Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Airtel,Jane Matinde akimkabidhi mshindi wa milioni 30 wa promosheni ya Nani Mkali,Bw.Abdi Ibrahim Mohamed mfano wa hundi ya sh. Milioni 30. Akishuhudia katikati ni Ofisa Mawasiliano wa Kampuni ya simu ya Airtel,Dangio Kaniki .

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imemzawadia mshindi wa kwanza wa mwenzi wa promosheni ya "Nani Mkali" Bwana Mkali Abdi Ibrahim Mohamed mkazi wa Muheza Tanga pesa taslimu shilling milioni 30.

Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Ofisa Mawasiliano wa Airtel Bi Dangio Kaniki alisema" leo tunayofuraha kumtangaza mshindi wa mwenzi wa shilingi million 30 bwana Mkali Abdi Ibrahim Mohamed ambaye amejishindia katika promsheni yetu inayoendelea ya nani Mkali. 

Kama mnavyofahamu tumekuwa tukitangaza washindi wa siku na wa wiki, Airtel bado inawapa nafasi nyingine watanzania kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali".

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, ili kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.

Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.aliongeza Kaniki.

Akiongea mara baada ya kukabithiwa zawadi hiyo Bwana Abdi Ibrahim Mohamed alisema" nachukua fulsa hii kuwashukuru kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kuanzisha promosheni hii na najisikia furaha kuibuka Mkali wa Airtel na kujishindia pesa taslimu shilling milion 30 leo hii.

Napenda kutoa wito kwa wateja wa Airtel kushiriki na wale ambao hawajajiunga kushiriki na kuibuka washindi kama nilivyojishindia leo,kila mmoja ananafasi ya kushiriki na Kushinda kama mimi nimeshinda toka Tanga wilayani muheza hii inaonyesha wazi kuwa nafasi ipo kubwa kwa kila mtanzania Kushinda awe wa mjini au vijijini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Ningekuwa na mamlaka serikalini ningewapa adhabu mashabiki wa yanga pia kwa kuifungia club yao kutumia uwanja wa taifa maana kama walivunja viti hiyo ni dharau kwa serikali na umma wa watanzania kwa ujumla, wajenge uwanja wao na wauvunje viti kama wanadhani ni rahisi kujenga kitu kizuri kama hicho!

    ReplyDelete
  2. mashaalah awowo hongera.huyu bwana mchapakazi sana, nimekula chipsi zake muheza.
    mdau usa

    ReplyDelete
  3. hako ka Kaniki ka Airtel huwa kananikosha sana!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...