Ile sherehe kabambe ya wanafunzi wote waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim miaka ya nyuma, imeahirishwa hadi Jumamosi ya Juni 30, 2012 katika ukumbi utakaotangazwa baadaye. Mabadiliko haya ni kuitikia maombi na kutoa nafasi kwa wenzetu wengi walio mikoani na nje ya nchi ili waweze kushiriki kikamilifu katika sherehe hii hiyo.
Lengo kuu la mkusanyiko huo ni kukutana, kufahamiana, kujua nani yuko wapi na anafanya nini ili hatimaye tuweze kuunda mtandao na kuendeleza mema yaliyopo.
Kamati maalum ya muda ya kuratibu mkusanyiko huo pamoja na kuangalia taratibu nyingine imeshaundwa. Vikao vya wadau vyenye kulenga kufahamiana, kuandikishana majina ya wanaopenda kushiriki na kupanga mikakati ya kufanikisha tukio hili, inafanyika kila Ijumaa kuanzia saa 11:00 hadi saa 1:00 jioni, katika ukumbi wa New Happy Hotel - juu ghorofani, iliyopo mtaa wa Ungoni na Kipande, jirani na zamani mgahawa wa Chef's Pride, maeneo ya Lumumba, Kariakoo hapa jijini Dar Es Salaam. Karibuni sana tukumbukane na tufahamieni zaidi.
Ukisikia au kusoma taarifa hii unaombwa uwaarifu na wengine.
Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na kamati ya muda kupitia:
Bi. Mambo Tambaza (0713236110) Mwenyekiti
Bw. Abou Liongo (0762298087) Mjumbe
Cast Vumi 0756 232821, 0713 232821(Mjumbe)
Abbas Mbonga 0767606970 (Mjumbe)
Barua pepe: kinondonireunion@gmail.com
USIKOSE NAFASI YA PEKEE YA KUKUMBUKANA NA KUFAHAMIANA
Wazo zuri mno na limetulia, jamani Juma Mkele (Magereza1) Fatuma Muya, Hoya (Nyau) wako wapi!!!!
ReplyDeletekaka umenikumbusha mbali sana siyo HOYA pekee jee MAKAKALA.displine master MR SHARIF WAKO WAPI?MAANA HUWEZI KUITAJA KINOSESCO BILA HAO WAHESHIMIWA
ReplyDeletekwa wale waliomaliza mwaka 1980 mtakao jariwa kufika msisahau kututumia picha za ukumbusho.Barry white
ReplyDeleteHello Jamani. Asantani sana kwa tafrija hiyo ya kukumbushana enzi ya 1978 I was a.student in those days Ms Usha. Mr Malik.Mr kambrudeen .Mrs Chaya I missed u all and thank you all for organizing the reunion. ..
ReplyDelete..Though I missed it but I pray for everybody from Kinondoni Muslim High Secondary school. My name is Hawa Yakub mail add malytz1@gmail.com
Miss mihogo maandazi maharage from mzee Shoka
ReplyDelete