Meneja kampeni za CCM,uchaguzi mdogo Arumeru Mashariki, Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Mwigulu Nchemba (kulia) akimnadi mgombea wa CCM jimbo hilo, Sioi Sumari katika mkutano wa kampeni uliofanyika leo, 14/4/12 katika kijiji cha Shambarai, Kata ya Mbuguni 
 Wananchi wa kijiji cha Shambarai, Kata ya Mbuguni, wakishangilia wakati wa mkutano wa kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo.
  Pamela Sioi akimuombea kura mumewe, mgombea ubunge wa CCM, jimbo la Arumeru Mashariki, Sioi Sumari kwenye kampeni zilizofanyika kijiji cha Shambarai kata ya Mbuguni jimboni humo leo.
 Mama Sioi(wapili kulia) akishiriki kuselebuka muziki wa hamasa za Chama, uliporomoshwa katika kijiji cha Msitu wa Mbogo kata ya Mbuguni kabla ya kuanza kampeni za CCM za uchaguzi mdogo jimboni humo leo
 "Tupo na ninyi" wanafunzi wa shule ya msingi Msitu wa Mbogo wakisema huku wakionyesha dole gumba msafa wa mgombea ubunge wa CCM Sioi Sumari ulipowasili kwenye mkutano wa kampeni kwenye Uwanja uliopo jirani na shule hiyo.

  Sioi Sumari akiwasalimia wapigakura wake baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Msitu wa Mbogo
Sioi Sumari akiwaaga wapigakura wake baada ya kumaliza mkutano katika kijiji cha Msitu wa Mbogo, leo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Spika wa Bunge alituambia, ubunge ni umasikini. Hive umasikini ndiyo unaombwa hivyo? Mama Makinda, mimi naomba utueleze zaidi hapo.

    ReplyDelete
  2. yule nae hajui analosema kabisaaaaa.kwanza huko arumeru CCM wamemwaga hela za hatari ili washinde hatuwaaki kabisaaaaaaaa maana nchi inazidi kudidimia maisha magumu kila kukicha,CHADEMA juuuuuuuu yani saivi ni CHADEMA tuuu kila kona,hawa CCM watatuchakachua huu uchaguzi wa mbunge

    ReplyDelete
  3. Hivi Jamani mtu anapokuwa ameolewa ni Lazima aitwe kwa Ubini wa Mume?

    PAMELA SIYOI...kwa nini asiendelee kiutwa kwa Ubini wa baba yake?...!!!

    Nomba mnieleweshe!

    ReplyDelete
  4. Ndege Mbuni ana Saikolijia ya kujidanganya sana!

    ...Pana wakati akikabiliwa na Maadui au tuhuma hutafuta rundo la machanga au vumbi na kuficha kichwa pekee huku mwili ukiwa nje akijidanganya kuwa amejificha!

    ReplyDelete
  5. Siasa,,,ama kweli Sihasa!!!

    Lohhh fitna na Mipango vimetembea sio kawaida!

    ReplyDelete
  6. Kumbe Sioi ana Mke. Basi Kaoa

    ReplyDelete
  7. mwacheni, kijana akapige kelele na Zitto. Akina Zitto wameacha ajira wamekimbilia ubunge angelikuwa CCM saa hizi angekuwa waziri sasa aungoje uwaziri wa uchumi mwaka 2015 mbeli kweli by the time anazowea 2020 keshazeeka.

    ReplyDelete
  8. Kuna umuhimu Asasi za Uwezeshaji wa Kiujasiriamali kama SACCOS, MABENKI,NGO,VIKUNDI VYA WASTAAFU NA MIFUKO YA AKIBA zinakendesha Semina na Mafunzo kwa Jamii ya Tanzania kujiamini kimaisha na kuzingatia kuwa Maisha bila Ajira ktk Siasa inawezekana PIA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...