Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo, Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe, Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Saidi Meck Sadick muda mfupi kabla ya kuondoka hoteli ya White Sands Hotel alikofungua warsha ya siku mbili ya Utafiti.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua warsha ya siku mbili ya mikakati ya kiuchumi ya kuondoa umaskini iliyoandaliwa na REPOA katika hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango akitoa mada ya ufunguzi wa warsha hiyo ya siku mbili ya REPOA. Wengine toka shoto Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.
Profesa Do Duc Dinh toka Vietnam akitoa mada ya jinsi nchi yake ilivyofanikiwa kuondoa umaskini warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini nchini.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Katibu Mtendaji a Tume ya Mipango Dkt Phillip Mpango kwa mada nzuri. Kati yao ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa Samuel Wangwe na Balozi wa Uholanzi nchini Dkt Ad Koekkoek.
RaisDkt Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa kwa hotuba nzuri ya ufunguzi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa REPOA Profesa Esther Mwaikambo na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa REPOA Profesa .Samuel Wangwe .
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Profesa Ibrahim Lipumba baada ya picha ya pamoja na washiriki wa warsha ya siku mbili ya utafiti juu ya mageuzi ya kuondoa umaskini.Picha na Ikulu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa moja ya magonjwa makuu yanayowakumba Watanzania kwa sasa ni ugonjwa wa Kitanzania wa kulalamika, kunung’unika wakimlaumu kila mtu isipokuwa wao wenyewe.
Aidha, Rais Kikwete amesisitiza kuwa Serikali yake itahakikisha kuwa utajiri na manufaa yanayopatikana na yatakayopatikana kutokana na raslimali za madini na gesi asilia nchini yanamnufaisha kila Mtanzania.
Rais Kikwete pia ameahidi, kwa mara nyingine tena, kuwa Serikali yake itaendelea kuwekeza katika huduma za jamii kwa kuboresha huduma za elimu na afya, kuendeleza kilimo na kuinua hali ya uchumi wa vijijini kama njia ya kuwainua Watanzania wengi zaidi, na hasa wale masikini zaidi, kutoka kwenye umasikini.
Rais Kikwete ameyasema hayo, leo, Jumatano, Machi 28, 2012, wakati alipofungua Warsha ya 17 ya Utafiti ya Mwaka ya shirika lisilokuwa la kiserikali la Research on Poverty Alleviation (REPOA) inayofanyika kwa siku mbili kwenye Hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam.
Rais Kikwete amewaambia washiriki wa Warsha hiyo wanaotoka nchini na nje ya nchi, na hasa wale kutoka nje ya nchi kujitahidi sana kuepukana kuambukizwa ugonjwa wa Kitanzania wa kulalamika, kunung’unika na kulaumu wakati wanapojadili changamoto na njia bora zaidi na za haraka zaidi kupunguza ama kumaliza umasikini nchini.
“Nawaombeni nyote mlioko hapa leo kutumia nafasi ya Warsha ya Utafiti hii kwa kutathmini kwa kina kabisa changamoto zinazohujumu dhamira yetu ya kupata mageuzi ya haraka zaidi ya kiuchumi na kijamii“, amesema Rais Kikwete na kuongeza: “Mnaweza kufanya hivyo kwa kutumia ujuzi wenu wa nyuma ama kwa kutumia uzoefu wa nchi nyingine.
Tafadhalini sana epukeni na jizuieni sana kutokuambukizwa ugonjwa wa Kitanzania wa kulalamika na kulaumu wengine wote isipokuwa sisi wenyewe. Ni ugonjwa usiokuwa na tija.”
Kuhusu nafasi ya raslimali za madini na gesi asilia nyingi iliyogunduliwa nchini, Rais Kikwete amerudia tena ahadi yake ambayo ameitoa huko nyuma kuwa Serikali yake itahakikisha kuwa raslimali hizo zinawanufaisha Watanzania wote bila kubagua kwa sababu kila Mtanzania anayo haki ya kunufaika na raslimali za nchi yake.
