na familia yake kutoka kwa mwajiri,usafiri(kupewa gari ama pikipiki,huduma za kushiriki mashindano ama michezo mbalimbali ya kumfanya mtumishi awe safi kimwili na kimawazo.
Kaka Issa nimeeleza vya kutosha juu ya mahusiano yaliyopo na yanayotakiwa kuwepo juu ya fidia anazostahili mwajiriwa kutoka kwa mwajiri wake.
Hoja yangu ni ipi kwa kuhusisha mgomo wa madaktari wetu?
(A)Naomba madktari wajue na kutambua kuwa kuna fidia ama stahili wanazopewa kutokana na kipenda roho cha mwajiri.(Discretionary Benefits).
(B)Naomba madaktari wetu watambue pia kuwa kuna fidia ama ujira wanaopaswa kupata kisheria bila kujari mwajiri ni serikali ama mtu binafsi.Kama kuna fidia ama ujira niliouainisha hapo juu wa kisheria na madaktari ama mwajiriwa yeyote haupati,anzeni sasa kuufatilia.
(C)Pamoja na kuwa mtaalamu wa mambo ya utumishi na utawala,hakuna sehemu yeyote niliyoelekwezwa ama kujiridhisha kwa kusoma kuwa,mwajiriwa ana mamlaka ya kisheria kumlazimisha mwajiri wake kumfuta kazi,kumfukuza kazi ama kumsimamisha mwajiriwa mwenzie kwa sababu hatendi majukumu yake vizuri kama wanavyo dai madaktari wetu.
(D)Nawaomba madaktari wetu wapitie madai yao ya mwanzo upya hili wajiridhishe wazi kwamba ni mambo yapi wanapaswa kuyasimamia kudai haki na madai yao ya kisheria.
Sheria ya kazi na mahusiano kazini ina mipaka yake linapokuja suala la madai ya mwajiriwa.
Hitimisho.
I:Nawaomba waaajiriwa watambue haki zao hizi katika makundi niliyo yaainisha hapo juu.
II:Nawaomba madaktari wadai madai yao ambayo wanapaswa kupewa kisheria bila kuathili upande wa pili wa wananchi wanaohitaji huduma zao za kitabibu.
III:Nawaomba madaktari wasiendelee kuishinikiza serikali (mwajiri)kuwafukuza kazi ama kuwasimamisha waajiriwa wenzao.Mh.Waziri na Naibu Waziri.
IV.Naiomba serikali itimize ahadi zake zote ilizotoa kwa waajiriwa wake ikiwa ni pamoja na kuwaboreshea zile discretionary benefits.
"Kila jambo linawezekena ila approach inaweza kufanya lisiwezekane"
Joachim K.Global
Asante kwa usaidizi huu kitaalam. Madaktari wajue pia kuna utaratibu wa migomo katika sheria na wanazuiwa kisheria kuingilia au kuvunja haki za mwajiri.
ReplyDeleteAsante sana kwa elimu,siyo madaktari tu hata waajiriwa sehemu nyingine tumepata 'shule' kwa namna moja au nyingine.Madaktari ni wasomi sidhani kama hawafahamu hicho ulichokiandika..Wanafahamu sana.nina uhakika chama chao kina wanasheria wa kila aina.Hawakurupuki kufanya wanachofanya..ndiyo maana wanafanya kwa kujiamini.Kuna tatizo hapo linatakiwa lipate ufumbuzi kwa majadiliano.Taratibu hao wanatugawia dawa za moto kila siku wasije kutumaliza..
ReplyDeleteDavid V
asante kwa kutuelewesha mtaalam,madaktari wenzangu huu ni ujumbe mathubuti tuufuate!
ReplyDeletemadaktari wapitie upya madai yao mgomo kwa gharama ya maisha ya binadamu wenzao haikubaliki wanasheria waangalie namna ya kuwashtaki kwani kudai haki kwa kuvunja haki za wengine si sawa.TUTAWAUNGA MKONO TU MNAPO DAI MASLAI YENU KIUSTARABU.
