Habari zenu wana jamii?Mimi ni kijana mtanzania mzalendo-nina kazi ambayo namshukuru Mungu inanifaa. Ninataraji kufunga ndoa mwakani. Nampenda mchumba wangu, ila tatizo nililonalo ni hili : mwaka jana january nilikuwa namuona msichana fulani kila siku asubuhi wakati naenda kazini. yeye pia anakuwa anaenda kazini, kwa hiyo tunaongozana hadi kituoni tunapanda gari moja-tunaachana njiani. Huyu mshichana ni mzuri sana kwa kumuangalia na ana adabu ambayo nimeiona kwa watu wachache sana. Hana makuu na humsalimu mtu vizuri kama inavyohitajika. Nikaona si mbaya tukawa friends. Basi toka february mwaka jana tukawa friends. Tukaanza mawasiliano madogomadogo, mara simu kwa sana, mara lunch dinner,movies kutembebeana home. Nikamtambulisha kwa mchumba wangu(Ila my fiancee hampendi kabisa!).
Tatizo linaanza: kwa hiki kipindi tulichohang out together tumejikuta ni marafiki close sana(mimi niko very timid na huwa siko comfortable arround girls hata mchumba wangu, lakini ajabu huyu rafiki yangu ndo msichana wa kwanza in my life kuwa that karibu na simuonei aibu na we discuss ideas deeply).
Kumuelezea tu ni mzuri sanaa, ana tabia nzuri sana yani perfect wife material, ni msomi na ameniambia wazi ananipenda.
Kiukweli nampenda sana kuliko mchumba wangu, ila sasa natakiwa kumtambulisa mchumba wangu kwetu wiki ijayo na home wanajua ntamleta siku iyo.
GUYS I HAVE MET THE LOVE OF MY LIFE AND UNFORTUNATELY I AM ALREADY COMMITED, sijamsaliti mchumba wangu ila nahitaji ushauri ili ni make this big decision of my life...


MDAU KD

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 107 mpaka sasa

  1. nikushauri kidogo mdau, fuata moyo wako kile kinachopenda. usifanye kitu kwa kumfurahisha mtu yeyote including wazazi kwasababu haitakuwa na maana kuwapelekea mtu ambaye moyo wako haujazama sawasawa wakati yupo aliyeuteka moyo wako. hayo masuala ya utambulisho unaweza kusogeza mbele, jipange ufanye maamuzi ya dhati, mwambie mtarajuwa mchumba kuwa umesitisha zoezi ingawa ni ngumu, waambie wazazi umebadili maamuzi. hii itasaidia kujenga maisha yako ya ndoa yawe yafuraha badala ya kumuoa usiyempenda na kuisaliti ndoa yako katika maisha yote kwavile atakuwepo unayempenda na umekiri kuwa unampenda sana na haumuonei aibu. kumbuka ndoa hainaga marudio, usije ukajuta baadae.

    ReplyDelete
  2. That now you are in reall Love...
    Piga chini huyo wa zamani.. chukua mpya ambaye mnaelewana..
    mweleze wa zamani ukweli..manake ndoa sio kubahatisha it is a reality...

    ReplyDelete
  3. Mr. KD, Katika kufanya maamuzi ya kuoa kunahitaji utulivu, busara na hekima ya hali ya juu ili kumpata mwenza anayekufaa katika maisha yako. Maana yake ni kwamba unaweza kuacha wachumba hata kumi lakini ukishafanya maamuzi ya kuingia kwenye ndoa huyo ni wako kwa shida na raha! jambo la msingi katika kuchagua mwenza ni kuangalia tabia zenu kama zinawiana na kubwa zaidi ni kuvumiliana manake kila binadamu ana mapungufu yake. Hivyo, pamoja na ushauri utakaopewa na wachangiaji bado uamuzi wa mwisho wa nani wa kumuoa unao wewe.

    ReplyDelete
  4. listen to your heart! but make sure your mind is awake!

    ReplyDelete
  5. mtose tu mchumba wako usije ukaregret for the rest of your life.

    ReplyDelete
  6. hujatulia.

    ReplyDelete
  7. Follow your heart! Usingalie watu watasema nini but angalia uko comfortable wapi. Pia zoezi la kutambulisha next week nakushauri uahirishe kabisa till further notice, ili ukae utathmini kwa makini who is who. otherwise waweza fanya Intro next week ukajikuta umemtambulisha asiefaa hata kama ni huyo fiancee wa mwanzo au unayempenda kwa sasa. Zaidi ya yote maswala ya uchumba unapaswa umshirikishe Mungu zaidi kuliko kufuata hisia au ushauri tu. Umefanya maombi kikamilifu?

    ReplyDelete
  8. Mdau KD, Situation uliyonayo ni Ngumu kweli ila haswaaaaaa.... kuwa makini na huyo dada, unamfahamu vizuri? Kakukuta ukoje kiuchumi? Je mapenzi yako kwakwe ni halisia au yanatokana na muonekano wake?

    Ukimkosea atakuwa na uwezo wa kukusamehe? au unaona upande mmoja? then ukipata majibu ya haya yote, fuata moyo wako.

    ReplyDelete
  9. Ushauri wangu kwako kwa vile umeshasema unampenda uyu binti ambae umekuwa na mazoea nae zaidi nakusihi kama una ummwona anafaa kuwa mkeo na unampenda zaidi ya mchumba ambae unataka kwenda kumtambulisha kwenu, mchumbie na ndio awe mkeo mwombe samahani huyo mchumbako mwambie ukweli. Hakuna kitu kibaya kujiingiza kwenye ndoa na mtu usiyempenda au huna uhakika nae kuliko ukamtesa kwa kutoka nje ya ndoa ukishamwoa bora usimwoe kabisa. bll

    ReplyDelete
  10. Mdau nimekuelewa:

    zingatia usemi ''TAFRIJA MBILI ZILIMPONZA FISI''

    Ni kitu kibaya sana ukawa ni nyoka wa vichwa Viwili yaani haijulikani mkiani ni wapi na kichwani ni wapi.

    Katika masuala nyeti kama hili la kwako ulitakiwa uwe na Msimamo kamili na kuwa muwazi kabla ni nani kati ya MCHUMBA HALISI na RAFIKI WA KARIBU !

    UNAKUWA NA UAMUZI MMOJA NA USIO WA KUMRUDISHA MTU NYUMA.

    ZAIDI YA HAPO UTAZUA KIZAA ZAA CHA WATU KUKOSA MAELEWANO PANDE ZENU (TATU) SASA SIO (MBILI), WATU KUZIMIA KWA KUKATA PUMZI KUTOKANA NA MAAMUZI YAKO YA MABADILIKO YA GHAFLA NA KUSHITUKIZA, UTAJAZA VICHWA VYA HABARI KWA WAHARIRI KUANDIKA MAKALA KTK MAGAZETI YA UDAKU, AU WATU KUANDIKA TAMTHILIA ZA VITABU AU MCHEZO WA RUNINGA KWA KISA HIKI!

    ReplyDelete
  11. Mdau,

    Naomba Nikuulize swali. Je mbona hujaeleza process uliyompatia huyo unayemtuia Mchumba? Ukiingia kwenye ndoa bila mapenzi uta-suffer sana. Na ikiwa ni mkristo, huruhusiwi kuvunja na kuoa mwingine au kutembea nje ya ndoa.

    Huyo mchumba ulipewa na Wazazi? unaweza kunipata kwa ushauri zaidi kwenye masterceh2009@gmail.com

    ReplyDelete
  12. Mdau Kijana,

    Kwa Mtindo wa jinsi ulivyolipeleka Suala lako Muhimu kama hili, ni mara nyingi watu kama wewe (Wasio kuwa wawazi, vigeugeu na wasio na msimamo) hujutia hapo baadae kwa maamuzi ya ghafla waliyo yafanya kabla !

    Hili suala lingekuwa rahisi sana kama ingelipeleka kwa busara na kuwa na mwelekeo mmoja na kwa uwazi kabla, badala ya kungojea muda umefikia dakika za majeruhi kipenga kupulizwa.

    ReplyDelete
  13. OK,USHAURI WANGU NI:(KWANZA)HUYU MCHUMBA WAKO NATUMAI MMEKWISHA IVUNJA AMRI YA 6 MARA NYINGI,HOW IS SHE??NA MLIPOKUTANA MARA YA KWANZA ULIMKUTA AKIWA VARGIN AU ULIKUTA TAYARI MLANGO UPO WAZI SO UKAANZA KUJILIA MAKOMBO??(PILI)NAKUSHAURI JARIBU KUMUONJA NA HUYU WA PILI ILI UJUE UTOFAUTI WA MAJAMBOZI CZ KUONJA KUNA FAIDA KUBWA SANA.(TATU)KWA KUWA UNATARAJIA KUOA MWAKANI(INGAWA HUJATAJA MWEZI CZ YAWEZA KUWA JANUARY,JUNI AU DECEMBER MWAKANI) NA LEO NDO KWANZA MACHI,MIMI NADHANI HAIRISHA KWENDA KUMTAMBULISHA HUYO MCHUMBA KWANZA CZ U STILL HV TIME.HIYO ITAKUPA NAFASI YA KUMSOMA ZAIDI HUYU MPYA IKIWA NI PAMOJA NA KUMUONJA CZ ASIJE AKAWA ANA-PRETEND.NATUMAI UMENIELEWA.NI VEMA UTUPE FEEDBACK YA UAMUZI UTAKAOUFANYA HUMUHUMU JAMVINI.NI HAYO TU

    ReplyDelete
  14. mdau KD, mke bora uchaguliwa na Mungu! Hivyo muombe mungu akuonyshe ni yupi atakayekufaa maishani.maisha ni safari ndefu na watu ubadilika.

