Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mbunge wa
Kigoma Kaskazini Mh Zitto Kabwe

Na Zitto Kabwe
Kwanza niseme wazi kabisa kabisa kuwa Urais ninautaka.
Ninaamini ninao uwezo wa kuwa Rais. Ninaamini nina uzalendo wa kutosha na utashi wa kuleta mabadiliko stahili wa namna nchi yetu inavyoongozwa. Ninajua kuwa nchi yetu imesahau maendeleo ya watu na kujikita katika maendeleo ya vitu. 
Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content). Ninajua kuwa maendeleo vijijini yamesahaulika. Ninajua nchi yetu inahitaji Uongozi wa kufanya mabadiliko makubwa (transformation) badala ya mabadiliko ya juu juu (cosmetic change). 
Ninajua ‘transformation’ inahitaji maamuzi magumu yatakayoudhi wengi na hasa mabwana wakubwa wa nchi za magharibi mfano kuzuia nchi yetu kuuza malighafi tu. Ninajua rushwa, ufisadi na ubadhirifu wa Mali ya Umma ni kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu na kwamba lazima hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia na kutokomeza ufisadi. Ninajua rasilimali kama Madini, Mafuta na Gesi, Ardhi n.k. ni lazima zifaidishe wananchi wa nchi yetu.
Hivyo, nchi inahitaji Kiongozi wa juu atakayekabili changamoto hizi. Ninaamini ninaweza kuwaongoza Watanzania wenzangu kukabili changamoto hizi. Sio kazi rahisi lakini ni kazi ambayo lazima Mtanzania mmoja aifanye. Mimi nataka kuifanya. Nina uwezo wa kuifanya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Yes, mi sio mwanasiasa ila kijana ni hazina ya Taifa. and let be 2020. naunga mkono hojA YAKE.
    Ametulia, anajua kujenga hoja, haungi mkono kila hoja hata kama ni msimamo wa chama chake, hana kashfa etc

    ReplyDelete
  2. Good on you Zitto, ni wewe tu utakayeiokoa Tanzania maana uko very clean in all aspects. God love you and we love you 2.

    ReplyDelete
  3. Ndio ZITTO U deserve it!We need pople kama wewe! Tuko nyuma yako.Wewe ni kioo na chachu kwetu vijana wa Tanzania.
    Na iwe hivyo.Ni wakati wa mabadiliko tumechoka na mazoea!
    Enough is enough!!

    ReplyDelete
  4. Kusema kweli Zito hafai kabisa hata kuwa Mkuu wa Wilaya, ni mtu wa tamaa na ukubwa sana na ni Ndumi la kuwili.

    Kwa wale waliokuwa wanafuatilia vizuri mienendo yake hasa kutoa siri kwa baadhi ya mawaziri kuhusu waliyokusudia wapinzani na baadae kuwaomba pesa!

    Hufai Zito hata kidogo!

    ReplyDelete
  5. Anonymous Mon Mar 26, 07:26:00 AM 2012 Huoni hata aibu ya ulichoandika?? toa uthibitisho wa tuhuma ulizomtuhumu zito, ni siri gani alizotoa kwa mawaziri, hizo ni chuki binafsi tu, na kwakua huyo sio mtu wa kanisa ndio maana mnampaka matope, chadema mmezidi unafiki na safari hii mkibana kumpa zito nafasi hicho chama chenu kitasambaratika maana huyo kijana ana wafuasi ile mbaya,..kazi kwenu sasa maana ameshatangaza nia hadharani na sisi tutamuunga mkono.

