Wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,wakishiliki katika zozi la uoteshaji miti katika chanzo cha maji cha Shiri.
Mkurugenzi wa mamlaka ya ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA) Anthony Kasonta akifurahia jambo na wafanyakazi wa mamlaka hiyo wakati wa zozi la uoteshaji miti katika chanzo cha maji cha Shiri.
Afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi(MUWSA)akiotesha mmoja ya miti iliyooteshwa katika chanzo hicho cha maji.
Wafanyakazi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Moshi,wakinawa mikono yao katika chanzo cha maji cha Shiri mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uoteshaji miti katika chanzo hicho.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii - Moshi.

Imeelezwa kuwa endapo uharibifu wa mazingira ukiendelea kufanyika Mkoani Kilimanjaro kuna hatari ya ukame wa kuendelea kuongezeka,tofauti na hali ilivyo sasa ambayo imechangia kukauka kwa vyanzo vya maji na mabadiliko hewa yanayosababisha kuwepo kwa joto kali.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi maji na maji taka Mjini Moshi (MUWSA) Anthony Kasonta wakati wa zoezi la upandaji miti kwenye chanzo cha maji cha shiri kilichopo Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji siyo nzuri licha ya kuwepo kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni kutokana na ukame ambaoo ulikuwa umesababishwa na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti ovyo ambayo imesababisha kukaukwa kwa uoto wa asili na vyanzo vya maji.

Alisema kuwa zoezi hilo la kupanda miti kwenye vyanzo vya maji litakua endelevu,pamoja na kumuunga mkoni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama katika jitihada za kutunza mazingira kwa kupiga vita ukataji wa miti na kupanda miti.

Akizungumzia suala la uhaba wa maji lililosababishwa na ukame hivyo kuwepo kwa mgao wa maji kwa manispaa ya Moshi,hali ya upatikanaji wa maji bado haijarudi katika hali ya kawaida licha ya mvua zilizonyesha siku za hivi karibuni hivyo kusema bado mgao huo unaendlelea ila hauna makali kama ilivyokuwa awali.

Jumla ya miti 600 ilipandwa katika chanzo hicho cha maji ambayo itatunzwa na mamlaka hiyo,huku akisema kuwa mwanzo wa maji katika vyanzo vilivyopo mbali kama mlima Kilimanjaro hivyo wananchi wanatakiwa kutunza mazingira bila kujali kwamba kuna chanzo cha maji au hamna.

Kasonta alisema kuwa suala la uharibifu wa mazingira ndilo lilipolekea kuwepo kwa mgao wa maji ambao ni mara ya kwaza mgao wa maji kuwepo Mjini hapa,huku akisema mazingira yasipotunzwa kizazi kinachokuja kinaweza kukosa kabisa maji pamoja na miti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Cha kushangaza Tanzania kote wanaotesha miti bila kuiziba na miwaya na kuifwatilia kadri inavyokuwa hadi isiwe chakula cha mbuzi na ngombe ndio waiachie huru ,bila hivyo baada ya wiki utakuta hakuna mti hata mmoja

    ReplyDelete
  2. It took them too long to come and take this action. In the actual fact we would appreciate if they tell us what plans do they have in that reserve land apart from planting trees which will be either be cut immediately after they have grown or used as firewood before maturity. We are interested to hear and see how will they preseve that land for the intended purpose. Not forgeting to involve the neighbood to be their watchdog.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...