    ReplyDelete
  15. Kijana ktk Masuala nyeti kama haya ya mahusiano unatakiwa uwe na mwekeo na kuwa muwazi zaidi.

    Kwa jinsi ulivyolipeleka suala lako, unaonyesha dalili za unafiki ktk mahusiano yako na watu!

    ReplyDelete
  16. haaaa....unachekesha eti love of your life,there are so many of such type sasa wewe utakua na love of yor life wangapi? walio committed hata hatuombi ushauri ww kichechee tu!

    ReplyDelete
  17. ndugu yangu ndoa ni safari ndefu na yenye misukosuko sana hivyo unapaswa kuwa na mtu unayempenda kwa dhati. katika maelezo yako inaonesha wazi kuwa huyo demu wa pili unampenda zaidi ya huyo mchumba wako. na inaonesha wazi kuwa hata kama utaproceed na huyo mchumba wako hutokuwa na mapenzi ya kweli kwa kuwa tayari moyo wako uko kwa mwengine.

    kwa haraka ningekushauri kuwa mchukuwe huyo wa pili na achana na huyo wa mwanzo ila nasita kusema hayo kwa sababu mwaka mmoja mliokutana na huyo wa pili ni kipindi kifupi sana. na kwakuwa mnakutana njiani tu unaweza usijue kwa undani tabia ya mtu.

    hivyo nakushauri pata muda wa kutosha na huyo wa pili kabla ya kuamua kumchukua maana usijejuta baadae. kupima tabia ya mtu kunahitaji angalau miaka 2 na sio muda mfupi kiivyo.

    asante.

    ReplyDelete
  18. pole sana kaka kwa mtihani ulionao, haya mambo yanatokea sana katika maisha na wengi wetu tumekua tukiingia katika commitment na hatimaye ndoa bila kuwa na uhakika na umpendaye au tu kwa sababu mlikua na historia flani nyuma au kwa sababu ya shinikizo la kuona kwamba jamii itakuelewaje matokeo yake tunaingia ktk ndoa za mateso au za kichina kama vijana wa mjini wanavyosema miezi miwili mitatu mmeachana.
    USHAURI wangu kaka, kama kweli unampenda huyo binti wa pili na una uhakika na mapenzi yake kwako ni ya kweli si ya kisanii coz anaweza akawa anajidai anakupenda kwa anajua upo kwenye mahusiano mengine ilimradi akuvurugie uvutiwe naye, basi kama una uhakika na huyo its better ukamwambia mchumba wako ukweli mapema, ni ngumu na inaumiza lakini u have to do that ili usimpotezee binti wa watu muda (huyo mchumba wako) coz unakiri kuwa unampenda huyo dada zaidi yake, usije ukaingia kwenye ndoa then huna furaha au una cheat siyo nzuri kwakweli, mwambie ukweli then fuata furaha ya moyo wako.
    GOOD LUCK
    Mdau, ms

    ReplyDelete
  19. Pole sana mdogo wangu,binadamu anahatua nyingi za kupitia na siku zote binadamu huwa na malengo,kwa ufupi msichana anapokuwa amesoma,amepata kazi anahitaji kuwa na mwenza...hivyo nahisi anahitaji mwenza na anajua unahitaji kuoa,angalia mapenzi siku zote mwanzoni ni matamu.Nakushauri stick kwa mchumba
    Lufingo

    ReplyDelete
  20. Listern to your heart! Mke sio wa siku moja au mbili, ndoa haijaribiwi... it's till death do u apart... Muombe Muumba wako akusaidie na AMUA kwa busara. Ukikosea mke, unaweza hata kukosea maisha!

    KWA USHAURI WANGU HUYO MPYA NDIO CHAGUO LAKO! ILA TAFUTA DATA NA ONJA TUNDA... NDIO UFANYE MAAMUZI!

    ReplyDelete
  21. lwinga josephMarch 23, 2012

    Kwa nza nikupe hongera kwa kutoweza kumsaliti mchumba wako na mke wako mtarajiwa kwa kipindi chote hicho ambacho umekuwa na mahusiano ya urafiki mwema na huyo msichana.
    La msingi kumbuka tu kuwa maisha yanataka uvumilivu na msimamo,leo unajisikia kumpenda huyo msichana na unafikiria kumuacha kwa kuwa tu hisia zako zinakupeleka huko na kumuona yule ambaye umekuwa naye muda mrefu hana maana tena,jiulize,je ukimuoa huyo msichana unayejisikia kumpenda sasa na kumuacha uliyenaye na ikatokea mbeleni ukajikuta unampenda mwanamke mwingine,utakuwa tayari kumuacha mke wako?
    Mshukuru Mungu kwa kukupa huyo uliyenanye maana bila huyo wala usingepata nafasi ya kumuona mwingine na kuwa na msimamo thabiti katika maisha maana hata ndugu zako hawatakuelewa,itapendeza zaidi mkabaki kuwa marafiki wa kawaida tu bila kuingiza mambo ya mapenzi.

    ReplyDelete
  22. hayo ni maisha yako kaka fanya maamuzi ambayo wew unaona utakuwa na amani nayo, pia washirikishe na wazazi wako kabla hujafanya decision yoyote, kila la kheri

    ReplyDelete
  23. Kwanza kabisa nakupa pongezi kwa kuwa na wachumba wawili, mmoja akionekana ndio love of your life. pili naomba nikupe ponngezi kwa kuwa 'open' about your feeling.
    mimi ushauri wangu ni kuwa mchukuwe yule ambaye unaona kwa sasa hivi chemistry zenu zinakubali. ao mtu unayempenda kwani hata mbele ya safari mambo yakiwa magumu kitakacho wapa nguvu ya kuendelea mbele ni hiyo feeling unayoipata sasa hivi. sasa hivi sio late kumuarifu huyo wa kwanza. actually itamuumiza sasa lakini ni better kwani later utakuwa na huyo wa pili na atakapojua ataumia zaidi na siajabu ndoa ikaharibika na huyu wa pili ukakuta kashapata mwingine. wasichana kama hawa hawakai muda mrefu katitka soko.. nakutakia mema.

    ReplyDelete
  24. Wewe kuwa mwenye hekima,ikiwa una mpenda mwengine na kuoa uso mpenda na kumuamini kiasi kikubwa ni balaa kwako,heri lawama kuliko fedheha,acha kuoa ili umuoe yule unayeridhishwa na nafsi yako!utalaumiwa lkn upate mke ambae utaridhishwa nae

    ReplyDelete
  25. Muombe mungu akusaidie kukuonyesha yupi anafaa kuwa mke kwa maana usifanye haraka ukaja ukajuta maishani mwako.Ushauri wangu kama bado ujafanya maamuzi ya kina kaa chini fikiri mara mbili kabla ya kuamua.Mtu achaguliwi mke anachagua mwenyewe.

    ReplyDelete
  26. pole sana chief wangu kwa hali unayokutana nayo,maana najua huwezi kuwa na wote kwa wakati 1,ila omba mungu akuonyeshe ni yupi kati ya hao 2.si unafahamu ndoa inatoka kwa mungu na siyo kwa sisi tutakavyo,pili angalia yupi moyo wako unamuhitaji nikimanisha kuwa na mtu ambae ukizeka unafurahi kuongea nae na bado utakuwa una mapenzi nae.thirdly kumbuka uzuri sio tija anaweza akawa mzuri lakini tabia haifai,fourthly don't rush chukua mda kumfahamu like 2yrs namanisha your new friend.then hakikisha kwao wanakujua ili ufahamu kama watakupenda ili usiji commit mapema kwanza.

    Regards SOKA

    ReplyDelete
  27. wewe mdau acha tamaa huyo uliyenae kwani hana adabu au ni mbaya sasa kwa nini ulimpotezea muda wake? huo ni uhuni wako na uamuzi unao wewe mwenyewe acha kutuyeyusha , tamaa mbaya na ukapime miwaya hujatulia kabisa umeniudhi sana

    ReplyDelete
  28. pole sana kaka kwa hayo yaliyokupata tunajua ni hisisa zinakuwepo ila kwa ushauri wangu ni bora ukaoa mtu unayependa ili baadae usije kujilaumu bure maana kama utamuoa usiyempenda kwa vyovyote vile lazima utakuja kumsaliti kwa huyo uliyempenda.ndo mawazo yangu hayo ila cha msingi ni kumtanguliza mungu muombe mungu akutangulie katika uhamuzi wako.