    ReplyDelete
  6. wewe unayesema Zitto ana tamaa inaelekea humfahamu vizuri, tuulize tunaomfahamu tutakwambia,jamaa hana tamaa hata kidogo, ni mtu wa kujiscrifice mara zote.... kwahilo nitakukatalia daima

    ReplyDelete
  7. URAISI:

    Sawa umerusha kete ya kukitaka Kiti likini Itikadi ya Chama ulichokuwa nacho ina Dosari kubwa tatu (3)

    1-'Makundi' yaani Chama chenye kujali

    2-'Ukanda' wa Maeneo miongoni mwa Wanachama

    3-Mgawanyiko kwa Misingi ya 'Udini'

    Kwa hivyo basi kwa Dosari hizo kuu tatu (3) itakugharimu wewe kufikia huo Uraisi na pia Sio Chama sahihi na Itikadi yenye kutupatia dira ya makusudio yetu ambayo ni kuweza kujenga Umoja wa Kitaifa !

    ReplyDelete
  8. Umechemsha mawe kwa kuutaka Uraisi.

    Tatizo umekalia KUTI KAVU hapo ulipo kulingana na Mwelekeo ,Dira na Sera za Chama chako!

    ReplyDelete
  9. Uraisi utafikiriwa angalau 'kufikiriwa' kuupata endapo utafanya maamuzi magumu na kuwa jasiri kwa kubadili Rangi za Koti lako kutokea huko uliko kwenye Magwanda hadi Jezi za Yanga ingwawa wewe ni Mwana Msimbazi mzuri tu na jana Umemshinda Algeria Mwarabu!

    ReplyDelete
  10. Hapo hapo jaribu kuongea na huyo huyo unaeshikana nae mkono upige bao lako.

    Ni KIASI CHA KURUDISHA KADI YA UANACHAMA NA MAFUNZO YA MGAMBO ILI UUPATE URAISI !

    Utapata Uraisi labda ukihama kutokea Chadema na kwenda ile timu nyingine ya ya ya ya ....(napata kigugumizi kidogo kutamka).....ya ya ya ya ya ya ya ya ....ile.....''YANGA Kamali'' !

    ReplyDelete
  11. CHADEMA mna kazi ya ziada, kwanini Zito hakubaliani na Slaa na Mbowe?? utata mtupu huko! MAGUFULI CHUKUA NCHI TUSONGE MBELE!

    ReplyDelete
  12. oh maskini kabwe! mzuri sana kuandika na kughani! swali: umekwishafanya kitu gani, angalau kimoja, kinachokufanya ustahili japo kuwa mbunge achia mbali rais! ati mbunge wa kigoma wakati maisha yako yote dar es salaam! unaonaje ukinyamaza tu na kujilia hivo vimilioni unavochuruzisha kupitia ubunge bila kujali vinatoka wapi na nani anabeba mzigo wa kujaza hilo kapu? unaongelea kuwanufaisha wananchi na rasilimali za nchi, ati utapambana na mataifa ya magharibi! kwa silaha gani! bakora au mikwaju? huna ubavu, kaa kimya!

    ReplyDelete
  13. Ukiutaka Uraisi ongea na unaepeana nae mikono,,,huko kwingine utahangaika sana na mwisho utajikuta unajuta umeukosa bureee !

    ReplyDelete
  14. Mimi ni Chadema but Zitto BIG NO.

    ReplyDelete
  15. Akitetea kwa nini umri wa u-Rais uteremshwe ili kuwapatia vijana wanaostahili mwanya wa uongozi wa nchi, Mh. Zitto aliandika mambo mengi. Sentenso yake moja inafaa kusahihishwa isiambukize wengine. Aliiandika, “Ninajua kuwa hivi sasa viongozi wetu wengi wanaangalia zaidi mitindo (styles) badala ya mambo ya msingi (content).”

    Katika Kiingereza kuna maneno mengi yanayotumika katika kulinganisha kinyume. Kwa mifano, “styles” na “substances”; na “contents” na “contexts”.

    Mosi, Mh. Zitto katumia neno “styles” katika wingi. Lakini neno la pili ameliweka katika umoja, “content”.
    Sawa kuyaweka tote katika umoja au wingi.

    Pili, nina hakika Mh. Zitto alikuwa na maana ya “styles” na “substances”. Zaidi, “styles” zina “contents”, pia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...