Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawako pichani) juu ya uteuzi wa wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii (TTB) kuanzia tarehe 23 Machi, 2012, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Bw. Ibrahim Mussa. 
=======    =====  =====

Mhe. Maige ATEUA BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii (TTB) kuanzia tarehe 23 Machi, 2012.

Uteuzi huo unafuatia Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete kumteua Balozi Charles A. Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTB mapema wiki hii. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi hiyo itakayodumu kwa miaka mitatu ni pamoja na:-

  1. Prof. Isaya Jairo PhD, Mhadhiri wa Biashara na Uchumi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha, IFM;

  1. Ndugu Teddy Mapunda, Mtaalamu wa Masoko (Marketing) na Afisa Uhusiano Serengeti Breweries Limited;

  1. Ndugu Samwel D.I. Diah, Mtaalamu na Mdau wa Biashara na Utalii na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Travel Co. Limited;

  1. Mhe. Kaika S. Telele (Mb), Mbunge wa Ngorongoro na Mdau wa Utalii na;

  1. Mhe. Abdulkarim Shah (Mb), Mbunge wa Mafia na Mdau wa Utalii.

Habari na picha ni kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Maliasili na Utalii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivi kwa nini bado hawa wanasiasa wanateuliwa kwenye Board? Kwa nini Mbunge ateuliwe kwenye Board? Hili ni kosa kubwa sana katika utawala!

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza nakubaliana na wewe, hivi kwa nini Rais aruhusu uteuzi wa Wabunge katika bodi?

    Watanzania tuko wengi tunaoweza kuchukua nafasi hizo, na baadhi yetu hatuna kazi, kwa nini usitupe nafasi na sisi? Au ndio kujazia mfuko wa allowance ya laki mbili?

    ReplyDelete
  3. Sasa yeye waziri afanyeje, kama 'sheria' inasema kuwa lazima kuwepo na uwakilishi toka bungeni? Lalamikeni sheria zibadilishwe, siyo kulaumu tu bila kujua kikwazo kilipo kwanza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...