    ReplyDelete
  29. Mdau KD,
    Kinachojidhihirisha hapa ni wazi kwamba huyu binti wa pili ndio chaguo halisi la moyo wako. Naweza kusema uliharakisha kufanya maamuzi ya kuanzinsha uchumba na mtu ambaye alikuwa bado hajaushibisha moyo wako.Na kwakuwa tayari umeshaliona hilo mapema kabla hamjafika mbali na mchumba wako huyo, ni vema ukakaa naye chini na kumueleza ukweli wako bila kumficha. Kwamba, hutaendelea na uchumba kutokana na sababu ulizozieleza. Naamini atakuelewa. Kikubwa ni kuwa na muwazi kwake na kutumia hekima ikibidi kumuomba radhi. Nasema hivyo, kwa sababu haitakuwa na maana yoyote kuendelela kumpotezea muda huyo mchumba wako ili hali tayari umempata unayempenda kwa dhati.Na kwa upande wa wazazi, huko ni rahisi tu. Unachotakiwa ni kuwafahamisha kwamba zoezi la kumtambulisha mchumba wako limesitishwa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wako. Najua watakusiliza kwani wewe ni mtu mzima mwenye kuamua mambo yako mwenyewe.Nao pia unapaswa kuwaomba radhi. Ni hatari sana kwenda kuingia kwenye maisha ya ndoa na mtu ambaye huna mapenzi naye ya dhati. Lakini angalizo ni kwamba,kama haya unayotaka kuyafanya yanatokana na msukumo wa tamaa za kupenda warembo,utakuwa na wakati mgumu sana wa kufikia maamuzi ya kupata mwenza.Vinginevyo,Goodluck!!

    ReplyDelete
  30. FROM DOCTOR PHIL.....!
    KD KATIKA WAPUMBAVU SAMAHANI MICHUZI KWA LUGHA KALI KIDOGO YAANI WEWE KD KWA KIFUPI NI PUNGUWANI, SASA USHAURI GANI UNAUWEKA HADHARANI CHOONI KILA MTU ANAUSOMA HUYO MWANAMKE WA MTAANI NA MCHUMBA WAKO HATA WAKWE WOTE WANAKUSOMA WANAJUA UNAENDA NEXT WEEK WAKATI TAYARI UMEANIKA UCHAFU WOTE KWENYE BLOG YA JAMII? KWELI WAJINGA NDIYO WALIWAO, LET ME TELL YOU HUYO MWANAMKE ATAKAYE KUPENDA UTAFAIDI NA MTAA MZIMA THAT IS WHATS UP BROTHER, KAA NA HUYO HUYO WA MWANZO TAMAA ITAKUUA. MICHUZI NIFIKISHIE UJUMBE KWA HUYU KD. HII TABIA MBAYA UNAMCHUMBA LAKINI BADO UNAKODOLEA MACHO TOTOZ ZINGINE TENA KWENYE VIYUO VYA BASI?
    DOCTOR PHIL

    ReplyDelete
  31. je una hakika unampenda huyo mpya au ni upya ndio unakuzuzua? na je hutampata mpya mwingine ukaona anafaa zaidi ya huyu wa pili? kaka mi naona hujatulia.

    ReplyDelete
  32. Lazima utakuwa na pepo wa ngono. Kuna hatari ukakutana na mwngine mwenye adabu mbele ya safari naye ukamfikiria ku-hang out naye. ushindwe

    ReplyDelete
  33. Hukutueleza huyo wa kwanza ulichaguliwa na wazazi? au ulimpenda mwenyewe.Na kama ulimpenda wewe mwenyewe na mpaka ukamchumbia,basi huyo unayempenda sasa yawezekana pia akawa si chaguo la maisha yako kwa sababu moyo wako haujatulia

    ReplyDelete
  34. KIJANA ACHA UTAPELI, JE ULIKUWA WAZI KIASI GANI KWA HUYU rafiki yako mpya KUHUSU HATUA ULIYOFIKA NA MCHUMBA WAKO? AU ULIKUA UNAFURAHIA TU UNAVYOMCHANGANYA HATA AMEFIKA MAHALI AKATAMKA ANAKUPENDA SANA (kitu ambacho asingeweza thubutu kufanya kama ulionesha msimamo wa dhati kuwa una Mchumba)

    PILI, KD KAMA WEWE NI MKRISTO, MWANAMKE KUMTAMKIA MWANAUME KWA HABARI HIYO SIO KIBIBLIA, MWANAUME NDIO KICHWA, SASA WEWE UNATONGOZWA VIP BWANA!!!

    TATU, SIKU ZOTE UNAPOKARIBIA KUOA VURUGU HIZO NDIO HUZIDI...INAKUA KAMA MPIRA WA KONA VILE...LAKINI MKE HAPO NI YULE AMBAYE AMETULIA ANAKUWA HANA MAKEKE HATA KIDOGO, SASA UKIKALIA KUTONGOZWA NA WEWE UNACHEKA CHEKA TU NDO UTAELEWA SAA HIYO MAANA YAKE NINI.

    NNE. AMUA MAANA YOTE NI YAKO
    VODACOM: KAZI NI KWAKO

    ReplyDelete
  35. DO WHAT TOU THINK IS RIGHT FOR YOUR LIFE. FOLLOW YOUR HEART

    ReplyDelete
  36. Zamani tulipokuwa JKT kulikuwa na kitu kinaitwa "Ajua", yaani anza tena. Simamisha zoezi la uchumba ,tafakari upya, hujachelewa!

    ReplyDelete
  37. KWANZA KABISA SITISHA HIYO PROCESS YA KWENDA KUTAMBULISHA NA KWA KUUSIKILIZA MOYO WAKO ANZA MAONGEZI NA HAO AKINA DADA NA SALI SANA MAANA HUU NI MTIHANI MKUBWA AMBAO HUJAWAHI KUUPATA MAISHA YAKO YOTE, KWA VYOVYOTE VILE UNAPASWA KUUFAULU, MIMI ILINITOKEA KABLA SIJAOA LAKINI ILIKUWA KITAMBO KIDOGO NA NILISOLVE VIZURI.

    ReplyDelete
  38. Mdogoangu, angalia usije ukamuumiza mchumba wako wa zamani kwa mapenzi mapya, hufanya kuona yale yaliyo mazuri tuuu. Mkishazoeana utamuona kama yule wa zamani. Hivyo ahirisha kwanza utambulisho kwa wazazi na umfahamu vzr huyo mpya ndo uamue uamuzi ulio mzuri wa kuanzisha familia itakayokuwa bora.

    ReplyDelete
  39. Ahirisha kwenda kwa wakwe kwanza, jipe miezi 6 zaidi uangalie upepo, la sivyo ukienda tu kichwa kichwa utaishia kuoa wa zamani, baadaye muachane, au uje kufanya dhambi ya kutoka nje ya ndoa...mbaya sana

    ReplyDelete
  40. Mkataa pema pabaya panamwita!

    Wakati mwingine kutapatapa kwingi kunapelekea 'ndege mjanja kunaswa na tundu bovu' unaweza kumwacha Demu wa kwanza Mchumba ukapapalika na huyo mpya kumbe Galacha ,bonge la Changu na 'mzigo wake mbovu' matokeo yake ukaja kujuta baadae, huku ukiangalia Mchumba wa mwanzo unakuta kesha olewa kitambo!

    ReplyDelete
  41. wakina dada wote wanapokwenda kazini wanakuwa wazuri,kaa tulia na ufikirie upya.kila siku utakutananao.huyo mpya ambaye unaye jaribu sana kumchunguza tabia,background history yake.ila kula TUNDA KWANZA,ila hata ukioa huyu mpya utakutana na mzuri zaidiyake.ILA FANYA KITU ILE ROHO INAPENDA.

    NEEMA,PASCAL,JOYCE

    ReplyDelete
  42. Utakua umefanya dhambi kubwa sana ambayo hautaweza kusamehewa,

    Wtoto wazuri wako weng na wanazaliwa kila siku.

    usije mdhalilisha mwenzako kwa mapenzi ya barabarani utakuja ijutia nafsi yako.
    Take care of your self endelea na mpango wako wa mwanzo kama ulivyopangwa.

    ReplyDelete
  43. Mbona arguement yako ipo biased. ww umemuongelea sana huyo demu unaempenda kuliko mchumba wako. Mchumba wako mmetoka wapi na mmepitia mangapi. usije jutaa.

