Habari za leo wazalendo, natumai wote wazima wa hali. Kwa mara nyingi tena nawaletea hii ngoma mpya wa kijana wetu QChiller. Nasema kijana wetu sababu wengi wetu tunajua kapitia nini na anapitia nini sasa.
Nimechukua jukumu kama mdau wa mziki kukaa na kufanya kazi na Qchief, nimekaa nimesikiliza sana sana tu na kilichofata ni kwenda studio mimi nayeye na kutengeneza nyimbo hii. Kila siku Napata ngoma nyingi ambazo sana kiukweli ubora wa mashairi , sauti na ladha ya muziki sio nzuri basi tu ilimuradi mtu kaandika na kaimba.
Mtakapo isikiliza hii nyimbo ya KAOGE nadhani dhumuni letu kati ya mimi na Qchiller litakua limekamilika kwa asilimia 50, na asilimia hamsini iliyobaki ni kuifikisha nyimbo kwa watanzania. Mimi ni mmoja kati ya watu wanao umia sana sana kuwaona wasanii wakongwe wenye uwezo mkubwa sana wakipotea tu bila sababu ya msingi.
kwa maswali, comment tafadhali tembelea link hii hapa,
Shukrani kwa wote.
Adam M Juma
Producer / Director
Visual lab: Next Level
------------------------------ --
Visual lab: Next Level
------------------------------
mob: +255754074323
e-mail: mtupah@yahoo.com
e-mail: mtupah@yahoo.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...