SIMBA, TOTO AFRICANS ZAINGIZA MIL 50/-
Mechi namba 141 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Toto Africans iliyochezwa Machi 11 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 50,336,000.

Jumla ya watazamaji 13,851 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000 viti vya bluu na kijani, sh. 5,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 10,000 kwa VIP C na B wakati kwa VIP A ilikuwa sh. 15,000.

Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 7,678,372.88 kila timu ilipata sh. 9,758,228.14, uwanja sh. 3,252,742.71.

Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,301,097.08, TFF sh. 3,252,742.71, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,626,371.36, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 325,274.27 na asilimia 10 ya gharama za mechi ni sh. 3,252,742.71.

Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa kamishna na waamuzi sh. 160,000, tiketi sh. 2,100,000, maandalizi ya uwanja (pitch) sh. 400,000, umeme sh. 300,000, usafi na ulinzi kwa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (Beijing Construction) sh. 2,000,000.

Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata tena sh. 969,570 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kilipata tena sh. 831,060.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. pamoja na mchanganuo mhuo,kwanza twambieni matokeo ya mchezo huo. Si watu wote waneona mechi hiyo.

    ReplyDelete
  2. .....duh

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...