    ReplyDelete
  44. kaka tatizo lako dogo,huyu wa pili hujaonja ndio maana unahisi umepata love of your life,ukisha onja tu utaona kumbe hakuna tofauti na utamrudia tu yule mchumba wako,kuwa makini

    ReplyDelete
  45. Kd hongera kwa kuopata ujasiri na kushare na sisi.

    na pole kwa kuwa njia panda, ila ki ukweli mwaka mmoja kumjua mtu si mdogo, watu wanajua miezi mitatu wanaoana,

    Ila mi navyoona umepata kitu kinaitwa cold feet, watu wengi sana kabla ya ndoa huwa wanajiuliza km wanafanya maamuzi sahihi, nakuanza kuangalia waliowacha nje na kucompare, uaweza ukadhani unampenda sana huyu dada ila kumbe ni uwoga tu wa kujicommit kwa huyu mwingine, na ukakuta kwasabb mapenzi yenu ni wa wizi basi yanakuwa matamu kwsbb hauna wajibu mkubwa kwake.
    tulia ujiulize alichomzidi huyu mwingine ni nn? na je huyu mchumba wako utaweza kumsahau kabisa.
    pili usichukulie ndoa km kitanzi, ni mapenzi tu, na kushare nyumba na majukumu, hakuna kuuwana uko ndani. lol

    ReplyDelete
  46. Mimi nadhani kaka mpaka umeamua kwenda kumtambulisha huyo mchumba wa kwanza tayari ulishaona wengi na ukaona huyo ndie chaguo lako na ukamsoma hadi ukaridhika nae.
    katika maisha msimamo ni kitu muhimu sana kaa chini tafakari je,huyu wa pili wafahamu historia yake?je,umeshafikiria swala la kupima afya?
    ujue kuna KUPENDA na KUTAMANI sasa isijekuwa UMEMTAMANI kutokana na uzuri wake.kumbuka uzuri wa mwanamke sio sura wala umbo bali ni Tabia kaka.
    Kama una imani hebu kubali usumbufu ahirisha zoezi la kwenda kumtambulisha ongea na Mungu wa mbinguni aliyetuumba mwambie akupe ujasiri wa kujua nani ni nani na pia kufanya maamuzi usiyokuja kuyajutia baadae.wanawake ni wajanja sana hasa akijua haujaoa bado atapretend mnoooo ngoja umpe ticket ndo utamjua vizuri.

    ReplyDelete
  47. Usiusemee moyo mdogo wangu, upe moyo ile kitu inapenda ili siku moja usije kujutia kwamba umechukua mke ambaye ulifanya hivyo kuwafurahisha watu, peleka hisia zako pale ambako unaona moyo unapenda. kwa maelezo yako kama hukushurutishwa na mtu kuandika mtose huyo mchumba wako chukua huyo mpya si ajabu hata kidogo hata wao huwa wanatutosa hivyovyo. bunyake

    ReplyDelete
  48. Kama hujaongeza kumpamba tu, basi anaelekea atakufaa. Cha kujiuliza kama alijua una mchumba iweje alijiweka karibu sana nawe, ampokonye na kumharibia wa kwanza?
    Muombe Mungu akuongoze katika hili

    ReplyDelete
  49. MJOMBA HAPO UNA OPTION 3 ( KWA MAWAZO YANGU)

    1. KAMA WEWE NI MUISLAM UNAWEZA CHUKUA NGOMA ZOTE UKAOA ILI KUEPUKA UTATANISHI.

    2. NAONA MOYO WAKO UMEKUFA KWA MTOTO MPYA SASA HAINA HAJA YA KUPOTEZEANA MDA NA FIANCEE WAKO MWAMBIE UKWELI ILI NAE AKATAFTE RIZKI YAKE.

    3.KWENYE MAPENZI HAKUNA USOMI. NI KUPENDANA KWA DHATI, SASA NAONA HATA WEWE UMEKUFA KWA MTOTO MPYA NDOMANA HATA HUTAKI IPITE SIKU 3 HUJAMUONA . HAHAHAHAHAHA

    MWISHO KABISA, KUOA NI MUHIMU, HAYA KAZI KWAKO

    ReplyDelete
  50. Kumbe ndio maana umekuwa unanikimbia sikujua yule ant alikuwa moyoni mwako ...kwa heri!

    ReplyDelete
  51. Umemsifia huyu wapili ila hujasema huyo wakwanza kwa nini haonekani kuwa anaweza kuwa mke wakuwekwa ndani wala hujasema kuwa yeye anatatizo gani mpaka huyu wapili achukuwe nafasi yakuwa mke.Kuowa nijambo moja kuishi nijambo jingine fikiria kuwawa unaitaji kuishi nasi kuzoea.Tulio kwenye ndoa wake zetu tuliwapenda kama wewe unavyopenda huyu ila ukiisha kuishi naye unamwona kama ndugu na yanayofuata pale ni mazoea

    ReplyDelete
  52. Follow Your Heart And It Will Lead To The Right Path / Possibly Give You JOY.

    Tatizo NA UZURI WAKE NI KUWA utakapo chemka maamuzi yako, hutokuwa na wa kulaumu ila nafsi yako.

    Prince Sab

    ReplyDelete
  53. WEWE HUNA LOLOTE NA NHUYO WA MWANZO NAE ILIKUWA HIVYO HIVYO UKAMEGA,SASA TENA UMEPATA MWINGINE NA HUYO NAE UTAMEGA UTAKUTANA NA MWINGINE NAE UTASEMA HADITHI HII HII.PIA INAONEKANA UNA TAMAA OOH HUYU NAPANDA NAE GARI ANAENDA KAZINI SIJUI NINI,UTAPONZEKA HUYO MCHUMBA WAKO WA MWANZO NDO HUYO HUYO KAMTAMBULISHE ACHA UZINZI NYAMBAFU.

    ReplyDelete
  54. Mdau kama bado hujasema I DO mbele za Mungu bado haupo Committed. Wengi watashauri lawama utazipata bali at the end of the day Moyo wako ndo una final say. Kuoa sio u gal friend, ni maisha yako. Muhusishe Mungu then sikiliza Moyo wako husijali watu hata kama wazazi wako kwani hayo i maisha yako. Huyo dada moyo wako uliomkubali ndo Mkeo. Imeandikwa kwenye Bible na vitabu vingine vya Mungu; We humans brainstorming options and plan, but God's purpose prvails Proverbs 19:21. ni kwamba binadamu tuna plan mambo MENGI sana tunasahau Mungu pia ana plan zake kwako. Wewe ulipanga mpaka ukajisikia kutoa mtambulisha binti lakini Mungu ankuonyesha kwamba ana plan kwako na plan yk ni huyo msichana moyo wako uliomchagua. Kubali lawama sasa hv for ur better future.

    ReplyDelete
  55. Follow your heart my dear!!!

    ReplyDelete
  56. oa wote,kwa mida tofauti,baadae maishani utaona mwingine ooooaa tu mpaka wanne,duniani wako wengi mungu anajua ratio ni 6/1 kwa kifupi wanawake hawafanani kila mmoja na uzuri na ubaya wake

    ReplyDelete
  57. Pole sana brother, haipaswi kukulaumu maana ni haki yako ya msingi kulingana na hisia zako. ila inategemeana na muda pamoja na hali uliyoanza nayo ukiwa na mchumba wako, je ulikuwa huna ajira au laaa. kama hukuwa na ajira basi tafakari zaidi. That love of your life mlikutana katika hali ya kikazi zaid, i mean ukiwa na kazi yako na yeye anakazi outing za kumwaga, movies, na raha zote mpaka ukajiona upo huru zaidi na yy, but hajawahi kukuona ukiwa apeche man. hebu mtoe mchumba wako out kama hizo naamin utamuona mpya. achana na kubadili maamuzi ya muhimu kama hayo at that stage. msimamo ni muhimu zaidi na ndoa ni uvumilivu pia usijidanganye kuwa utacheka siku zote na huyo love of your life. ni mapenzi ya wizi tu ndo yanakudanganya lakini akiwa na uhakika kuwa ww ni wake u will c.

    ReplyDelete
  58. Duh.....
    Hongera kwa kutaka kuzitii hisia zako tuu. Leo utamwaacha mchumba kisa katokea dada mzuri zaidi. Kumbuka mchumba alikua mzuri pia ndo sababu ulimpenda mpaka ukafika nae hapa ulipo. Ni sawa unaweza ukamwacha ukamuoa huyu mpya ambaye ni mzuri zaidi. Itakuaje atakapotokea mzuri zaidi ya huyu unayetaka kumuoa? Utamuacha mke wako umuoe huyo mwingine? Kuishi kunahitaji adabu, heshima, upendo, uvumilivu na sheria ya dhahabu. Mfanyie mwenzio kile ambacho unapenda kufanyiwa. Maumivu atakayoyapata mchumba wako yafanye kuwa ya kwako. Umia kama atakavyoumia then mwache uende na huyo wa pili. Unaweza ukafikiri wewe ndo dili kwa mchumba wako lakini ukifanya utafiti utajikuta mchumba wako amevumilia mengu kwako kuliko wewe na amekutana na wanaume wazuri zaidi kuliko wewe lakini akatumia upendo, hekima na akaona mbali akaamua kuwa na wewe tuu. Fikiri hisia na tamaa zinadanganya mara nyingi. All the best my brother,
    Emmanuel

    ReplyDelete
  59. Bwana KD, kutokana na maelezo yako mi naona umevutiwa zaidi na uzuri wake, kuwa na kazi pamoja na usomi wake. Ninahisi huyo mchumba wako wa awali hana hizi sifa, ingawa mthibitishaji wa hili ni wewe. Bado hujawa na uhakika kama utamfurahia kunako sita kwa sita, pia umekaa naye muda mfupi kuweza kujua tabia yake halisi kwa undani. Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu, msichana akishamaliza shule, akapata kazi, basi kifuatacho ni kutafuta mume. So be very careful with her,and please don't rush - she might be very strategic such that you can cannot see all she has in her heart. Utajuta mwanangu! Nina amini yule wa awali unamjua vizuri mno - yaani mazuri yake na mapungufu yake. Kwahiyo usifikiri utapata asiye na mapungufu!

