Kumekua na tabia Fulani kwa mtu akifanyiwa jambo ambalo hakulipenda, au akiona mtu anafanya jambo ambalo yeye binafsi halipendi,hupenda kusema “haa huyu anafanya mambo ya Kiswahili”, “waswahili hao”, ‘acha uswahili” n.k

Ankal niwekee hii wadau wanipe maoni ya juu ya
1. Mswahili ni nani?

2. Mambo yepi ni ya Kiswahili na yepi si ya Kiswahili, kama si ya Kiswahili ni ya wapi hayo?

3. Huyu anatoka uswahilini, ni wapi huko uswahilini?

Ahsante ankal
Mbegu-Kigambono

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Baadhi ya maneno huenda na wakati, sehemu na hali fulani ya utani. Uswahili katika baadhi ya sehemu humaanisha ujanja ujanja, uwongo wa kiana au sehemu ambayo kuna vituko vya kiana aina aina.

    ReplyDelete
  2. Bro Mbegu.
    Mimi sio msomi,wala mjuzi,lakini hilo swali lako naweza kupambana nalo kwa upeo wangu.
    Baada ya kuchunguza kivyangu kasumba nyingi tulizowachiwa na wakoloni wa Kizungu na wa Kiarabuhiyo ni moja ambayo mpaka sasa Waafrika tunaendela nayo.Ukiwa
    mtu mzuri, mpole watu wanakukubali unaambiwa wewe ni Msta-arabu.
    Nimekutenganishia hapo uone bro,na ukiwa hukubaliki umefanya jambo silo wewe ni Mswahili.Ni kasumba ambayo ishaota mizizi kwenye jamii yetu na kundoka sio rahisi,watanzania wenye asili zote wanatumia neno hilo,mimi nishalifuta kwenye kamusi yangu.
    Mungui akubariki Bro

    ReplyDelete
  3. Angalia kipindi cha USWAZI utapata majibu yako yote. USWAZI ni synonym ya USWAHILI. Mambo yote yafanyikayo uswzi ni ya kiswahili. Sasa pia unaweza kukuta mtu anakaa uzunguni lakini anatabia zote za kiswazi, hii ni kwasababu alizaliwa huko na kulelewa huko. Bahati nzuri kapendwa na kuolewa na mtu mwenye maaendeleo na kuja kukaa naye kwenye ustaarabu, yeye anashindwa. Atataka kusugulia mcgnga masufuria ingawa ndani ana steel wire! Umenipata!!!

    ReplyDelete
  4. Swahili:- neno lenye asili ya kiarabu linalomaanisha mwambao wa pwani.
    Hivyo Waswahili itakua ni watu wa makabila tofauti wa mwambao huo. Hivyo Waarabu walipofika mwambao hasa wa Afrika Mashariki, walikuta watu wanaozungumza lugha za makabila yao. Maneno ya lugha hizo( za Kibantu) pamoja na maneno ya Kiarabu zikazaa lugha ya Kiswahili.
    Hiyo ndio fact.

    Sasa kuna tafsiri ya mtazamo wa watu. Ki historia watu wa kutoka bara walikuja pwani na kufanya kazi za nguvu, kama kwenye mashamba (ya mkonge) etc. Watu wa pwani...... Waswahili hawakujishughulisha na kazi za sulubu. Hence equating Waswahili na tabia tabia za uvivu, kuzungumza lugha hiyo kwa ufasaha na kuweka maneno matamu ndani yake, na pia kuishi katika mazingira ya umaridadi na kujipenda.
    Ikawa mtu mwenye mwenendo wa tabia hizi, kiutani ataitwa Mswahili.
    Halkadhalika watu wa pwani ( Waswahili) walikuwa na utani wa jadi na watu wa bara hasa Wanyamwezi na Wasukuma kwa kuwaona wao ni vibarua na watenda kazi ngumu kwao. Watu wa pwani walikuwa wakiwaita watu wote wa bara Wanyamwezi, regardless of whether they were or not.

    Nadhani mdau utapata ka-historia kafupi cha swali lako.

    ReplyDelete
  5. Kwa sisi watu wa Bara, mswahili ni mtu wa Pwani na mambo ya kiswahili ni mambo ambayo hayaendani na tabia au desturi za sisi watu wa bara.

