Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Siyo 'Solo' mdau ni 'Sorro' na manyamanyama

    ReplyDelete
  2. hakuna lolote..Uswahili mtupu!

    ReplyDelete
  3. HIYO HARUSI YA MICHUZI ILIFANYIKA LINI? NAONA BWANA HARUSI ANACHAGUA NYAMA KAMA VILE NGUO. MBONA WANAFUNIKWA?

    ReplyDelete
  4. Hizi desturi zimepitwa na wakati kwa sasa. Inabidilike kwa kweli.

    ReplyDelete
  5. Uswahili mtupu sisi si waswahili lazima tudumishe mila kaa na uzungu wako

    ReplyDelete
  6. kwani aliyekwambia hao wazungu nani we mdau wa pili hapo juu mijitu mingine kwa kujiona mizungu kumbe pumba tupu heshimu tamaduni ya mtu wewe sio unapelekwa kama ling'ombe

    ReplyDelete
  7. jamaa wakisema uswahili wanamaanisha uislamu.

    ReplyDelete
  8. Hayo manyamanyama nasikia hua yanahifadhiwa sehemu nyeti na bibi harusi kabla ya siku ya tukio. Jamani , dunia imebadilika magonjwa mengi tubadilike. Ankal Mithupi, tafadhali tafadhali na hayo manyamanyama!!! Ukienda nani atatuhabarisha?

    ReplyDelete
  9. bwana harusi mbona anatia chakula kama anafukuzwa?

    ReplyDelete
  10. Nyie wote waongo.
    Nani kawaambia huu ni utamaduni wa kiswahili??
    Hizi mila za kiarabu na siku zote mnafikiri ni zenu.
    Acheni ujinga, mmeshapoteza utu na utamaduni wenu, kaeni chini kufikiri upya. Acheni Uarabu fateni zenu.

    ReplyDelete
  11. Wewe mdau unaesema ni utamaduni wa mwarabu nikuulize ni mwarabu gani uliemuona anafanya mambo hayo?

    Hayo mambo yangekuwa ya kuvaa suti na kugongesha glas basi hii mitwana ya kitumwa isingesema kitu
    mtabakia kuwa watumwa mpaka mwisho wa dunia
    jambo likifanywa kizungu ndio mnaliona kuwa lakwenu shame on u

    ndio maana mpaka kesho mnaamini wanachofanya wazungu ndio cha kuigwa mshaanza kutembea uchi mbele ya babazenu eti ni uzungu ama kweli nyie ni kama mandondocha mnatembezwa kwa control au bendera mnafata upepo hamjui njia yenu.

    ReplyDelete
  12. Hapa bwana harusi anamuwekea chakua mke wake kuonesha mapezi kwa kila kizuri achokipenda bwana basi ampendelee mke wake.

    Manyamanyama kuhifadhiwa sehemu nyeti na bibi harusi kabla ya siku ya tukio ni uzushi wa kusikia huo.

    Acheni kusituzi mila za waswahili nanyi mnazo zenu na kama hamuna basi poleni.

    Natumai mmepata somo.

    ReplyDelete
  13. jamani nyama inawekwa sehemu nyeti ya bibi harusi?????????????????acheni kututukana akina mama,kwani hiyo nyeti ina fridge na ni kubwa kiasi gani kuhifadhi nyama yote hiyo??????????acheni hizo kuleni kwa raha zenu

    ReplyDelete
  14. Wewe mdau wa pili nyinyi munaojivalisha maveli meupe mumeyapata kutoka vijijini kwenu? Afadhali ya huo uswahili kuliko kujivisha manguo ambayo eti ya kuiga uzunguni na huku mukaongezea na vya kuiga vya 'kwaito' sasa.

    Na kitu kidogo eti mwarabu, kwani watu wa pwani wenyewe hawakuwa na ustaarabu wao tangu enzi?

    Na hiyo ya kuweka nyama kwenye nyeti hebu wacheni ujinga mumeona wapi mambo hayo? Au ndiyo munataka kuwazushia tu hao waswahili?

    Arrrrrrrrrrrrrrrggh!

    ReplyDelete
  15. Hivi huyu mdau anaesema ni mila za waarabu unatoa wapi? ni waarabu wa nchi gani wanafanya hivyo? hivi unataka useme kabla ya waarabu kuja pwani, watu walikua hawana mila? acha kufuata mambo ya wazungu wewe.Kuvaa suti na veli siku hizi umekua utamuduni wa waislam na wakristo, je hizo ni mila zetu? Kila wanachofanya na kusema wazungu ni sawa kwasababu unaona kwenye TV.Na wao ndio, wana control TV.Wakileta movie kwenye TV za amerika wana sensor( wanaondoa sehemu chafu)katika public TVs, lakini kwetu tunaona kila kitu.In america, mtu haruhusiwi kutembea na pombe barabarani ikiwa wazi, ni mpaka aifunike. Unajua kwa nini? Acha hizo,wanasema ni mzungu ndio amegundua mlima kilimanjaro. Sasa sijui wakati yeye anagundua kulikua hamna watu wanaishi hapo. Vilevile ningependa kuongezea, nilisoma Moshi High school. Nilishangaa wao wakisema waswahili wanamaana waislam. Na mimi nilikua nafikiria waswahili ni watu kutoka pwani. Najua mdau hapo juu, u nailed it. Ni kweli alichosema, na umenichekesha.

    ReplyDelete
  16. Huyo Mswahili ana Utamaduni wake ,na huyo asiye Mswahili ana Utamaduni wake.

    1.Kwa mtu Mstaarabu huheshimu Imani, Mila na Jadi za watu wengine.

    2.Iwe MZUNGU, Iwe MWARABU, Iwe MSWAHILI, Iwe MWAFRIKA,,,Kila Jamii ina Tamaduni,Mila na Jadi zake,,,,Pia hatuwezi kubisha zipo Mila potofu na mila endelevu ktk Jamii zetu.

    TUHESHIMIANE, TUCHUKUE KILICHO NA MANUFAA TUACHE KISICHOFAA NA KILOCHO POTOFU!

    ReplyDelete
  17. Mswahili ni mtu anayetoka (Maili kumi toka baharini kwenda bara)pwani ya afrika mashariki ukianzia lamu hadi mtwara, ila hapa naona watu wanachanganya mada, mswahili si lazima awe muislamu.watu wasichanganye dini na mila.mtu wa mwanza huwezi kumwita mswahili eti kwa kuwa anaongea kiswahili cha bara.
    Ankal haya ndio mambo yetu sisi wazee wa pwani.

    ReplyDelete
  18. USTA-ARAB (Ustaarabu) = Utu bora kufuatana na mila na desturi za waarabu!? Au ndio nimewachanganya kabisa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...