Dkt. N T. Jiwaji
Sayari mbili zinazong’aa vikali, Zuhura (Venus) na Sambula (Jupiter) zilizokuwa zikionekana angani tangu Novemba mwaka jana, sasa ziko jirani katika anga za Magharibi saa za jioni ya saa moja.  Sayari zote mbili zinang’aa mno ila Zuhura inang’aa zaidi.

Sayari hizo mbili zitaonekana jirani kabisa jioni ya Alhamisi Machi 15.  Sambula, iendayo polepole sana, itaipita Zuhura baada ya Jumamosi Machi 16 ambapo zitakuwa sawia.  Kuwa jirani angani ni muono wetu tu tunavyoziona.  Sayari zenyewe zimepishana angani kwa mamilioni ya kilomita.  Baada ya Machi 16 Sambula itaonekana chini ya Zuhura inavyooneshwa katika picha.

Hali hii ya kuwa jirani hutokea nadra sana.  Tukio la kusisimua kama hili halitatokea tena hadi July 2015 ambapo sayari hizi mbili zitakuwa jirani zaidi kwa mara tano ya zilivyo sasa hivi.

Jioni ya tarehe 25 na 26 Machi, Mwezi hilali mwembamba utaunganika na sayari hizi mbili na kutoa mandhari ya kuvutia mno katika anga za jioni. 

Kati ya sayari nane (siyo tisa!) katika Mfumo wetu wa Jua, sita kati yao huonekana kwa macho bila kutumia darubini.  Kwa wakati huu sisi tunaweza kuona sayari tano kwa wakati mmoja.  Ukiangalia angani baada ya saa mbili usiku, Zuhura na Sambula zina tua katika upeo wa Magharibi.  Wakati huo, sayari ya Mirihi (Mars) inang’aa kwa rangi nyekundu kali upande wa Mashariki.  Wakati huo huo, sayari ya Zohali (Saturn) inaanza kuchomoza kwenye upeo wa Mashariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Ahsante Mnajimu Dr. N.T Jiwaji,

    Hivi unapoandika ''Kati ya sayari nane (siyo tisa!) ,katika mfumo wetu wa jua'',,,,una maana gani wakati nakumbuka Shuleni nilisoma Jiografia nikielimishwa kuwa Mfumo wa Sayari zipo tisa?

    ReplyDelete
  2. MH KAKA SALAMA SAANA ILA HII HALI INAWEZA IKAWANA MADHARA YOYOTE KWA WENYE NYOTA HIZO AU INA FAIDA

    ReplyDelete
  3. Ni vijimapambo vya mandhali au kuna faida/hasara zinazoambatana na matukio hayo?

    ReplyDelete
  4. Wadau Anonymous wa Wed Mar 14, 09:01:00 AM 2012 na Anonymous wa Wed Mar 14, 03:10:00 PM 2012.

    Msichukulie Uchambuzi huu wa Dr. N.T.Jiwaji kwa MISINGI YA KUTAZAMIA AU 'RAMLI' yeye Mtaalamu sio Mganga wa kienyeji kama wengi wanavyoainisha matokeo ya Sayansi hii na Masuala ya Ushirikina,,,huu ni ''UNAJIMU NA SIO UGANGA''

    ReplyDelete
  5. Wadau wa pili na wa tatu hapo juu , msiingie ktk upande wa Pili wa Sayansi tafadhali!

    ReplyDelete
  6. Kwa mdau aliyecomment kwanza ni kweli mfumo wa jua una sayari nane baada ya wanasayansi mwaka 2009 kugundua kuwa pluto si sayari. Hivyo yuko sahihi pia ni vema tukawa na mazoea ya kujisomea somea mambo mengi ya kidunia yanabadirika kila siku

    ReplyDelete
  7. Katika mwaka 2006, Umoja wa Kimataifa wa Astronomia (IAU) iliamuwa kwamba Pluto ni ndogo mno kuweza kutambulika kama sayari. Kwa hiyo zimebaki sayari nane tu ambazo zina ukubwa wa kutosha, na zina umbo la tufe kamili, na zina mvuto wa kutosha wa "gravity" wa kuweza kuvuta maada yote kakita mzingo wake wa kuizunguka Jua. Pluto sasa inaitwa sayari-kibeti. Dr N T Jiwaji

    ReplyDelete
  8. Hali hii ya kukaribiana angani haina madhara yoyote kwa vile katika anga za juu, sayari zenyewe zina baki kuwa na umbali mkubwa kati yao, na ni mamilioni ya kilometa kutoka kwetu. Dr N T Jiwaji

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...