ReplyDeleteDuh, yaani kama vile unayoongea ni mageni sana masikioni mwa waajiriwa. Arobain ya upuzi wa serikali ikifika hakuna siasa mkuu...Hata hivyo tunashukuru kwa maelezo yako.
ReplyDeleteHuyu katumwa si bure.
ReplyDeleteushuri mzuri...ila suala la kushinikiza mawaziri wajiuzuru si kwa maslahi ya madaktari tu, bali ni kwa maslahi ya taifa zima...swali langu langu kwako mtaalam..kwani ina maana hata sisi raia wa kawaida haturuhusiwi kushinikiza waziri kujiuzuru kwa kuwa we are not part to the contract?
ReplyDeleteHuyu mwandishi katoa story ambazo ziko kwenye vitabu, Madaktari wana kila haki ya kuomba mazingira mazuri na vitendea kazi ambazo ndio kigezo kikuu katka madai yao.
ReplyDeleteMaongezo ya mshahara ni nyongeza tu ya madai yao.
Hivi nyie Watanzania mnajua ni madaktari wangapi vijana wanaacha hiyo kazi kutokana na mazingira mabovu ya kazi na ukosefu wa vitendea kazi pamoja na malipo madogo? Madaktari wote niliomaliza nao form six PCB wameacha udaktari na kuingia katika fani zingine. Au kwenda nchi zingine.
Nitanzania pekee ninayo ijua mbunge anamzidi Daktari mshahara na ubora wa maisha. Ni aibu kuona mnawapinga watu ambao wanagombea haki za watanzania wote. Hii ni kwa manufaa ya umma. sjaona nchi yeyote ile inapingana na Madaktari katika dunia hii ya leo. Wakati nchi zingine zinawatafuta hao madaktari nyie mnawanyanyasa.
Ushauri wangu ni kwamba kama huoni sababu kwanini wanalalamika NYAMAZA, waache wapambane na hao viongozi wa nchi wananchi wapate huduma nzuri za afya.
Acheni siasa kwenye suala la afya ya wananchi walio wengi.Kama nilivyosema mwanzo, wengi wenu inawezekana hata hamuendi kwenye hospitali za serikali.
VITA ISIYO KUHUSU INAKUUMAJE?
Asanteni,
Makongoro Wassira
Ni ufafanuzi mzuri wa kitaalam, ahsante sana, Kama alivyochangia alotangulia, kuna tatizo la serikali kutojali ama kutotekeleza makubaliano Yao na madaktari, kuwajibishwa kwa hao viongozi aw wizara lilikua moja ya masharti kwenye makubaliano Yao ya awali, waziri kujiuzuru hakuhitaji bajeti, watanzania hatuna utamaduni wa kuwajibika tunapoboronga!
ReplyDeleteHAIWEZEKANI MAWAZIRI WANAOTUHUMIWA AU KULALAMIKIWA WAKAWA SEHEMU YA MAJADILIANO KATI YA MADAKTARI NA SERIKALI!! TAFADHALI HAO MAWAZIRI WAPISHE ILI TUWEZE KUFIKIA MWAFUAKA TUKIWA NA AMANI MIOYONI MWETU.
ReplyDeleteHili ni tatizo kwa hizi taaluma zinazosoma kitu kimoja tu. Madaktari ni viongozi kwa mazingira yao ya kazi lakini hawasomi uongozi, fedha na sheria za kazi japo kwa intro. hili ni tatizo maana uelewa wao unajionyesha kwenye baadhi ya maoni hapa.
