Brother Michuzi habari zako?
Naomba uniwekee suali langu hili kwenye blog yako. Tatizo langu ni kuwa natafuta website za 
uhakika huko nyumbani zinazotangaza kazi mbali mbali za nchini tanzania na afrika mashariki.
Ninaposema za uhakika ninakusudia sio zile za kubabaishana, 
nitashukuru kama atatokea yeyote
yule kunisaida kwa shida hii. 

Mdau Forodhani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Try...jobstanzania.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. Ahsante sana Mdau wa Forodhani huko Majuu kwa kuamua kurudi nyumbani Bongo, na kuachana na Kibarua cha kitumwa kwa Wazungu cha kubeba ma box !

    Angalia hizi hapa:

    1.naombakazi.blogspot.com

    2.google TAESA ili mradi uwe professional na unavyo veti

    3.www.vijana.co.tz

    UMELILIA CHAI MWENYEWE SIO UPEWE KIKOMBE UANZE KULALAMIKA UNAUNGUA!

    ILI MRADI UMETOKA MAJUU ISIPOKUWA USIWE MCHAGUZI WA MAENEO YA KAZI UNAWEZA KUPANGIWA MIKOANI AU VIJIJINI USILETE MAMBO YA KIMUJINI MUJINI UNAWEZA TUPWA BIHARAMULO, AU NEWALA-MTWARA HUKOOO!

    ReplyDelete
  3. nenda www.tanzanianewslink.com

    ReplyDelete
  4. What's up with all that scarcastic comments...."Kazi za kitubwa" and so on... Can you just help somebody without rub it in or offending others. You make a choice to live Tanzania and deals with power ratio, inequality and all other challenges comes with it. And they choose to live abroad and face all challenges comes with it. Get over it...Don be a hater!!!

    ReplyDelete
  5. Watu wengine vichwa box tupu.
    Mdau wa pili unayesema jamaa majuu aachane na kazi za kitumwa za kubeba box unamaanisha nini?
    Upuuzi mtupu, ACHENI HUU MTINDO WA KUDHARAU KAZI, ndio maana Afrika hatusongi mbele. majuu kazi ni kazi bila kujali ya aina gani ili mradi unalipwa kwa haki.
    Tena nafikiri watu wakisikia kubeba box wanafikiri ni kama kule kariakoo shimoni kubeba mizigo, kama mliambiwa hivyo mmedanganyika.
    kila kitu majuu standard na sherika za kazi usalama kazini na afya vinapewa kipaumbela.

    ReplyDelete
  6. Kubeba box, ni kubeba box tu. Haijalishi walibeba kwa kichwa, mkokoteni au 'forklift'. Lakini ikiwa una elimu ya kawaida, hakuna tatizo, kwa ulaya hii ni kazi ya kawaida tu. Balaa ni pale mshikaji unakuta kasoma kweli, ana masters lakini anaingia mtaani, na kuishi ki-gorilla, na anaishia kufanya kazi hizo za kubeba box, au kufagia. Swali, masters kwa mtanzania ni kiwango cha elimu cha kufanya kazi hizo ulaya? Mtu kama huyo anakuwa mpumbavu, anatakiwa arudi bongo ili atafute kazi au mradi wa maana wa kufanya kama ikiwa hawezi kutafuta kazi za 'profession' yake ulaya.

    ReplyDelete
  7. Ubebaji Box ni Utumwa acheni kujitetea tena ni woga wa maisha haiwezekani usome kwa gharama kubwa halafu unakuja bebeshwa maboxi ahhh hii hapana!

    Zaidi ya hapo huyo anaetaka kurudi Nyumbani aje atafute kazi akikosa bora akalime Kijijini akiwa Tanzania ajenge nchi yetu badala ya kubeba ma box Majuu!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...