Katika hotuba yake, Rais Kikwete ambaye amesisitiza mageuzi makubwa ya sera ambako sasa wajibu wa Serikali ni kufungua njia za uwezeshaji na sekta binafsi kufanya biashara tofauti na sera za zamani ambako Serikali ilikuwa inafanya hata biashara ya bucha za nyama na maduka ya sindano na viberiti amewaambia washiriki wa Warsha hiyo:
“Serikali kwa upande wake itaendelea kutekeleza mipango na sera ambazo zinamnufaisha kila mtu na zenye kuhudumia maslahi ya jamii zilizo masikini zaidi na zisizojiweza. Tutaendelea pia, kuwekeza zaidi katika huduma za jamii kwa kuinua kiwango na ubora wa elimu, huduma za afya, kuboresha kilimo na uchumi wa maeneo ya vijijini.”
Mwisho.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
28 Machi, 2012
Kwanza HATUJUI kwanini sisi ni maskini. Hivi tunatafutaje ufumbuzi? Tutaishia kutibu dalili badala ya ugonjwa
ReplyDeleteRaisi mwenyewe anatulalamikia kwamba sisi walalamishi sa unategemea nini???
ReplyDeleteUgonjwa kutibika inawezekana lakini ari ya kufuata dozi ndio tatizo.Dozi yenyewe inamhusu kila mtu tukianza na serikali yenyewe.Kama hatupo siriaz basi mambo yataendelea kama kawaida na kuongezeka zaidi umasikini.Serikali itoe muongozo mzuri na sisi tukubali kufuata muongozo huo.Watu wanaendekeza starehe kuliko kitu kingine kwahio umasikini utabaki palepale.Kila hatua mbili tatu utakuta duka la ulabu linafunguliwa na mapemaaaaaaaa.Sasa watu hawa watafanya kazi wakati gani??Halafu tunalalamika oooohhhhhhhh wahindi oooohhhhhhh warabu?????????Hawa jamaa hata kama anakunywa lakini anakunywa kwa mahesabu na huku anajisevia vijisenti vyake kuendeleza uchumi wake.Sisi tunapenda starehe tuuuuu na kuhonga kwenda mbele.Yaani mtu anahangaikia kutafuta mihela ya kutanulia sio atafuta mihela ya kujijenga kimaisha????????Na kwanini JK hamtumii LIPUMBA ktk uchumi?????????Mbona amesomea uchumi vizuri tu na anayo expiriensi ya kazi hii hata Uganda kaifanyia kazi?Tukiacha hizi siasa zetu tukaungana kuokoa jahazi basi tutafika tu why not??
ReplyDeleteHivi kweli umaskini wa watanzania unahitaji utafiti?angalia rushwa za viongozi wetu!angalia ufisadi,angalia kutowajibika kwa viongozi wetu na watendaji wake,angalia wizi na kutojali mali ya umma,angalia ubinafsi wa viongozi wetu,angalia hadhi ya shule zetu,angalia afya na tiba kwa hospitali zetu.MIMI NAONA WAAFRIKA TUMEROGWA KAMA KWELI HAYA MAMBO YANAHITAJI UTAFITI WAKATI YAPO NA HAKUNA HAJA YA KUTAFUTA MCHAWI.
ReplyDeleteAngalia walivyovaa, masuti toka Italia. Eti kuzungumzia umasiking, phewwwwwwwwwwwwwwwwwwwwww
ReplyDeleteUmasikini utatoka kama tutajenga utamaduni huu:
ReplyDelete1.Kuthamini mawazo baina yetu,
2.Kuwa waadilifu wa kufuata kanuni na taratibu zetu,
3.Kutoa Ushirikishwaji na kuaminiana,
4.Kuchaopa kazi na kujituma,
5.Kusimamia matekelezo, kupima utekelezaji na Kuwajibishana hasa yanapoharibika mambo.