Hapa ni Kituo cha Daladala Buguruni Sokoni ambapo kuna sehemu nzuri tu ya kuegesha magari haya.lakini kutokana na kutotii sheria ya usalama barabarani,dereva wa gari hii kasimama upande wa barabarani kabisa na upande wa pili wa barabara hii kuna kituo kikubwa cha polisi lakini bado madereva hawa wa daladala hata hawaogopi.
Hapa ni Tabara Matunbi ambapo uzembe wa kusimama na kushusha abiria barabarani unaendelezwa.sasa sijui ni juhudi gani na ni sheria gani za kiusalama barabarani zinapaswa kuchukuliwa ili kulitokomeza kabisa tatizo hili.
Sheria ni kuover take na kuchapa mguu watu tumeshajichokea na sheria za tz zisizona manufaa sioni umuhimu wa sheria na wanasheria
ReplyDeleteKWA TZ KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI TUMEFAIL KABISA...SHAME ON US!
ReplyDeleteAogope nini wakati hao na wao ni damdam.
ReplyDeleteHii ndio sababu kubwa ya foleni Dar pamoja ni miji mingine Bongo.
ReplyDeleteMadereva wa daladala ni wazembe wa kutupa, wanasimama ovyo mno.
Sehemu zenye kichefuchefu Dar ni pamoja na buguruni, ilala sharifu shamba, ilala Amana, Ilala sokoni, msimbazi na kariakoo.
niungane na anon aliyetangulia kwakweli hali ni mbaya kwenye vituo vya mabasi sheria azifuatwi ukifika Ubungo kwenye mataa kituo cha pale ni kichefuchefu.Huwa najiuliza serikali iko wapi hao wasimamizi wa vituo wako wapi inasikitisha sana sielewi tuendako.
ReplyDeleteSasa jamani akasimamishe wapi, wakati abiria ndio wateja wake? Tatizo kubwa kwetu ni UVIVU wa hata kufikiri, haya yanaweza kupungua au kuisha kama kila mmoja wetu atatimiza wajibu wake. Abiria tutumie vituo vilivyopo kwa ufasaha nina hakika hao madereva wa daladala watafuata sheria.
ReplyDelete