Mtoto anayeonekana kwenye picha amepotea tangu tarehe 16/02/2012, jitihada mbalimbali za kumtafuta zimefanyika lakini bila mafanikio.Anaitwa Felista Sialeo,ni mwanafunzi wa darasa la tano,shule ya msingi Mtambani,kwa mara ya mwisho alivaa sare ya shule ,yaani sketi ya blue na shati jeupe,alikuwa anaishi Tabata magengeni.

Kwa yeyote atakaye mwona,apige namba 0755382300 au 0758491854 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Loh poleni.Na mimi nina binti wa darasa la tano analingana na huyu.Naweza kuhisi uchungu mlionao wazazi/walezi wake.Hope atapatikana..Bado mdogo huyu kama kuna m2 kamtorosha apelekwe kwenye mkono wa sheria.Kuna wengine tunawaona humu wamepotea tukiangalia umri wao mkubwa "tunahisi walipo" lakini siyo huyu..huyu ni mdogo sana.

    David V

    ReplyDelete
  2. I hope she's still alive!

    ReplyDelete
  3. Duh inaniuma, nilifiwa na mtot wangu the same age, nahisi uchungu, Mola InshaALLAh ataajaalia kupatikana hai na salama. mzidi kufanya maombi

    ReplyDelete
  4. Hatua kali zichukuliwe kwa atakaehusika na kupotea kwa Binti huyu wa Darasa la Tano !

    Mambo kama haya sio mtu ahusike halafu anapewa dhamana anaonekana anatamba Mtaani hii sasa imetosha HAPANA KABISA!

    ReplyDelete
  5. JAMANI WAZAZI POLENI SANA,HII YAWEZEKANA MTOTO KACHUKULIWA NA WAFANYABIASHARA WANAOTUMIA BINADAM WENZAO KUPATA PESA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...