Rais wa Bendi FM Academy na mkali wa masauti Nyoshi  el Sadaat (wa pili shoto) amejiunga  rasmi kwenye Music Academy ili kutoa fursa ya kuwafundisha wanafunzi namna ya kuimba vizuri vilevile kuwapatia uzoefu. Nyoshi ataungana na  Komandoo Hamza  Kalala  (wa pili kulia) pamoja na Mandela kutoka Twanga katika mjumuisho wa pamoja wa kutoa mafunzo halisi ya muziki ili kuwanoa ipasavyo wana academia na hatimaye kuweza kufanikiwa kuibua vipaji vya muziki nchini Tanzania. Music Academy imejikita zaidi katika kutoa mafunzo na pia kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yataendela kufanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
Wana  Twanga Academy wakipewa somo kutoka kwa Nyoshi el Sadaat leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. NOCHA na wewe unaimba?

    ReplyDelete
  2. WAPE VIPANDE VYAO!

    Zaidi ya waujuavyo,

    Muziki ni zaidi ya Taaluma!

    ReplyDelete
  3. Usisahau kuwakumbushia kuhusu KULEWA NA MAFANIKIO!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...