    ReplyDelete
  60. Umeshampotezea muda huyo mchumba wako haitakiwi kumuhacha.halafu punguza umalaya magonjwa ni mengi.

    ReplyDelete
  61. Nina umri wa miaka 61 sasa. Miaka 35 iliyopita nilikuwa katika situation kama yako......
    Uamuzi, japo ulikwa mgumu niliufikia na kuweza kuvunja uchumba.
    Mpenzi wangu wa moyo na rafiki yangu wa kweli ndiye aliekua mke wangu. Tuko kwenye ndoa ya furaha kabisa kwa miaka 34 sasa!!!

    Huu ni mfano hai..... amua mwenyewe sasa.

    ReplyDelete
  62. Hacha tamaa utamaliza mabucha nyama ni ileile

    ReplyDelete
  63. Hi KD

    Niungane na wadau wengine nami kuchangia na ninaomba mawazo yangu yawe bayana kwako na hata kwa wengine kama ifuatavyo:-

    1. Mtangulize Mungu katika maamuzi unayotaka kuyafanya, kwake hakuna kigumu;
    2. Usifuate moyo katika kufanya maamuzi yako kwani sifa ya moyo ni tamaa, fuata akili yako ambayo nadhani ilishakupatia sifa na vigezo za mke mwema utakayependa kuwa naye. fuata vigezo hivyo ulivyojiwekea kisha utapata picha kamili;
    3. Pima mazuri na mapungufu ya wanawake wote hao kisha utapata picha zaidi;
    4. Huyu mwanamke wa pili naye ni wa kumchunguza sana kwani una uhakika na agenda yake, wako wawindaji siku hizi unaweza ukakuta alikuwa amekuwekea mitego nawe ukanasa;
    5. katika maisha wapo watu pia unaowaheshimu na kuwatumia kama washauri wako katika masuala yako muhimu mbalimbali, nahisi ni wakati mwingine tena ukawaone na kuona nao wanashauri lipi;
    6. kwavile mda umekutupa mkono, nashauri uhairishe utambulisho kwa sasa tafuta sababu yoyote na hata kama ndugu hawataelewa kwa sasa kubali tu huo msalaba kwani watakuelewa baadaye kwani unazungumzia maisha yako hapo; na
    7. Mwisho kabisa kumbuka hauko peke yako, wadau tuko nyuma yako na tutaheshimu maamuzi yako.

    ol the best

    ReplyDelete
  64. we wacha uhuni wako, unatafuta sababu za kufanya umalaya wako tu, huna sababu nyingine. Unawezaje kuwa that close na msichana mwingine wakati una mchumba!?

    We mchumba wako angekuwa that close na mwanaume mwingine ungeona sawa!

    Wacha uhuni wewe na usitake kuhalalisha umalaya wako kwa kuonewa huruma huku hewani bhana!

    ReplyDelete
  65. Kwa vile huyu wa pili ni msomi anajua "marketing strategies" and "security strategies". Mwanzo ametumia "marketing strategies" kuweza kukugeuza ukampenda baada ukishakuwa nae tu kwa vile anajua udhaifu wako sasa atatumia "security strategies" kulinda maslahi yake. Kwa vile wewe ni dhaifu na pengine una kijikazi kizuri cha kujipatia vijipesa basi popote utapokutana na mwanamke kama huyu wapili utatekwa tu. Ndoa mdau ni sasa na kuingiza mkono kizani. Unachotakiwa kufanya ukishaingia ndoani ni ustahamilivu na kutimiza majukumu yako.

    ReplyDelete
  66. wewe kaka unaonekana ni mnafki tena player!iweje huyo wa mwanzo ulishamfahamu vizuri just uingiliwe na huyo wa njiani tuuuu?yawezekana huyo kaficha tu makucha yake ila akiyafumua utajuta!na ndoa za hivi mara nyingi huwa ni majutooooo tuuu!ila mwombe mungu akupe maamuzi!
    na je ulijipangaje kufikia wazo la kwenda kutambulisha bila maamuzi yaliyo thabiti?ohooooooo,ndo si lelemama!ndoa ni agano ambalo si la kuchezea.

    ReplyDelete
  67. Kaka mimi na kuombea na pia nashauri usali busara na hekima ziwepo katika uamuzi wako wa mwisho. Sali kuwa inaempenda awemcha Mungu.
    Kisha wahenga husema fuata uamuzi mgumu maana in the long run it is the best.
    Kutokana na maelezo yako ni kama vile umefanya maamuzi ya ku move ila unatafuta maoni ya wengi.
    At the end of the msalaba na uamuzi ni wako tu. Kama hadithi yako ina dosari yeyote basi ushauri wote utakuwa na dosari. Kama wewe ni mkweli than ushauri wa wengi utakufaa.
    Make the tough decision now.

    ReplyDelete
  68. Aggripina AdolphMarch 23, 2012

    Kijana Pole. Upo katika najaribu makubwa. Kutokana na maamuzi utakayofanya, yaweze kukujenga au kukuangamiza kabisa. Ushauri mwingi umepewa hapa, mwingine kwa maoni yangu ni ya kukuangamiza jumla iwapo utaupa umuhimu.

    maoni mengi hapa yaonesha hisia za mwili kuwa kigezo muhimu cha kumchagua Mchumba na hatimayi Mke! Je huyu unaemuona mzuri leo, bado uzuri huo utauona miaka 10 ijayo? Je, Wasichana woooote wazuri umesha waona hata ukafanya uamuzi kwamba huyu wa pili ndiye mzuri kupita wote? Kama uzuri ni kigezo muhimu kwa mke, ilikuwaje ukachagua Mchumba asiyeridhisha hisia na hamasa zako kutokana na uzuri na tabia yake! "beauty is in the eyes of the beholder". Inaelekea huna definition hako binafsi ya "Uzuri". Uzuri wa Mke na Mume ni TABIA hasa ya UPENDO wa dhati. Kwa sababu hiyo utakutana nao wengi wazuri wa sura na umbo katika maisha yako na utakuwa wa kutanga tanga. Omba sana Mungu akuongoze katika mstakabali huu nyeti.

    "Kuonja" ni ubinafsi uliyokidhiri. Mwanamume hasa ni yule anayemridhisha mpenzi wake, anamtosa kileleni daima. Napo ndipo ujisikie raha kwamba uu Mwanaume kweli. La unaonja ni togwa hilo!! Shule in kwenu wawili.

    Ulitegemea Mchumba ampende na kumfurahia huyu msichana uliye mtambulisha kwake kwa lipi? Napenda kukueleza, Huyu mchumba ana karama ya kuwasoma wewe na Miss wako "through your Bodies language" na ametambua huyo ni competitor wake. Nashangaa ulitegemea ampende ili udumishe undumakuwili wako!
    Kijana, sitisha taratibu za kumtambulisha "Mchumba" wako, ili apate fursa ya kukusoma na kukugundua hufai kuwa mume wake. Kwa maoni yangu. HUFAI. Baada ya harusi utakuwa unamletea washikaji wako kama wafanyakazi wenzio! " Na huyo ni Secretary wa Boss wangu, mama naniii! Huyu tunaenda naye Field!" Hujatulia kabisa na hujui unachotaka katika maisha kwa ujumla wake. Kwa hili Tafakari na Omba mwongozo kutoka kwa Mungu mwenye rehema. Siyo sisi wadhambi wenzako.

    ReplyDelete
  69. hayo ni majaribu ya mwenyezi mungu anataka kukuona kama una msimama kaka. wazuri wako wengi na wenye tabia nzuri wako wengi pia utapenda wangapi. siajabu anaficha makucha tu. binadamu atusomeki ndugu yangu. kama huyo wa kwanza ulikuwa unaona hana tabia kama ya wa pili, ungemuacha mapema. umemuona anafaa ndiyo maana unataka kumpeleka kwa wazazi wako. kumbuka wa kwanza ulitoka naye wapi na hajawahi kukukosea. na anakupenda bado.kamtambulishe na songa mbele uzee unaingia baba two years ni mingi sana kuendelea kupima mademu. shauri yako.

