Na Mery Ayo,Arusha

HATIMAYE ule mgogoro ambao ulikuwepo baina ya vijana wa kabila la kimasai na waumini wa kikristo katika eneo la Elerai wa kuwatembeza mitaani baadhi ya waumini ambao wanapingana na mila hiyo umekwisha na badala yake wamefanikiwa kuweka misimamo ambayo haitaweza kuwaumiza jamii ya kikristo pamoja na kabila la wa masai.

Muafaka huo ulifanikiwa kufikiwa mapema jana katika eneo la Elerai ambapo pande zote mbili ambazo zilikuwa zinakinzana kuhusiana na mila ya Tohara kwa njia za kienyeji hali ambayo ilisababisha watu wengi kutembezwa mitaani wakiwa watupu

Akiongea katika kikao hicho mzee wa boma la kimasai, Bw Labani Konina laizer Alisema kuwa mila hizo zinawakandamiza sana baadhi ya watu ambao ni wa kabila hilo ambao hawaamini kwa maana hiyo ni bora mila kama mila ibaki kama iliuvyo na wala si lazima kufuatwa

Aliongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa matukio mengoi ya kutembezwa umbali mrefu kwa wale ambao wanakinzana na tohara za kienyeji familia nying sana zimekuwa katika wakati mgumu sana ambapo kwa sasa ni bora kanisa kama kanisa liwe na msimamo dhidi ya mila na pia anayetaka mila pia asibugudhiwe na mtu

"jamani kilichotokea ndugu tusamehane lakini hapa ni kwamba mtu asiingilie imani ya mtu kwa kuwa unapojaribu kuingilia imani ya mtu ndipo yanapotokea matatizo kama haya ya kutembezwa mitaani wakiwa watupu na pia hapa anayekwenda kanisa wazee wenzangu tuwaache na anayekuja huku aje lakini na sisi pia tuweze kuangalia mila ambazo hazina umuhimu kwetu tunapeleka wapi nchi"alisema Bw Laizer

Akiongea kwa niaba ya viongozi wa makanisa ya kikristo ambao walikuwa wanapinga na kukataa mila hiyo Bw Noel Urio alisema kuwa walichokubaliana wao kama wao ni kuhakikisha kuwa wana simama katika ukweli ambao utaweza kuokoa jamii hasa ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuachana na kuabudu mila ambazo zina madhara makubwa sana

Bw Noel aliongeza kuwa kwa sasa jamii ya kimasai ambayo ipo ndani ya madhehebu mbalimbali haitaweza kubugudhiwa dhidi ya Mila hiyo ambayo hapo awali ambao walikuwa hawaifuati walikuwa wanapewa adhabu kubwa sana ambayo inawapelekea kuwadhalilisha wao na familia zao.

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata hiyo ya Elerai Bw Obedi Meng'oriki alisema kuwa bado mila hiyo ya Tohara kwa njia ya kienyeji ina dhalilisha sana kwa hali hiyo jamii hiyo ya Kimasai inatakiwa kuangalia hata hali ya Maisha ya sasa na kuachana na mila ambazo zimepitwa na wakati.

Bw Obedi aliongeza kuwa bado kuna watu ambao wana nganinia mila za hapo zamani na kutokana na wao kungangania mila hizo wamekuwa chachu ya umaskini ndani ya jamii zao hali ambayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana hata familia zao kuteseka sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Wamasai ni watu tunaopenda mila, desturi na utamaduni wetu. Wamasai tunakubali mabadiliko. Lakini hao wanaotaka tubadilike lazima watueleze mambo kwa busara na mantiki badala ya kuja kwetu kututukana na kutudharau. Wamasai wengi sana tumeacha kukeketa ndito (wasichana) wetu. Kinachotuudhi ni kuona Watanzania wazawa wenzetu wakija kwetu kututukana na kutuita washenzi. SISI SI WASHENZI. Hatutaki tena kutumiwa vibaraka na kanisa la kkkt kuja kututukana

    ReplyDelete
  2. Mimi binafsi nawapenda sana wamasai kwa mila zao zile nzuri, Lakini nawachukia sana pale wanapo mlekebisa Mungu aliye dizaini maumbile ya mwanamke, kwanini mnakata ndimi{vinembe}za wanawake ambazo kwa vyovyote ndizo wanazotumia kuonjea utamu wa chakula, hayo mnadhani ni mazuri, kwanza mnamlekebisha Mungu mlimsaidia kuumba? mimi niulize kwanza, unasema wamasai mliowengi mumesha acha kukeketa na hao wasio acha wanasubiri nini? au mnataka mpaka tutunge sheria itakayo wafunga kwa kosa hilo ndo mtaacha huo ushenzi wenu maana huo ni ushenzi unamkataje mwanamke kinembe, kwanini ninyi wanaume msikate ndimi zenu huko midomoni tuoni kama itawapendeza, Mungu ameumba kila kitu kwa maana maalumu.wala msisingizie eti mwanamke akiwa na kinembe anakuwa malaya hiyo siyo kweli, umalaya wa mwanasmke unatokana na au humtoshelezi kimapenzi ya kitandani au tu tabia yake mbaya, kwahiyo dawa ni kuwatosheleza hamu zao na muwafundishe tabia njema (win their minds}na siyo hayo mnayofanya na ndo hayo yanayo tutia sisi hasira na kuwatukana, tena hiyo ni kidogo, tungeweza kuwapiga na kuwatupa jela kwakosa hilo.
    mimi binafsi simtaki kabisa mwanamke asiye na kinembe, kwasababu hawezi kufurahia tendo la ndoa au ngono utakavyoita mwenyewe, kinachoendelea kwa mwanamke aliyekatwa kinembe wakawa wa tendo ni uigizaji tu ukweli ni kwamba anasikia maumivu badala ya utamu.ndo nini siyo upumbavu huo. achani wote kabla hatujawashukia na tafarani zingine zaidi ya matusi ambayo inaonekana hayawatoshi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...