MWANAFUNZI wa kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya St. Anthony Mbagala, mkoani Dar es Salaam, Franco Donald Kisongo (18), amepotea jijini humo.
 Shangazi wa kijana huyo, Adelaide Kisongo amesema, Franco ni mgeni jijini Dar es Salaam amepotea tangu Jumapili asubuhi ikiwa ni siku nne tu tangu ajiunge na shule hiyo kuanza masomo ya kidato cha tano. 
Kwa mujibu wa Adelaide, kijana huyo aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa alikuwa anakwenda kwa shangazi yake Kariakoo, hakufika huko, na pia hakurudi shule na hadi sasa haijulikani alipo. 
Amesema, walimu na walezi wa kijana huyo Mrangi, wametoa taarifa katika vituo vya Polisi Mbagala Kizuiani, Chang’ombe na Msimbazi, na wanatumia RB namba 3343/2012 ya kituo cha Msimbazi kumtafuta. 
Kwa yeyote mwenye taarifa kuhusu mahali alipo kijana huyo anaombwa kutoa taarifa kituo chochote cha polisi au kuwasiliana na wenye namba zifuatazo za simu. 0784- 384035,  0717-371763,  0713- 761006, na 0715- 247544

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. poleni sana tutasaidiana lakini akipatikana popote pia mtujulishe sio kukaa kimya. Je ametoka mkoa gani? anapenda kutembelea wapi? na o level kasoma wapi?

    ReplyDelete
  2. Angekuwa mtoto wa kike waosha vinywa wangesema kaenda kwa bwana, haya huyu wa kiumu mwasemame?

    ReplyDelete
  3. Kama wa kike kaenda kwa bwana wa kiume kaenda kwa bibi. Mwenyezi Mungu awape subira wanafamilia na amuwezeshe kurudi nyumbani salama

    ReplyDelete
  4. nendeni muangalie na mochwari

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...