Afisa mawasiliano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi. Dangio  Kaniki akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla ya kutangaza washindi wa  promosheni ya Mkali nani ambapo washindi wa siku hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kushoto ni Afisa Uhusiano  wa kampuni ya Airtel Bi. Jane Matinde akishuhudia  tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini Dar-es-Salaam.

Afisa Uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania Bi. Jane  Matinde  akitanzanga washindi wa  promosheni ya Mkali nani kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) ambapo washindi wa siku hujinyakulia kitita cha shilingi milioni moja na washindi wa wiki hujinyakulia kitita cha shilingi milioni tatu,kutoka kulia ni Afisa
mawasiliano wa kampuni ya Airtel Bi. Dangio Kaniki akishuhudia  tukio hilo lililofanyika makao makuu ya kampuni hiyo eneo la morocco jijini Dar-es-Salaam.

 Washindi 7 wa kila siku na mshindi wa wiki atangazwa 29, March 2012 Kampuni ya simu ya mkononi ya Airtel inayotoa huduma nafuu na yenye wigo mpana zaidi wa mawasiliano, leo imewatangaza washindi wa wiki hii ya promosheni ya nani Mkali pesa taslimu ambapo washindi wa kila siku watakabidhiwa shilingi milioni moja kila  mmoja na mshindi wa wiki ataondoka na shilingi milioni tatu. Washindi hao wamepatikana kutoka katika mikoa mbalimbali Tanzania ikiwepo Arusha, Zanzibar, Dar es Salaam, Nzega - Tabora na Manyara Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hizo Afisa uhusiano wa Airtel Dangio Kaniki alisema" Airtel inawapa nafasi nyingine watanzania
kushiriki na Kushinda fedha taslimu zaidi ya shilingi milioni 200,kwa washindi 110 watakaopatikana kila siku, kila wiki na kila mwezi katika promosheni yetu kabambe ya Nani Mkali.  Na leo napenda kuchukua fulsa
hii kuwatangaza washindi wa wiki hii ambao ni: 

KAANAEL LEMLE KANUYA (ARUSHA) 1,000,000.00, RAKESH MANSUR DEYAL (ZANZIBAR)           1,000,000.00, NAPEGWA DAVID MONGO (DSM) 1,000,000.00, MARIAM WAZIRI HAMISI (DSM)          1,000,000.00, GUVANTRAI SACHDEV SHANTILAL (ARUSHA) 1,000,000.00, YUSUPH NOHAI ANNAI (MANYARA)1,000,000.00, YUSUPH  MATHIAS MANONI (NZEGA-TABORA) 3,000,000.00

Tunaendelea kuwajali na kuwazawadia wateja wetu nchi nzima kuhakikisha washindi wengi wanapatikana, tunaendelea kuimarisha dhamira yetu ya kutoa huduma bora zenye viwango vya juu na kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru, aliongeza Dangio  kujiunga na "Nani Mkali", mteja anatakiwa kuandika neno "Mkali" na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. UNAJERUHI HISIA ZANGU ANKAL !

    Hiyo ni kauli ya malalamiko aliwahi kutoa Mdau humu baada ya kutundukwa Picha ya Msaa Linah aliyepo Marekani.

    Sasa leo Ankal ni zamu yangu 'umejeruhi hisia zangu' naomba Kontact ya DANGIO KANIKI,,,Tafadhali Ankal Michuzi niwezeshe !

    Mdau Heri

    e-mail:heribahati@aol.com

    ReplyDelete
  2. Ahhh jamani machoooo !

    Nipo tayari Dangio Kaniki anifilisi mali zooooteee !

    ReplyDelete
  3. Duh huyu mtoto wa Ki-Tanga(kisambaa) Dangio Kaniki naona kumekucha sio mchezo " Onga Dangio...imi niedi:-)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...