Bwana Kaka, Pongezi kwa Simba SC na angalizo pia kwa Ushindi wake dhini ya timu ya ES ya Algeria. Yakhe ktk clip hii hapa chini ya timu ya Maroc Wac dhini ya Simba 2011 mpaka dakika ya 85 mpira ulikuwa bila bila. Ila Simba iliwapa fursa lukuki timu ya WAC ya Maroc kupachika mabao matatu ktk dakika za lala salama ingawa Kipa Juma Kaseja alijitahidi sana. Nawaomba viongozi wa Simba na wachezaji warudie kuangalia tena na tena mechi hii dhini ya Wac Maroc 2011 wasijerudia makosa na kuwapatia ushindi timu ya ES ya Algeria ktk siku kumi zijazo. MDAU MWEKUNDU |
Home
Unlabelled
Pongezi kwa Simba sc na pia angalizo toka kwa mdau mwekundu
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Kwa kweli hapa simba walishambuliwa sana na baadae walichoka na wakafundishwa kucheza mpira.
ReplyDeleteTanzania, kuanzia Taifa stars ya Poulsen, Yanga hadi Simba tunapenda sana kukaba badala ya kushambulia na kukaba. Unapokaba tu halafu ushambulii ndio hapo unaporuhusu mabao.
Pili, Timu za Tanzania including Taifa Stars, zinakaba tu halafu wachezaji hawajiamini. Wachezaji hawana uwezo wa kumiliki mpira, wakatulia wakapiga pasi na chenga za uhakika. Utawaona kabisa wakiwa na wasiwasi muda wote, kitu kinachowafanya wapoteze mipira na kuruhusu kuchezeshwa mchaka mchaka. Ndio maana hufungwa na waarabu na wakibahatika sana wanatoa sare.
Tatu, acheni tabia za kufikia kwenye hoteli zao. Jitafutieni hoteli zenu. Lipeni pesa zenu. Siku hizi teknolojia kubwa. Kwenye hoteli zao mtachunguzwa hadi wawajue vizuri kabla ya gemu uwanjani.
Tatu, chezeni mpira wa kujihamini na kushambulia. Msitegemee offside trick. Yanga iliwaponza kwa Zamalek. Simba iliwaponza kwa Wyadad. Hata Taifa Stars ilishawaponza Central Africa. Vunjeni offside tricks na chezeni soka. Mkabe na mshambulie na sio tu kushambulia bali pia kupachika mabao!
Mimi sio kocha ila hilo nimeliona mara nyini kama tatizo. Kwa mantiki hiyo, makocha wenye ujuzi watakuwa wakichekelea kwani wanaziona timu za TZ mtelemko.
Mdau safi sana kama Viongozi wengi kule SIMBA wana Akili kama ww OK. Ikijirudia basi SIMBA isirudi hapa bongo.
ReplyDeleteTatizo kwa wachezaji wa Tanzania ni kugeuka kuwa watazamaji wa 'mpira' unaenda wapi uwanjani badala ya kuwakaba kwa karibu wachezaji wa timu pinzani ili wasiweze 'kuutawala' uwanja kwa pasi rahisi kama mechi hii ya WAC (Wydad ya Maroc) dhini ya Simba May 2011.
ReplyDeleteUtaona kabisa ktk hii video mabeki wa Simba hawana habari kama nyuma yao au pembeni yao kuna mchezaji wa timu pinzani anasubiri pasi ya kirahisi kutokana na mfumo wa kufukuza 'mpira' wa timu za Tanzania.
Ni ajabu pamoja na wachezaji wa Tz kuangalia mechi nyingi za ligi za ulaya kupitia televisheni, lakini hawajifunzi kitu toka kwa timu zilizo ktk ligi kubwa kupitia televisheni.
Mdau
Kocha wa Mchangani Kigamboni
Kaseja Excellent!!!!
ReplyDelete