    ReplyDelete
  6. TANZANIA SEHEMU ZA SWAHILI LAND NI MIKOA YA PWANI TANGA,DAR,KILWA,BAGAMOYO, NA SEHEMU ZENGINE ZA PWANI NDIO SWAHILI LANDA NA WASWAHILI KABLA WATU KUJA KUJAZANA MIKOA YA PWANI WALIKUWA WATU WA KIMYA WASTAARABU NA NENO WASWAHILI LILIKUWA SAFI HAPO MIAKA YA NYUMA WATU WAMELIHARIBU SANA NENI WASWAHILI. MTANGA HALISI JAMES.

    KAMA ENGLAND KUWA WA ENGLISH AMBAO BRITISH. ZAMANI WA ENGLISH WALIONEKANA WATu WASTAARABU SIKU HIZI WANAONEKANA WALEVI MAMBO KAMA HAYO.

    ReplyDelete
  7. WATU WENGI WAMEHARIBU MAANA YA KISWAHILI NA WASWAHILI NA SIFA ZA USWAHILI IMEHAIBIKA IMEKUWA KAMA KULE MAREKANI KUSEMA JAMAA KATOKA HOOD, TUNAZARAU YETU KWA KUWEKA MAANA MBAYA NA NDOMANA YANAKUWA MABAYA MUNGU ANATULAANI HAPAHAPA TUWE TUNAWEKA MAANA NZURI NA KUWEKA SIFA AMBAZO WALIZOKUWA NAZO WATU WA KISWAHILI. KULWA

    ReplyDelete
  8. Konyagi 7 timesMarch 26, 2012

    Mambo ya kiswahili ni hili swali lako, mswahili ni kama mimi na acha uswahili ni aliyeuliza swali.

    ReplyDelete
  9. Midladjy MaezMarch 26, 2012

    Wakati fulani katika kuenzi Uswahili nilitaka kujitangaza Chifu wa Waswahili nikafikiria tuanzishe Dini yetu pia maana hizi dinizote zina chimbuko lake ...kama unabisha uliza utaambiwa ..ttungechaghua tu wapi tungeweka mahali rasmi pa kutambika Waswahili. Juzi mwanafunzi mmoja wa Sekondari mjini Nairobi akihojiwa katika KBC kwanini Wanafunzi wa Kenya wanakidharau Kiswahili ( wanafanya vibaya katika mtihani wa Taifa) akajibu wanasema 'Kiswahili ' ni lugha ya kimasikini! Hapa ndipo mambo yote yanapoaanza ..Hata hapa Wabongo wanahangaika kuwapeleka shule zinazofundisha kila somo kwa lugha ya kiingereza hata kiswahili chenyewe kule kinafundishwa kwa 'kiingereza' Teheehehee..Wasema kwa kiingereza ukitaka kumua mbwa mmpe jina baya kwa maana msingizie chochote kitakachoaamsha hasira za watu halafu inakuwa kwako ni rahisi kumuadhibu hata ikiwa ni kifo..! Mimi sijatembea duniani sana lakini kule Usovieti USSR wakati huo) sasa Urusi wawo pia kuna Mataifa walikuwa wanayadharau mathalani Wapoland walikuwa wanawajua ni Mtapeli kutokana na kufanya baishara ya uchuuzi wananunua vitu kwa bei rahisi Usovieti wanakwenda kuuza Berlin kule wananunua bidhaa za magharibi wanarudi kuziuza Poland na Usovieti kwa bei kubwa nk..nk..Walistahikli kuitwa Walanguzi ..! Kama vile Warusi wenyewe Ulaya Magharibi walikuwa wanawachukulia sio wazungu waliostaarabika.. ( Washenzi tu) Dharau dharau ..sio ajabu Waarabu na Warusi wananunua timu za mipira kule UK sio kwa upenzi peke yake na ukwasi walio nao bali kuonyesha na wao ni watu katika watu..! Waswahili tunajidharau wenyewe siku tutakapoacha kujidharau ndio hivi vijisifa ambavyo vinapatikana kwa jamii zote duniani zitaachwa na kubakia utani..Uswahili ni ujanja ujanja na kutumia lugha ya kimafumbo kwa nia ya kumshughulikia mtu labda bahili au 'mzikaji'..! Kwa mfano kule Ulaya ukimuita Muingereza weye Mrusi nini ina maana mzungu asiyeendelea sio mstaarabu mtu wa mitulinga.. nk..nk..Hata leo Mrusi mbele ya Waingereza wanamuona Abramovich katika hisia hizo ....! Sio ajabu kwa hapa kwetu turudi enzi zile za Ubwana na Utwana kwa maana ya sasa Mswahili hawezi kuwa Muungwana yaani Bwana..! Sasa kama nilivyosema hapo awali hii dhana iliyojengeka dahari na dahari haitofutika kwa Sala wala Maombi bali kwa vitendo vya kiungwana kokote pale walipo Waswahili iwe Afrika au mabara mengine ! Sio ajabu Wanigeria hawajui kiswahili lakini kwa watu wengine wanaitwa 'Waswahili' ( Waafrika)..! Tukubali hiyo picha hasi ipo imejikita kila mahali natuazimiye kuibadilisha ndio utatuzi wa suala la Uswahili kuhusishwa na mambo hasi kitabia na vitendo vyetu..! Meneja anaweza kuwa Mswahili, Waziri anaweza kuwa Mswahili na ata Mmachinga anaweza kuwa Mswahili vilevile kulingana na mhanga husika..! Ije siku tutakuwa muda wa kiungwana na sio 'British time' ..au Yule Bwana ni Mzungu au ni Britsh kwa vile anatimiza ahadi zake..! Tuazimie kubadili kwa vitendo muonekano hasi wa sisi Waswahili..! Tusijinyanyapae ..na hatua tya kwanza kukuenzi Kiswahili na kuitosa dhana kuwa Kiswahili ni lugha ya kimasikini..!