    ReplyDelete
  70. My friend wewe ni muhuni tuu hata huyo mpya iko siku utamchoka na kumuona wa 3 anafaa. Nadhani ulivyo anzana na mchumba wako alikuwa kama unavyoelezea sasa iweje leo hafai. Wewe umekwisha na hata kama ni hiyo ndoa ukifunga na wa 2 iko siku atajuta. Kusema kweli hizo ni dalili za umalaya tuu si kingine kama ulikuwa hujijui.

    Mkongwe!

    ReplyDelete
  71. Kaka una mtihani ila Kila kitu unatengeneza mwenyewe...Kwani before Hujamuona huyu binti mpya Mchumba wako ulikuwa wamuonaje? Mpaka ukawa ready Kumtambulisha kwenu and everything?Means ulikuwa umeona anakutosheleza au sio? Sasa umetengeneza huyu mpya kichwani na unaanza muona wazamani hafai...Umeona Jinsi unavyo create vitu,Itatokea siku tena Utamuona mwingine na huyu mpya pia utamuona hakufai. So Please Stick to your Plan A, Plan B is lil' bit complicated mkuu alafu ujue siku huyu mpya akikuzingua utakosa kabisa Support kila mtu atakuwa anasema Umeona umemwacha yule now your facing this na ww pia utakuwa haupo Comfortable kusema lolote kama itatokea kuna shida na huyu mpya coz uta feel guilt na Hapo utakuwa umetengeneza SUMU yako mwenyewe. Huyu Mpya aendelee kuwa Friend a Best friend ww muoe huyu mchumba wako. Ukifanya hivyo pia mchumba/mke wako atakuwa anakuheshimu sana mtakapo kuwa kwenye ndoa atajua kweli una Mapenzi ya Dhati, Ujue hata huyu mpya kwenye mind yake atakuwa sometimes anajiuliza kama uliweza muacha mchumba wako last minutes vp yeye security yake itakuwa aje ktk future yenu? Utakuwa na kazi ngumu sana ya ku prove kwake kuwa yeye ndio choice halisi. Watu wengi hapa kwa Blog watakuambia kuwa follow your heart ila kumbuka your heart was somewhere else before... Na hili swala kama ni la Kweli kaka lipo zaidi kisaikolojia. Maana kama unavyosema huyu mwingine hujawahi hata S..X nae so your mind is playing trick on you, Hayo ni matamanio tu kaka. I wish ningekuona ww mwenyewe pia na huyo Binti pamoja na huyo mchumba wako ili niweze kukushauri vizuri. Am so interested sana na hii CASE yako, Ingawa huwa na charge kwa Ushauri wa mambo haya but wewe ningekusaidia Bure ili nikuonyesha DUNIA halisi. Kama ankali akiona poa email yangu hii hapa : gtheangel_1@yahoo.co.uk contact me nitakusaidia na mtihani huu.

    ReplyDelete
  72. mmhh!! kwakuwa umesema huyo mdada wa pili ni rafiki na mpo wawazi kuelezana kila kitu, nijuavyo wanaume wengi mlivyo,hapo umeshamweleza weakness za mchumbako zote, na sisi wanawake tulivyo,hapo huyo dada anatumi hiyo as a loop hole kukuteka,so far eshajua kitu gani hupendi kipi unapenda. Napenda kufahamu,kwanini wewe na mchumbako hamko wawazi kama huyu rafiki mpya? kwa mtazamo wangu huyo rafiki mpya anatufauta mwanaume huyo,am sure atakuwa keshafika age ambayo anahitaji kuwa na familia,so wewe ushajilengesha kwake.
    Wazuri hawaishi kaka yangu, nakushauri endelea na mchumbako kama kawaida,sijui mna muda gani kwenye relation,lkn itakuwa mshafahamiana a to z mpaka umefikia hatua ya kutaka kumtambulisha kwenu....

    ReplyDelete
  73. Hapa si mahala pake wewe......nenda kaulize mambo haya kwenye magazeti ya udaku!! kila mtu angeleta matatizo yake ya mapenzi kwenye blog hii ingekuwaje!!?

    ReplyDelete
  74. Just answer me these couple of questions? (1)Kama ingekuwa wewe ndio huyo mchumba wako akapata mtu mwengine ungelihisi vipi kukuacha at the last minute?

    Kumbuka wahenga walisema,Usiwache mbachao kwa msala upitao.

    Na Kumbuka mbali ya cha zamani ni dhahabu pia Mwenda tezi na Omo hurudia ngamani.wengi yamewakuta kama hivi wanakimbia kwa wake zao kwenda kwa vimada kisha wanakuja kujuta baadae.

    (2)Na Je huyo mchumba wako ulichaguliwa au umemchagua mwenyewe? na mna muda gani?
    kwa hiyo inaonesha akitokea mwengine pia utamuacha huyo wa pili.KUMBUKA WAZURI HAWESHI.

    mdau mmoja amekupa ushauri mzuri kwanza onja onja huyo mpia ujue utamu wake,kisha ndio amua,lakini kumbuka you can not judge book by cover huyo wa zamani ushalisoma daftari na ushalijua uzuri kwa hiyo tahadhari kwanza mwambie akacheki HIV pia.
    NA CHA MWISHO MICHUZI ONDOA HII VERIFICATION INASUMBUA SANA KUWEKA MAONI FANYA KAMA JR UNAWEKA TU MAONI BILA KUTYPE.

    ReplyDelete
  75. Ndugu mtaka yote sikiliza maoni yangu kwa makini.Hawa wachumba wako wote wawili fanya utafiti kwanza wa faimilia zao zikoje nikiwa na maana: wanapendana ,wanashirikiana,wana umoja na je ni wacha mungu au wacha shetani ukisha fanya hivyo mchukue ambae wanavipengele vizuri hapo juu.Nasema hivi kwa sababu hata kama unampenda wife lakini familia ni shetani utajikuta kutwa unakwenda kama mwendawazimu hujijui mbele wala nyuma.Uzuri wa sura sio kipaumbele sana siku hizi wastani ndio kizuri na tabia yake na famili yake pamoja.Pia usitilie sana maanani machine kwani taka ni dakika moja.

    ReplyDelete
  76. Kaka pole sana,mimi ushauri wangu nakuomba tu uendelee na mchumba wako wa awali.Mimi ni mwanamke nakawaida yetu,kama unamtaka bwana naukagundua ulikuwa na mchumba,nitakuwa mzuri sana kwako mambo yote,kukuheshimu sana wewe na watu wote wanaokufahamu wewe ilimradi nikupate basi,ukishafunga ndoa na mimi,hayo yote yamekuisha utaona rangi zote.ushauri wa wazazi pia utakusaidia kuweza kupata ndoa njema.mchumba wako wa kwanza naona atakufaa.

    ReplyDelete
  77. Kijana kipya kinyemi, ushauri wangu ni kwamba take ur time and no rush. Maana hata ukija kumuoa huyu mpya u will see wapya wengine na pia inaonyesha kwamba unatamaa na huridhiki na demu mmoja. Jitahidi kuomba na mungu atakufungulia na kukuonyesha mke mwema na si kuchange wachumba kama nguo. Kitu kingine ni kwa utakuja ku blow trust from your family and friend maana apparently you are showing that u r very unstable kwa hiyo kuwa mwangalia maana usiache mbachao kwa msaala upitao. Sali sana kijana na mungu yupo maana I see utakuja kujuta mbeleni. Pia u need to be rational fanya maamuzi yako siyo kwa moyo bali akili. Chunga sana na acha kuwa desparate and irational.
    Mdau Maryland, USA

    ReplyDelete
  78. Pole kaka,
    Kuna vitu muhimu unatakiwa ujiulize, umesema ulimtambulisha kwa mchumba wako, halafu hapo mwishoni ukamalizia kuwa ni msomi na amesema ananipenda!! So inawezekana kabisa anakutia majaribuni mana anajua wazi una mchumba na unakaribia kuoa, Kingine huyo dada na uzuri wote uliomsifia na kudai kuwa ni WIFE MATERIAL hana mtu??u usiniambie kuwa kwa uzuri uliousifia hapa hakuna vijana waliotaka kumuoa?? kwanini yupo available kama kweli ana sifa zote za kuwa mwanamke? So na yeye atamuacha mpenzi wake ama inakuwaje?? Mh siamini kama she is single na wewe ndo mtu wakwanza kukupenda!!

    ReplyDelete
  79. sometimes I careMarch 23, 2012

    Ningetengeneza Hit-romantic movie with that personal experience...the trick part is ur endings depends on how u play the love game...Be careful kid

    ReplyDelete
  80. Mwenzetu kaomba ushauri kama hauna cha kumshauri ni afadhali ukae kimya kuliko kutumia maneno ya kejeli.

