Mazoezi ya kucheza yakieendelea kutoka kwa Dansa wa Twanga Pepeta Mandela alievaa t shirt ya kijani.

Baada ya kumaliza mchakato wa usajili na usaili wa kutafuta vipaji vipya ndani ya Music Academy Tanzania hatua iliyofuatia ni kuanza rasmi mazoezi ya nguvu yatakayoweza kuwaandaa na kuwanoa vyema wana academia hao ambao wamefaulu kupita katika mchujo wa kwanza chini ya usimamizi kutoka kwa gwiji na nguli wa Muziki Tanzania Mzee Kalala, ASET na URBAN PULSE CREATIVE. Pia kwa upande wa kucheza dansa mkali kutoka Twanga Pepeta Mandela atakua akitoa mafunzo katika fani hiyo.

Lengo la kuanzisha Music Academy hii ni kufundisha na kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yatakuwa yakifanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
wana academia wakiimba wimbo walioutunga wenyewe.
Mzee Hamza Kalala akiwapa somo la muziki wana academia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ankal

    Hizi picha ziweke vizuri ktk Maktaba ya Blogu ya Jamii kwa kuwa ni utamaduni wetu mtu akipanda ngazi ya Maisha na kuwa JUU anakosa Ubinaadamu,Heshima, Utu kwa umaarufu na Ukubwa alioupata.

    Mfano mzuri ni ile picha ya Waheshimiwa Wabunge mwaka 1984 wakipanda bus la kata shingo kwenda Dodoma Bungeni.

    Sasa picha hii itafaa kuwakumbusha Ma Nyota hawa wa Muziki wa baadae walikotokea wakiwa Manyasini ( Ma-Underground! )

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...