Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akikung'guta gitaa la solo leo leo alipopata fursa ya kipekee kujiunga na Bendi ya Twanga Pepeta "Kisima Cha Buruduni" na kufanya nao mazoezi ndani ya ofisi za Aset. Baada ya kufanya makamuzi ya nguvu ilidhihirika wazi kwamba ukiachilia mbali siasa Nape ni msanii mkali wa kuimba, na kupiga vyombo mbalimbali vya muziki. Aidha Mkurugenzi wa Aset Asha Baraka alifurahishwa na kumshukuru sana Nape kuja kuwatembelea na kuwapa sapoti, vilevile alimuahidi kuwa nafasi yake itakua wazi kwenye bendi mara tu atakapo amua kuachia ngazi kutoka katika jukwaa la siasa na kuamua kujiunga katika tasnia ya muziki.
Nape akipapasa Kinanda
![]() |
Asha Baraka akimfurahia Nape wakati akifanya vitu vyake |
Kija akimwangalia kwa makini Nape akipiga gitaa la Bass
Nape Nnauye akipiga Drums huku Msafiri Diouf akiimba
Michuzi, huyu jamaa Diof alipotea hivi majuzi tu. Je alirudi lini na alikuwa wapi? Tupe habari.
ReplyDeleteNaamini kuwa mara nyingi watoto wengi hufata nyayo za baba au mama,huyu kijana wetu Nape kafuata nyayo za marehemu baba yake kwa wasiokuwa wakimfahamu marehemu Brg Nnauye alikuwa mwana siasa,na pia alipenda muziki sana kiasi kwamba alikuwa na chombo cha muziki nyumbani kwake.Hongera sana Nape,you are good boy.
ReplyDeleteDah! Msafiri Diouf. Jamaa ana kipaji cha muziki lakini ndio hivyo tena. Kweli Mungu hakupi vyote.
ReplyDeletepapaa nape nadhani hii ndiyo inakufaa zaidi,siasani ni habari nzito kidogo.
ReplyDeletehapa unaweza kuwaburdiiiiisha watanzania kwa kina zaidi.sanasana ukizingatia pia lugha yako inavyofanana na hao,ushansoma mwana,kwani huko busara si lazima...
chego