    ReplyDelete
  81. Usiache mbachao (kijimkeka cha walalahoi) kwa msala au hata zulia lipitalo. Wewe unadhani unamjua huyo "friend" wako mpya, lakini kutokana na nilivyosoma uliyoyasema hapa juu, nina hakika unamjua vizuri zaidi huyo mchumba wako. Tafakari sana usije ukainingia katika mtego wa huyo "home wrecker" na kumsononesha mchumba wako. Tafakari sana. Majuto ni mjukuu. Usije tu ukalilia maziwa yaliyokwishamwagika bro! Yaani ukishayamwaga maji hayatozoleka tena.

    ReplyDelete
  82. KD Changanya zege, lakini ukiisha limwaga likikauka halijengeki

    ReplyDelete
  83. Unachotakiwa kujua ni sifa kuu za mke sahihi wa kuoa na ndizo nitakupa hapa;
    1.Muwe mnaamini Mungu mmoja.
    2.Awe anakusikiliza.
    3.Awe anakuamini.
    Mengine yanarekebika au Kuvumilika.

    ReplyDelete
  84. OA WOTEWAWILI

    ReplyDelete
  85. kama ukimwacha huyu mchumba wako inamaanisha ni tabia yako ya kubadilisha wanawake kicho ni kipimo cha jinsi ulivyokomaa kimawazo na kimaisha biashara za kubadilisha wanawake sasa hivi ziko wapi?hapo ulipo waweza kuta hata nyumba huna wakimbilia kubadilisha wanawake, hiyo si tabia nzuri kama umemwona huyo anafaa kuliko mchumba wako hata yeye kuna aliyemzidi na siku moja utamwona hafai.tulia wanawake sio sura kijana utakufa ungali mdogo.

    ReplyDelete
  86. Mnafiki mkubwa wewe, ushatembea na dada wa watu kwa muda wote huo halafu unataka kumwacha..thubutu..utajuta

    ReplyDelete
  87. Sikiliza rafiki, hapo huchelewi kucheza pata potea. kabla hujafanya ushauri wa mwisho zingatia yafuatayo:
    1. Moyo wako unampenda nani zaidi.
    2. Je ni nani kati yao anaeweza kukuvumilia katika shida?
    3. Je ni nani kati yao ana mapenzi ya kweli kwako?
    4. Je ni nani kati yao ni mvumilivu na mkweli nk
    Umeeleza zaidi kuhusu sifa za huyu mdada mpya, vipi kuhusu mchumba wako. Nakushauri upime na kumuomba Mungu kabla hujafanya uamuzi wa busara na si bora uamuzi.
    Napenda kukupa mfano tu, mimi binafsi ni mdada na nilishakuwa katika situation kama hiyo na kwa bahati mbaya nikadondokea kwa new catch thinking that we have that bond forever. Ukweli ni kwamba, mara baada ya kujuana kimwili wote wawili tukaja kugundua kwamaba it was lust na ilibidi wote tuachane. kwahiyo zingatia ushauri wangu na wadau wote isije ikawa unachodhani ni mapenzi ya kwali kwa huyo dada ni matamanio tu.

    ReplyDelete
  88. Chukua tahadhari kaka maana wa zamani umeshajua mapungufu yake na ndo maana ni rahisi kumtofautisha na huyo mpya, chukua muda msome tabia zake usijesema ningelijua!!!

    ReplyDelete
  89. Sababu ya kumwacha mtu kwa kupata amabaye unahisi unaendana naye sana si sababu tosha ya kwanini huwezi kumuoa huyu wa kwanza. Kaka angalia sana utakuja juta huo ndo ukweli. Hawa wanawake ambao ndiyo inaonekana mnaclick vibaya mno katika kipindi cha muda mfupi ndo hatari kupita maelezo. Bado hujalipata file lake vilivyo. Mi ningekushauri ufikirie mara mbili mbili na umshu\irikishe mungu kabla hujafanya maamuzi. huyo rafiki yako wa sasa hivi alikuwa wapi siku zote na hana mchumba mpaka sasa hivi. Jiulize sana. Mwaka mmoja hautoshi kumjua mtu. Utapokuja kumjua vizuri wakati umemwacha mliyetoka naye mbali ndo utajuta. Mlikuwa naye kwenye raha na shida. Mapenzi yanainvolve vitu vingi sana kuna kugombana kuna kupatana yaani ndo mnafahamiana vizuri kwenye process.

    ReplyDelete
  90. usihangaike sana kutafuta njia ya kumwaga huyo wa kwanza....alafu usiusikilizie saaana moyo..ushauri wangu mtie mimba uyo mwanamke mpya umalize shughuli...ACTIONs speak louder then WORDs...

    ReplyDelete
  91. Mdau KD,

    Ndugu yetu IKIWA WEWE NI MUISLAMU KWA KUOA WOTE WAWILI,

    JE, UTAZIMUDU TAULO MBILI ZA VYUMBA VIWILI TOFAUTI KUNING'INIA MILANGONI CHUMBA CHA MKE MKUBWA NA MKE MDOGO?

    Mambo yanaenda kwa zamu utazingatia ratiba na utakuwa mwadilifu?

    JE, INA MAANA UTATOSHEKA?... INAONEKANA UNAYO HULKA YA KUPENDA PENDA WEWE !

    ReplyDelete
  92. "Kipya kinyemi"

    Hata huyo wa kwanza hukukurupuka,na dhahiri ulimchagua mwenyewe hadi ukamfanya mchumba.Au wataka kusema ulitafutiwa na wazazi!

    Huko ni kutokuwa na msimamo,halafu unataka watu wengine wakushauri.Itakuja siku utataka watu kukushauri kuacha mke.Utakuwaje umma wote ukushauri kuhusu hili?

    Utahangaika sana "the beautiful ones are not yet born."Ushauri utakuponza.Uzuri ni tabia si sura.Wewe wadhani kuna mwanamke mbaya!Tizama kila mwanamke ana mume au hawala unayesema mbaya au unayesema mzuri.Kuna kitu mwanamume anataka kwa mwanamke sidhani kama ni sura.

    Uzuri Mungu alitupa mwanamke,lakini hakutupa mfano wa picha ya kuangalizia ili kuweka kipimo cha uzuri au ubaya.

    Hivyo ndugu yangu yako wewe ni tamaa,na hata ukioa tamaa hiyo utaendelea nayo.Kaa chonjo.

    ReplyDelete
  93. Jibu ni hili:-

    Mithali 19:14 "Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kwa babaye; bali mke mwenye busara, mtu hupewa na Mungu."

    Fanya mfungo huku ukijitenga na wote wawili baada ya kuwaambia kila mmoja wao kuwa unahitaji muda wa kutafakari jambo hili muhimu kwenye maisha yako. Katika kipindi hicho cha mfungo epuka kukutana na kimwili na vishawishi huku ukiomba Mungu akuonyeshe aliye wako. Utahitaji busara binafsi na wala si za blog ya jamii kutambua jibu la Mungu...you will see the true colors for each of them!
    Soma pia 1 Wafalme 3:22-27 itakusaidia. All the best and May the Lord guide you!

    ReplyDelete
  94. kwenye relation nyingi inapokuja ishu ya kuoa ni mwanamke ndio muathirika mkubwa sana, imagine yeye umempotezea muda kiasi gani au na yeye alishawakataa wangapi kwa ajili yako? maana ninavyoamini mimi wazuri hawaishi na bado wanazaliwa unless otherwise unipe vigezo vingine, mambo kama adabu, anakusalimia vizuri, mzuri are just minor braza namtu anaweza kupritend as amekuona bado kijana na yeye amejua unaweza kutangaza nia.
    Msemo mmoja wa kiswahili unasema ukitaka kusafiri bus la kwanza utakaloingia ndio hilo kubadilisha kunaleta bad lucky. Ni ushauri tu take it or leave, usimuche mchumba wako kama huna exposure za wasichana basi anza na huyo rafiki na more girls kama 6 then ndio utajua nani wife material.

    ReplyDelete
  95. Jamani penzi jipya siku zote ni tamu , angalia saaana huyo mpya. kwa sasa sitisha kuoa wote wawili kwanza akili yake ikae sawa. hata huyo mpya mpe muda, maana wadada wenye heshima ukisema unamchumba wanaheshimu sasa yeyey tayari kakwambia anakupenda, ukipata chungu kipya usitupe cha zamani, hayao ni mapenzi ya mwanzo tu hakuna chochote.

