Hellow Ankal,
Habari za kazi! Naomba msaada in ze tutaz mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 40 nimeoa na nina watoto watatu. Tatizo nililonalo ni kwamba kwa sasa mke wangu hawezi tena kufanya tendo la ndoa kutokana na matatizo yaliyompata ambayo si vyema kuyaongelea hapa kwani si mada yake. 

Msaada ninaoomba ni kupata mwanamke ili awe mpenzi wangu lakini awe na heshima kwani sitaki kabisa mke wangu afahamu jambo hilo kwani linaweza kumsababishia matatizo makubwa. Napenda awe na umri wa kuanzia miaka 30 hadi 40.

Email: jabbilay@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 47 mpaka sasa

  1. Hiyo itakuwa ni ZINA!!

    ReplyDelete
  2. Pole Sana. Ukipata shida kama hii ni vyema kuvunja desturi na Kumuomba mkeo kama anaweza kukusikia na Kukuelewa. Ama sivyo weka msichana wa kusaidia kazi za ndani, Kisha unakuwa unajiliwaza taratibu. Haya ndio Maisha

    ReplyDelete
  3. Kwa hiyo unataka kum-cheat mke wako sio?? Na wakati huo huo uwe unamuheshimia mke wako sio? eti awe mpenzi wako? Yaani uwe unazini:-? Wee hujui kuwa ndoa ni kwa raha na taabu ikiwemo uzima na ugonjwa?

    ReplyDelete
  4. Upuuzi gani huu?

    ReplyDelete
  5. nilifikiri mkeo ndo kakutuma,una shilingi ngapi short time?

    ReplyDelete
  6. oa mke mwingine acha uzinzi...halafu mr michuzi hii sio sehemu ya kutoa matangazo ambayo hayana maadili jamani. hivi kweli mtu anatafuta mtu wa kuzini nae hazarani tena kupitia blog ambayo inaaminika na kutumiwa na watu wengi kwa heshima na adabu zote leo mtu anatamka hazarani humu anatafuta mpenzi na hataki mkewe ajue...sikubaliani naye.ingekuwa hajaoa ningeweza kumsapoti lakini kwa hili la kumsaliti mke wake kupitia humu ashindwe kabisa.

    ReplyDelete
  7. Nenda kwenye danguro utawapata wengi tu wa kumwaga

    ReplyDelete
  8. duh Michuzi blog yako imegeuzwa kuwa mahali pa kutafuta mahawara?

    Ok tuje kwa aloleta hii topic umesema kuwa hutaki mkeo aje kufahamu kama una mpenzi, sasa suali langu unadhani vipi kama huyo mkeo hasomi blog ya michuzi? kama anasoma si ndio tayari keshajua siri yako? Tena haitamchukua hata dakika mbili, anajua ana watoto watatu na hawezi tena kufanya ile ishu, basi ni moja kwa moja ni mumewe tu aloleta hii post hapa.

    Ushauri wangu kaa mkao wa kula, mkeo akiiona hii ujue vya kujitetea uzuri.

    ReplyDelete
  9. Ungepata matatizo wewe ungekubali tukusaidie Mke wako????? na ungejisikiaje?????

    ReplyDelete
  10. Unaishi wapi?
    If in Dar, just drop by q-bar, maisha etc and you can get what you are looking for very very easily.

    ReplyDelete
  11. hii habari haina kichwa wala kidole....michuzi hizi hadithi za kitoto usituwekee hapa hii sio blog ya kutongozana au tueleweshe na sisi kama hapa watu wanaweza kutongozana

    ReplyDelete
  12. Hivi jamani "Katika shida na raha" maana yake nini? Yani huna hata aibu kupost hicho ulichopost?

    ReplyDelete
  13. shetwani mkubwa wewe yani mijianaume mingine hovyoooo huna hata haya na nakuapia hutopata kbsaaaaaaaaaa labda km hakuna Mungu.

    ReplyDelete
  14. Hii misaada mingine Michuzi uwe unaielekeza chooni ikasaidiwe vizuri, Mtu kama huyu utamsaidia vipi.

    ReplyDelete
  15. Habari kaka Michuzi.

    Napenda kumpa ushauri huyu ndugu yetu kuwa wazo analofikiria la kutafuta mwanamke mwingine sio zuri.Jaribu kufikiria kuwa ungekuwa ndio wewe huwezi kufanya ngono tena na mke wako ndiye atafute mwanaume mwingine ungejifikiriaje?.Cha muhimu zidi kumtanguliza Mungu katika tatizo la mke wako na atakuonesha miujuzi na njia sahihi ya tatito lenu.

