Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani akifungua mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Mkutano huo wa siku mbili unaowashirikisha wajumbe kutoka nchi za Ethiopia,Sudan ,Djibouti, Uganda, Afrika Kusini,Kenya, Tanzania na Burundi pamoja na mambo mengine unajadili masuala mbalimbali yatakayoweza kuboresha utendaji kazi wa nchi husika katika kuheshimu utawala bora na kulinda haki za binadamu.
Rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (kulia) akizungumza na washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kanda ya Afrika Mashariki leo jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora wakipitia nyaraka mbalimbali wakati wa mkutano huo leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kutoka nchi 9 za kanda ya Afrika Mashariki wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kutoka Tanzania Jaji kiongozi mstaafu Amir Manento (aliyesimama) wakati wa mkutano huo ambaye amewataka washiriki hao kubadilishana uzoefu na kuboresha utendaji kazi wa nchi husika katika kuheshimu utawala bora na kulinda haki za binadamu.
Waziri wa Katiba na sheria Celina Kombani (kushoto) akizungumza jambo na Rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (kulia) mara baada ya kufungua mkutano wa siku mbili unaowashirikisha wajumbe kutoka nchi 9 za Afrika leo jijini Dar es salaam. Katikati ni mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora nchini Tanzania Jaji kiongozi mstaafu Amir Manento.
Washiriki wa mkutano wa umoja wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora kutoka nchi 9 za kanda ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja wakiongozwa na Waziri wa Sheria na Katiba (katikati mstari wa mbele), rais wa taasisi za Afrika zinazoshughulikia utawala bora (AOMA) Dkt. Paulo Tjipilica (wa pili kutoka kulia) na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania Jaji Ramadhani Manento (wa pili kutoka kushoto).Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...