Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano,Mh. Samia Suluhu Hassani akipata maelezo kutoka kwa Afisa mipango wa wilaya ya mkoani,Bw. Amour juu ya mradi wa usambazaji umeme huko magomba katika jimbo la Mkanyageni mkoa kusini Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano,Mh. Samia Suluhu Hassani akizunguza jambo na Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni,Mh. Habib Juma Mnyaa mara baada ya kumaliza kuangalia usambaji wa umeme katika vijiji vya jimbo hilo ambao Umefadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo (CDCF).
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano,Mh. Samia Suluhu Hassani akionyeshwa Bwawa wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Ufugaji wa Samaki unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) huko Chambani Kisiwani Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano,Mh. Samia Suluhu Hassani akivuka Mtaro wakati wa ukaguzi wa Ufugaji wa Samaki unaofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) huko Chambani katika Ushirika wa kwa dawa kichimba chambani kisiwani Pemba.
Bi Amina Khamis ambaye ni mfanya biashara ndogo ndogo katika Soko la mbogamboga liliopo Wawi,Akimpa Maelezo Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mungano,Mh. Samia Suluhu Hassani kuhusu hali ya biashara katika soko hilo lililojegwa kwa ufadhili wa TASAF.
Hivi huyu mama ni mfanyabiashara serious kweli mbona kama anatania. Bidhaa zenyewe za kuhesabu au ilikuwa ni kwa maonyesho kwa mheshimiwa?
ReplyDeletena mimi nimejiuliza hivyo hivyo!!
ReplyDeleteInaonesha wazi kuwa masoko kama haya yanayojengwa na TASAF ama ni kisiasa au kupoteza rasilimali pesa kinyume na malengo.
ReplyDeleteAma TASAF imeshindwa kusimamia vizuri rasilimali wanazozitoa kwa wananchi kwa malengo mazuri tu, lakini tija yake ndio hii tunayoiona pichani.
Serikali washabihisheni wananchi watumie rasilimali walizowekewa.
Hivi wachaniaji wa wawili wa kwanza hamjawai kuona biashara za magengeni nini? Mtu anaweka mafungu matatu ya nyanya na meingine matatu ya vitunguu anakuambia anafanya biashara. Msimlaumu huyu mama mtaji ni shida na hapo labda katumia hela yake ya chakula kwa siku mbili kununua hizo bidhaa anazouza.
ReplyDeleteKwani hamjui maana ya display? Bidhaa zote siyo lazima ziwe mezani. Mfano ni kama duka la vitabu, pale ambapo display kinawekwa kitabu kimoja kimoja, lakini ukihitaji unachukuliwa 'store'. Hapo mtu akihitaji fungu moja anauziwa toka mezani, lakini akitaka zaidi, anatafutiwa kutoka kwenye gunia lililopo chini ya meza, ijapokuwa wadau hamlioni.
ReplyDeletePANA 'MZIMU' WA SIASA HAPO, SIO BURE!
ReplyDeleteKudorora kwa Biashara ktk Soko hapo Pemba kunatokea kwa sababu kubwa nyingi lakini hizi 2 ni za kwanza:
1.HALI HALISI YA KIUCHUMI KISIWANI:
Hali halisi ya Kiuchumi Kisiwani Pemba ni tete kulingana na Wananchi kuwekeza zaidi ktk Siasa za Ukinzani zaidi ya kuwekeza katika Biashara za Kiushindani.
2.HUJUMA ZA KISIASA:
TASAF imefanya umamuzi mzuri wa kutumia fedha za Mfuko kuwekeza ktk Ujenzi wa Soko ili kutoa msukumo ktk mzunguko wa Kiuchumi kisiwani,kuwakwamua Wananchi kwa kutoa Ajira ktk sekita ya Biashara Ndogo ndogo.
KWA VILE MFUKO WA TASAF UPO CHINI YA SERIKALI, HIVYO WANANCHI WALIO WENGI WA PEMBA WAMEONA WATUMIE HUJUMA ZA KISIASA ILI KUKWAMISHA MPANGO HUO, KWA KUWEKEZA KTK UKINZANI WA KISIASA BADALA YA KUONGEZA USHINDANI WA KIBIASHARA NA KUJIKWAMUA KIUCHUMI!
Halafu Ohhh, Muungano hatuutaki!
ReplyDeleteSoko Kisiwani Pemba jeupeeee kwa vile Wapemba wote wapo Bara kuanzia Dar Es Salaam, Morogoro, Tanga, Iringa, Mbeya, Arusha na Mikoa mingine wakifanya biashara mustarehe bila kuulizwa Vibali vya Biashara, Pasipoti wala Karatasi za Uhamiaji kwa vile wao ni Wananchi halali wa nchi inayoitwa JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
JE WAPEMBA HAMUONI HIYO NI NEEMA NA FAIDA YA MUUNGANO KUONDOKA KWENU PEMBA MKAFANYA BIASHARA BARA MUSTAREHE?
AU MPAKA TUWAPATIE WANAWAKE WA KUOA?,,,HIYO NI NYIE TU WENYEWE HAKUNA ANAYEWAZUIA MINDHALI MPO BARA SEHEMU YA NCHI YETU TANZANIA NI NAFASI YENU TU NA NDIO FAIDA YA ZIADA YA MUUNGANO!