    ReplyDelete
  96. WEWE KAKA INAONYESHA HUJATULIA KABISAA!TENA WALA HUMUOGOPI MUNGU!NINA UHAKIKA NA HUYO UKISHA ANZA KUMCHUMBIA UKAJA KUONA MWINGINE UTAONA NA YEYE HAFAI,,KITABIA NI MUHUNI,,JARIBU KUKAA CHINI UJIWEKE NAFSI YA HUYO MCHUMBA WA MWANZO!INAUMA SANA SANA WEWE!UNAONA NI VIZURI KUMFANYIA MABAYA MWENZIO,WEWE UKITENDEWA KITENDO KAMA HICHO NA MWENZAKO UTAJISIKIAJE?...KWANI ULIVYOMTANGAZIA UCHUMBA MWANZO,HUKUONA KUWA HAFAI KUWA MKE WAKO?,,NA KWA NINI SASA UNATAKA KUMTIA KATIKA MAWAZO NA FIKRA KATIKA MAISHA YAKE YOTE?,,HUYO DADA MPYA ACHA AENDELEE KUWA RAFIKI TUU!NAKUSIHI USIMFANYIE HIVYO DADA WA WATU UTAMUUWA,,NA WEWE KAMA WEWE,MWANAMME ACHA URAFIKI NA MABINT NI HATARI SANA,,UTAACHA WACHUMBA MPAKA WAKE,,
    MUOE HUYO WA ZAMANI,,MWENYEZI MUNGU ATAWAJA'ALIENI MAPENZI KATI YENU,,,,NA IKITOKEA LABDA HAMKUPENDANA SANA AU KUNA VITABIA FLANI FLANI VITAJITOKEZA,HUTOJUTA SANA,ILA UKIMUOA HUYU MPYA KIKITOKEA KITU CHOCHOTE UTAJUUUUUUTTTAAA KUKUTANA NAE!

    AHLAM,,,UK

    ReplyDelete
  97. jamani mimi ni mwanamke na nilishaachwa kwa mtindo huo huo wakati tukisubiri vikao vya harusi vianza, jamani inauma na inatesa haina mfano. naamini wachangiaji wengi hapa ni wanaume kutokana na comments wanazotoa. cha kwanza huyo jamaa atueleze na yeye tabia zake.. na tabia za huyo wa kwanza ili tuweze kuona yupi ni match yake.

    kwa kuwa wanawake ni wengi zaidi ya wanaume then mchezo ndio huo kwa wanaume. ni - kuonja na kuacha na kuonja na kuacha kwa kisingizio cha kuwa anachagua "life partner" ni yupi. Mungu atunusuru! nakushauri upige magoti, ukeshe na kuomba ili uweze kuendelea na mipango yako ya harusi ya huyo wa kwanza.... otherwise onja onja ndio maana gonjwa la ukimwi haliishi.

    ReplyDelete
  98. Soma kitabu cha form three: Three suitors one husband!

    ReplyDelete
  99. Wote nyie ni wasaniii huyo dada msanii na wewe msanii
    Hana tabia nzuri kama ulivyosema hiyo sifa ifute asingeweza kukutia majaribuni wakati wewe umeshamtambulisha kwa mchumba wako uliye nae
    Hivyo kuhusu heshima hana ni msaniii tu huyo na wewe pia huwezi kuanzisha mahusiano mapya wakati tayari uko na mchumba wako sana ni usaniii

    ReplyDelete
  100. KD, wakale husema BETTER THE DEVIL YOU KNOW THAN THE ANGEL YOU DON'T KNOW.

    Huyu wa pili ulianza naye kama rafiki, na ndiyo why ukawa free kwake kama rafiki (japo wa kike), sasa tamaa zako za mwili juu yake na tabia yetu ya (kiafrika) yakuwa ni vigumu kabisa kwa mwanaume na mwanamke wakawa marafiki bila mapenzi ndiyo kinacho kutesa.

    Je, hizo tabia ulizopenda kwa huyu wapili, huwezi kumweleleza mchumba wako ili ajue nini unapenda?

    Kwakua sababu ulizozisema juu ya kwanini umpende huyo wapili sio tu hazina msingi, lakini inaonyesha wewe ni dhaifu. Kwasababu mapungufu unayoyaeleza juu ya mchumba wako zinarekebishika UKIJUA jinsi ya KUWASILIANA. Lakini pia, siku ukiwa na V8 halafu ukawa unampa dada mmoja lifti na akawa anakuamkia utahamia kwake kama siyo kuhama kwako.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  101. 100% confidence levelMarch 23, 2012

    Michuzi! nianze na kukushangaa wewe binafsi!!unaonenekana unapenda dhana za mapenzi zaidi!
    Pili nawashangaa wachangiaji wote hapo juu!hawajui wanachokifanya!!mwenyezi Mungu awasamehe! sana!!!!!
    Jifunzeni yaliyo yangu!na msifunge nira na wasio amini!!na waacheni wafu wazike wafu wao!!!
    Soma biblia upate maarifa!!!!

    ReplyDelete
  102. Wazuri hawaishi. Muhimu ni kutulia. Kama wewe roho iko juu juu tu uonapo msichana mpya mzuri, nakuapia hata siku ya harusi, maid wa kike anaweza kuvaa na kujipamba vizuri akavutia, sasa badala ya kumwangalia huyu binti mwizi wa wachumba za watu, utabakia kumwangalia huyo maid. Wazuri wapo, wataendelea kuwepo, hata huyo wa mwanzo ulimwona mzuri ndo maana ukamchagua. Nguo mpya wakati wote ufunika ya zamani, lakini na yenyewe ukisha izoea utatamani kununua mpya tena. Nafikiri umenielewa!!!!

    ReplyDelete
  103. HEHEHEEE UZINIFU TU NDIO UNAKUSUMBUA, hakuna mahali wakakaa watu wawili wa jinsia tofauti mkatembeleana mpaka vyumbani kwenu shetani asiwepo kati yenu. Tena kuwa kwenu karibu kumepelekea mpaka kula tundi, sasa umenogewa unataka kuchonga mzinga. Ila kumbuka tu kuwa malipo ni hapa hapa duniani maana utaliwa zako wakati bwana wake wa ukweli atakapotangaza ndoa wewe utatemwa kama bigijii. Kwani hakuna mwanamke mwenye sifa ulizotaja yuko single, kama hana kijana mwenzie wa kutoka nae kama wewe basi atakuwa na buzi lake au ATM inayompendezesha. Usione vyaelea jua vimeundwa hivyo ama kuna mume wa mtu anahudumia hapo na vile mume wa mtu hawezi kumpa ndoa, msichana kajilengesha umuoe. UTAENDELEA KUSHEA MPAKA UTASHANGAA KAMA WAUME WENZIO WANAVYOSERVIWA KWA MAFUNGU! MJINI HAPA AKILI KUMKICHWA SIKU HIZI WASICHANA TUNATAKA NDOA ILI TUPATE SHEREHE ZA HARUSI, TUVAE SHELA NA TUPEWE MIJIZAWADI KWENYE KITCHEN PARTY! and that is from the horses mouth, we can say anything to fulfil our goals na we can do anything to make men infatuated with us, chezea wanawake wewe! kwisha habari yako!

    ReplyDelete
  104. Hivi ulisema mdada wa pili anatabia nzuri ? Je wizi ni moja ya tabia nzuri? wakati ashajua una mchumba mwenye tabia nzuri angekaa mbali na wewe mkawa ni rafiki tu wa familia,

    Kaa ukijua Hakika ya zinaa ni deni na kama haijakjufika wewe basi ni mtu wa familia wako,ikiwa wewe unampiga chini huyo wa zamani basi ujue huyo mpya atakupiga chini vile vile atatokea tu shabab mwengine,
    Nyamaffffff 3#$@u#&*)???//

    ReplyDelete
  105. baki na shemeji yetu wa mwanzo, kaka usiyumbe plz.kidada chapili hujamjua vizuri try to learn ha moo.

    ReplyDelete
  106. Kumbuka siku za mwanzo ulivyompenda huyo wa zamani! Sasa hivi unahisi kama unampenda zaidi huyo mpya sababu una mahali pa kulinganishia, na zaidi sana ni mchuma tu hujamjua vizuri huyo wa pili. Waulize walioa na kuacha, mara nyingi sana wanatamani warudi kwa wakwanza wanashindwa! Kama umekuwa na muda mrefu na huyo wa kwanza (kuliko huyo wa pili) basi achana na huyo wa pili. Kama umekuwa nao muda sawa, basi endelea na wapi, lakini mweleze wa kwanza mapema kabisa!

    ReplyDelete
  107. Uwe muangalifu sana na huyo wa pili. Kama alijua kwamba una mpenzi wako na mnapanga kuoana lakini bado akakubali kutoka na wewe bila kumjali mpenzi wako, basi usishangae kama siku za mbeleni akiamua kukuacha na kwenda kwa mwanaume mwingine bila kujali hisia zako... what goes around comes around... Nakushauri umchunguze (na huyo #2) na mjuane tabia zenu kama zinaiva wakati wa raha na shida. Mara nyingi mwanzo ni mtamu kwennye mapenzi na hakuna mazozano, lakini muda unavyoenda na mnavyotumia muda mwingi pamoja ndio utajua kasoro zake...Tumia busara na mjulishe mpenzi wako wa sasa kwamba umeamua kusitisha suala la engagement mpako hapo utakapofikia uamuzi muafaka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...