    ReplyDelete
  10. Naona wengi wameeleza kwa kirefu. Nadhani neno hilo kwa kiswahili lingekuwa na maana ya watu wa pwani. Kuna mdau nae hapo juu ameelezea ni kutokana na ukoloni ndio maana tumekua na tabia ya kujifananisha na mabwana.mfano mbwa wa kizungu akiwa mkubwa.Mbwa wa kiswahili kwa sababu hana afya na ni dhaifu.inategemea na sehemu, mfano eneo la pwani bado neno la uswahili linatumika kama hivyo hapo juu nilivyoandika.Bali kuna sehemu nyingi bara, wana maana ya uislamu.mfano nimesoma moshi, nilikua na rafiki yangu ambaye ni kutoka mkoa huo.siku moja akaniambia tukaenda kiboroloni(eneo la moshi) akaniambia wale jamaa pale ni waswahili lakini wanakula nguruwe.nikawa sikuelewa, nikumuuliza wamehamia kutoka pwani? akasema hapana ni wachaga.lakini wana majina yenu na ni waswahili kama wewe.sasa nilipokaa sana ndio nikajua kule mtu yeyote kutoka bara akiwa muislam wanamwita mswahili.nikaelewa neno linatumika kutokana na sehemu.Kwa hiyo NDUGU MBEGU. maana ya neno hilo inategemea na sehemu.La pili, mambo ya kiswahili ni mambo ya kutotaka maendeleo.la tatu, uswahilini ni kule ambako nyumba zetu unapita uani kutokea kwa jirani yako.Uzunguni ni mageti.mdau usa.

    ReplyDelete
  11. Maana ya waswahili nakubaliana na wengi ilikuwa nzuri na ni watu wa pwani ila mjazano wawatu natabia kuchanganyika waliotoka mabara huko ndio wakawafanya waswahili sasa kuonekana na tabia mbaya nakuonekana Waswahili wanatabia mbaya ila kumbe watanzania tumeiharibu uzuri wa waswahili. Pia ukichunguza Pwani walikuwa Waswahili na sehemu za waswahili safi sana na nyumba zilijipanga safi wanatumia seheumu za kazi vizuri. Mfano sisemu watu vibaya CHUO CHA MLIMANI WANAKUJA WATU MIKOANI HAWAJUI KUTUMIA VYOO VYA KUFLASH BASI WANAHARIBU KWELI Inataka ELimu mwisho utampa mtu FLAT atapanda juu na KUNI. ELimu na maana ya Waswahili inaharibiwa.