    ReplyDelete
  16. Ww mwanaume hauna akili hata kidogo.Kama mkeo ana matatizo Basi hayo matatizo ulimpa wewe.umempa matatizo eti natafuta mpnz huna hata haya babu mzima ovyoooo.

    ReplyDelete
  17. This is called Cheating, I don`t condone it at all, mtunze mkeo, kwenye taabu na raha, kama wataka cheza nje cup basi tafuta nyumba ndogo mwenyewe.

    ReplyDelete
  18. Pole sana ndg yng, kwani mficha uchi hazai, lakini leo nimefarijika sana na hii hoja yako humu ndani na kujiona kuwa kumbe tupo wengi wenye tatizo moja, hivyo basi wadau na mimi ndugu yenu, natafuta mpenzi kwa tatizo kama la ndugu yngu aliyeni tangulia, isipokuwa mimi nipo hapa London, maeneo ya Southeast na haya ndiyo mawasiliano yangu +44 746 669 53 plz!

    ReplyDelete
  19. YOUR NOT SERIOUS.

    ReplyDelete
  20. kubaliana kwanza na mkeo ili baadaye isije ndoa ikaisha na kuwapa taabu watoto.Anza kidogo kidogo kuongelea hilo jambo.Mimi naamini moyo ukikutuma hakuna mtu yeyote atakaye kukataza hata kama akijua.

    ReplyDelete
  21. ulipokuwa unaapa kwenye shida na raha ulidhani shida ni kukosa hela tu? je kama ni wewe ndio ungekuwa na matatizo ungejisikiaje kama angetafuta naye mtu pembeni na kurudi kwako kajikausha kama unavyotaka kufanya?

    ReplyDelete
  22. Wewe kaka sasa unageuza globu ya jamii kuwa mahala pa kufanyiwa ukuwadi, kwani mwenyewe hujui kutongoza, mkeo ulimpataje?, usipotezee watu muda, ingia mtaani utafute, lakini angalia usije ukavamia popobawa.

    ReplyDelete
  23. kwenda zako usipotezee watu muda. We hujui kama ndoa ni kuvumiliana?We bana kama ukizidiwa kina dada pouwa wapo kibao nenda wakusaidie kwa muda huo then endelea na taratibu zako za maisha kama kawaida. Unapoomba msaada kwenye jambo la kipuuzi kama hilo unategemea watu watakusapoti!?LIMBUKENI MKUBWA WE.

    ReplyDelete
  24. Ankal Michuzi sasa mbona una promote wizi?

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  25. wewe ni mpuuzi wa hali ya juu na huna maana kabisa, sijui wewe ni dini gani hasa ,anyway huna budi kusaidiwa hata kama wewe ni chizi wa aina yake, kwanza unatakiwa umwache huyo mke wako ili ukubalike kuoa mwingine-la kama tu unataka kutembeza jando kila unapojisikia wahaya wapo na ni halali kabisa -ila kumbuka kutumia kondom-lakini unaposema upate mwingine wa pembeni lakini mkeo asijue,tena awe na heshima,hii ni dharau kwa dada zetu.Labda awe kafungua mwenyewe duka anajiuza ,hiyo ni hiali yake ,hata huko Ulaya sex trade ipo. bahia Sengule

    ReplyDelete
  26. kaka pole sana,ila nadhani ungelezea story yote pengine ungepata ushauri kutoka kwa wadau iliuweze kumsaidia mkeo aweze kupona,hayo mambo ya kutafuta ngono nje ya ndoa achana nayo.Mdau london.

    ReplyDelete
  27. TAFADHALI KAMA WEWE NI MUISLAMU BORA UOE ZINAA MBAYA

    ReplyDelete
  28. Nitakubali vipi bila kujua matatizo ya mkeo?

    ReplyDelete
  29. kwa hiyo unataka kuoa au kufanya uzinzi?

    ReplyDelete
  30. BEING AN IDIOT YOU DON'T NEED TO HAVE A LABEL ON YOUR FACE. SHAME ON YOU

    ReplyDelete
  31. Unatoka michuzi awe sehemu ya Ufuska wako?

    ReplyDelete
  32. Kaka nenda Muhimbili national Hospital(NMH) kaonane na Gyenacologist watakusaidia kumtibu mkeo kama bado hajatibiwa. Hayo unayo yataka mmmhhh... mwanaume hatafutiwi.

    ReplyDelete
  33. Mdau Jabbilay:

    Unakuwa husomeki kwa kuwa umekuja Jamvini kututaka Ushauri na Kusakasaka Mke mpya huku ukiwa unabana undani wa tatizo lenyewe,

    Sasa wewe unafikiri huyo Mwanamke mpya unaemtaka huku undani wa yaliyojiri na Mkeo wa kwanza unayabana unafikiri utampata nani?