ReplyDeleteMadktari wajue kuwa hata sisi tunajua ni haki yao kihalali na nini sio haki kwa mujibu wa sheria zilizipo. IKIBIDI TUTAUNGANGA NA SERIKALI NA SISI TUTAWANYIMA HUDUMA MADKTARI POPOTE TUTAKAOWAONA KUANZIA KUWAFUKUZA KWENYE NYUMBA ZETU WALIZOPANGA, KUWAWEKEA MAFUTA KWENYE MAGARI, KUWAUZIA VITU KWENYE MADUKA N.K maana huwezi kumchekea mtu anayekuua kwa kisingizio cha maslahi. NADHANI SERIKALI IAMUE KUWAFUTA KAZI WOTE NA KUFUTA PENSHENI ZAO, VYETI VYAO NA KUWAPIGA MARUFUKU KUFANYA KAZI NDANI NA NJE YA NCHI. NI DAKTARI GANI KASOMA KWA HELA ZAKE? HAO WANOSHABILIA WANAJUA KUWA HAWA JAMAA WANATAKA TUTOZWE KODI ZAIDI ILI WAO WAISHI KWA RAHA KULIKO WENZAO WENYE ELIMU HATA KUWAZIDI WAO?
Makongoro Wassira lazima ana matatizo kichwani....
ReplyDeletehivi ulifikiria wananchi wanaathirika vipi haswa wale wasimudu huduma za kulipia???
MCHANGO MZURI
ReplyDeleteLAKINI KWAKUWA LENGO LA MTALAAM HUYU TUNALIJUA TUNAWAOMBA MADAKTARI WAZIDI KUKAZA BUTI, HATUWEZI KUZUNGUMZIA UTAWALA BORA KILA SIKU AND YET HATUJAWAHI KUONA MTUMISHI HATA MMOJA AKIWAJIBIKA KWA MADUDU ALIYOFANYA. KAMA NAKUMBUKA VIZURI JANA TAREHE 7/3/2012 MHE. RAIS ALIKUWA ANAZUNGUMZIA MAMBO YANAYOHUSU UTAWALA BORA AFRIKA, HIZO NGUVU ZA KUZUNGUMZIA UTAWALA BORA ANAZITOA WAPI WAKATI HAKUNA HATA MTUMISHI WAKE MMOJA ANAYEKUBALI KUACHIA NGAZI KWA VITENDO ALIVYO VIFANYA.
NAJUA KUNA ATHARI ZITAJITOKEZA, SO LET IT BE A LESSON TO THE GOVT
Huo ufafanuzi wako ni sahihi lakini muajiri ana wajibu wa kuhakikisha mahusiano mema yanakuwepo kati ya uongozi (uliowekwa na muajiri) na waajiriwa katika sehemu ya kazi hata kama hilo halijasemwa kwenye sheria. Ni common sense tu.
ReplyDeleteMadaktari hawataki au hawana imani na huo uongozi uliopo. muajiri makini angeuondoa uongozi huo. Kwani Mponda na Nkya tu ndo wanaweza kuongoza wizara hiyo? mbona madaktari waliobobea kwenye taaluma zao na walio na uwezo wa
wa kuongoza wamejaa lundo?
Hili sakata lote linasababishwa na uongozi usio makini
Asante sana kwa ushauri wako wa kitaalam,ata mimi ningependa madaktari wajikite kwenye madai yao ya msingi ya uboreshaji wa mazingira ya kazi,suala kuwajibisha viongozi waiachie serikali Rais yeyote asingependa kumwajibisha waziri kwa kushurutishwa bila kujiridhisha na tuhuma,nionavyo mimi hapa kila upande unataka kujiosha kutokana na madhara yaliyotokea,ni vyema serikali na madaktari wakakaa meza moja na kutafuta ufumbuzi.
ReplyDeletemadaktari wakifanyakazi zao kwa unyonge watakufa wengi bila jamii kujua kwani tutafikiri ni mpango wa mungu kumbe wataalamu wamenuna, lakini wakigoma tunaweza kuokoa wachache kwa kuwapeleka hata kwenye tiba za asili kwani hali halisi tutakuwa tunaijua. muuaji wa kweli hapa ni serikali kwani inaidhinisha watu wawili wawe sababu za vifo vya watanzania, kama ni lazima watu hawa wawili wawe viongozi kwenye serikali hii basi wawatoa wizara ya afya wapelekwe wizara nyingine kwa vyeo vyao hivyohivyo, kwa kufanya hivyo wao wataendelea kuwa mawaziri kama wanastahili kuwa mawaziri, (maana wanaweza kuvurunda hata huko), na madaktari watarudi kazini maisha ya watu yatanusurika.