    Kwa taarifa yako kwa dalili za suala lako unavyoliweka itawafanya Wanawake waone inawezekana huyo Mkeo wa kwanza ameshaathirika hivyo na wewe pana wasiwasi ukawa hauko salama!.

    Kama ni matatizo ya kimaumbile ya Mwanamke kama masuala ya uzazi, ya nini iwe ni siri si useme tu?

    JARIBU KUJIWEKA USOMEKE !!!

    ReplyDelete
  34. Kapime kwanza ndio uje tafuta mwingine!

    Acha zako wewe, inaonyesha Mkeo amepima na ameukwaa,,,na wewe unapiga chenga Kipimo unakurupuka kuja humu kwa siri kutafuta Mwanamke mwingine!

    Watu kama ninyi ndio mnaokataa Kupima mnataka wenzenu tu wapime.

    Si ndio ninyi mnaokwenda kupima halafu majibu hamchukui ?

    ReplyDelete
  35. Acha unafiki !!!

    Kwa nini uwe na Mwanamke mwingine kwa siri?

    Huo si ndio usaliti wenyewe ?

    ReplyDelete
  36. Kwa umri huo, watoto wa 3 umeshapata mwanamke mwingine wa nini? imebaki uendeleze Sala tu !

    ReplyDelete
  37. Sasa Mdau wewe Mkeo hastahili kupata tendo la ndoa, hivi utakuwa unamtendea haki mwenzio Mke wa Kwanza kama utataka uwe unapata tendo la ndoa na Mwanamke mwingine tena kwa siri?

    ReplyDelete
  38. kwa umri wako huo,sikutegemea kama ungekuja kuweka shida zako humu,huoni aibu?jee wewe ungekuwa unaumwa na yeye angetaka kufanya kama unayotaka kufanya wewe,jee ungekubali?unless muwe mmekubaliana.shame on you mr.

    ReplyDelete
  39. MPUUZI KWELI WEWE SASA UNATAKA TUKUTONGOZEE HUYO MWANAMKE AU?
    MBONA WAMEJAA KIBAO MITAANI HATA WAZURI WA SURA KULIKO HUYO MKEO,NYAMBAFU TUPE MATATIZO YA MKEO TUKUPE USHAURI SIYO UNATELEZA UTOTO WAKO HAPA.

    ReplyDelete
  40. Ankal, inakuwaje unakubali kuwa mjumbe wa Ibilisi?

    ReplyDelete
  41. We kaka muombe Mungu, akufungulie tatizo la mkeo apone, hakuna kwa Mungu kisichowezekana. Kupata mwanamke mwingine siyo solution bali ni kujitafutia matatizo makubwa. Kumbuka kiapo cha ndoa mtapendana kwa shida na raha.
    Jabilal, Sex is not everything, kuna mambo mengi anaweza kukutendea mwenzako na akakufikisha na ukaridhika, i beleave so.

    ReplyDelete
  42. Wewe kula kitu roho inapenda. Majanamke yenyewe ya siku hizi ni masaliti ya kutupwa. Likipatwa na matatizo kama hayo ni nafuu kwako maana utakuwa umepunguza presha. Twanga maisha kwakwenda mbele achana na huruma.

    ReplyDelete
  43. Matatizo ya akili huanza taratibu, na baadaye.........................
    Wewe watoto 3 tayari, maisha yenyewe haya, dunia yenyewe hii, maradhi mpaka kwenye hewa. unataka kumwachia nani hao watoto? Tumia akiloi, kilichobaki ni ibada kwa sana ndugu, acha tamaa.

    ReplyDelete
  44. umejitakia mwenyewe baba. Kama muislamu hata mkeo anatakiwa akushauri uoe. Mimi Mume wangu hawezi kunitosheleza kwa muda mrefu kama miaka 10 hivi. Watu hata hawajui maisha yanaenda namhurumia lakini dawa za kienyeji wala hataki kuzisikia, hivyo tuko kama mtu na dada yake na maisha yanakwenda vizuri tu. kwani ni lazima kama mungu kafunga riziki, yeye peke yake ndie anaeweza kuifungua. Urohomwa ngono ndio inayowaaibisha watu.

    ReplyDelete
  45. wewe uliyesema mumeo hakutoshelezi kwa miaka kumi sasa!! du nadhani utakuwa unae wa pembeni tena si mmoja kwa sababu mambo haya huwezi kumvumilia mumeo kipindi chote hicho! huku raha ukizikosa!!!! sema kweli dada!!

    ReplyDelete
  46. Kama upo Arusha kaka mimi naptikana Mrina bar na Sheevers bei maalewano ni kuanzia buku tatu na kuendelea. Karibu kaka!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...