ReplyDeleteNaomba niufahamishe umma wa Watanzania kwa nia ya dhati kutoka moyoni mwangu bila kumudhiaki Bwana Mungu kwamba,hiki nilichokiandika hapa,sijatumwa na kiumbe yeyote,taasisi yeyote,kampuni yeyote,wakala yeyote,serikali yeyote ama kikundi chochote kilichoko chini duniani ama juu mbinguni.
ReplyDeleteNimesema kwamba mimi ni mtaalam wa mambo ya utumishi na utawala.Ukitaka kunifahamu zaidi wasiliana nami kwa mail id hii, thejunior.global@gmail.com
Joachim K.Global.
joachim umeeleza mambo mazuri lakini na0na ulicho gusa ni robo tu ya madai ya madakitari hii inanipa maana yakwamba huna uelewa wa kina wa madai ya madakitari. Madaktari wameyapanga mdai yao tena kwa mtiririko mzuri tu kwanza nikuwaondoa hao watendaji walio shindwa kutatua matatizo yao ya mda mrefu,kutengenezewa mazingira mazuriya kazi na mi nafikiri kipindi ulipo kua ukiandia hayo uliyo yandika ungelikua ukifikiri na kutafakari jinsi mazingira ya kazi ya hospitali nyungi za serikari zilivyo wagonjwa kulazwa zaidi ya mmoja kwenye kitanda kimoja, ukosefu wa madawa na vitendea kazi vingine...
ReplyDeleteHilo la madai nao wanalielewa ya kwamba ningumu kwa sasa kupatikana kwa pesa...
mi kwa upande wangu naona ni waendelee kukaza uzi mpaka kieleweke..
In theory u r right, but in practise doesn't work like that in tanzania.
ReplyDeleteHalafu eti uende mahakama ya kazi ukadai haki yako against mwajiriwa, kesi ya nyani umpelekee ngedere utapata nini? mwajiri anayetumia nguvu lazima na mwajiriwa adai kwa kutumia nguvu.Historia inajirudia pale pale, wapi wafanyakazi walioajiriwa na serikali wakaomba madai yao kwa amani na wakasikilizwa na kutekelezwa?
Jamani Madaktari acheni ubishi kwa hili mmechemsha.Mnawakomoa wasio na hatia na kudhurumu maisha yao bure bila sababu za msingi jiulizeni tangu mlipoanza mgomo ni Wabunge wangapi au Mawaziri wangapi wamekufa kama si walala hoi.Acheni hizo daini haki zenu kistaarabu bila ya kuua au kusababisha vifo kwa watu. Je Polisi au wanajeshi nao wagome na kuanza kutumia mitutu waliyopewa na Serikali kutupiga risasi mtasema ni wendawazimu? Nyinyi tumewapa dhamana ya kututibu sio kutuuwa jaribuni kuelewa na kuwajibika na dhamana mliyonayo sio kujisahau na kuanza kutuua kisa mmesomea udaktari sio haki kwa namna yoyote ni ufinyu wa mawazo huo.Hivi wote tungesomea udaktari si ingekuwa vurugu nani atafanya kazi nyingine? Acheni usaliti wa maisha ya ndugu zenu. Mimi sijatumwa wala sijui kupendelea kwa hilo mmekosea ndugu zangu hakuna haki isiyo na wajibu.
ReplyDeleteKama mapatano yalifikiwa ya kuwa Waziri na Naibu wake wajiuzulu je sasa wanangoja nini?
ReplyDeleteUkweli wa mambo maji yamezidi Unga lakini Mamlaka inazidi kuvimbisha kichwa kwa ubishi usio na faida!