    ReplyDelete
  12. Iwe wewe ni Mzungu iwe ni Mwafrika , iwe wewe ni wa rangi ya Buluu kama utafanya mambo kienyeji utaitwa 'Mswahili'.

    Ina maana 'Uswahili' ni kufanya mambo bila mpangilio,,,lakini sio maana yeke kuwa kila Mswahili ndiye afanyaye mambo bila mpangilio, hii imetumika kwa maelezo ya 'Kubeza tu, mafano unaweza sikia 'sisi wakonongo' huwa tuanachukulia hivi na hivi n.k

    Ila kwa watu wenye nia mbaya huifanya hii kuwa utwezaji dhidi ya kundi fulani hata kama naye mwenyewe muhusika ni miongoni mwao.

    ReplyDelete
  13. STORY ZIMEKUWA NYINGI.
    MKUBALI AU MKATAE,HILO NENO LIMELETWA NA WAKOLONI KUWADHALILISHA WAAFRIKA WEUSI NA KUWAPA MOYO WALIOKARIBU NAO NA WALIOCHANGANYA,TAFUTENI CHIMBUKO LA NENO USTA-ARABU MTAJUWA.
    NA MBEGU HAJAULIZA NI VIPI? AMEULIZA KWA NINI? NDIPO NILPOMFAFANULIYA KUWA UKIWA MTU MZURI WEWE NI MSTA-ARABU UKIWA MTU MBAYA NI MSWAHILI,HAYA YA UBARA NA UPWANI,UVIVU NA UTWANA YAMEKUJA BAADAE. AAMKANE BASI LINAONDOKA HILO.

    ReplyDelete
  14. Mjumbe mmoja kati ya waliotangulia kuchangia ameongea vizuri.
    Unajua kuna jinsi kadhaa za kulidadavua jambo hili.
    -Katika sanaa(elimu) ya lugha, Neno lolote katika lugha yoyote likitumika linaweza kuwa na maana zaidi ya moja kulingana na mazingira au muktadha husika.Neno huweza kutumioka kwa maana halisi(Conceptual meaning) au maana zilizozoeleka au za kuchukuliwa(conotative meaning)Mathalani mtu akisema fulani kapata mtoto, kwa maana halisi unaweza kusema -kazaa, lakini conotatively neno hili linaweza kumaanisha mtu kupata mpenzi. Tukirudi kwenye maana ya msingi ukisema Waswahili unamaanisha watu wanaozungumza lugha ya kiswahili, wanaokimiliki kiswahili kama vile tukisema Kichina tukimaanisha wachina.Utaona siku hizi ukimwambia mtu kifaa hiki ni cha kichina watu wengi kwa haraka watachukulia maana za mazoea kwamba ni kifaa cha kubumba ambayo ni (konotative meaning)badala ya conceptual meaning ya kuwa kimetengenezwa Uchina.
    Katika hoja ya msingi, mtoa mada aliuliza mswahili ni nani na asiyekuwa mswahili ni nani. Muktadha alioutaja inaonesha ni maana zilizozoeleka(au maana iliyopanuliwa) yaani (conotative meaning). Katika lugha isiyokuwa rasmi waswahili humaanisha watu wenye uwezo au maisha ya chini, mfano chukulia manzese. Wamezoea kusema mtu anaenda kuoga kabla ya kulala bafu liko nje, anatoka bafuni hata bila ndala mguuni kisha anaenda kulala hivyohiyo. Nyumba mbili tatu zinachangia bafu na choo. Wanachangia jiko wanaibiana mboga jikoni. Hawa ndo huitwa waswahili katika maana zilizozoeleka. Inavyoonekana hapa mtoa mada ameongelea katika maana halisi na aliyemkwaza alikuwa katika conotative meaning.

    ReplyDelete
  15. nimeangalia mawazo ya watu wengi hapa sijapata hata maana ya moja kwanza kabisa swahili ni neno la kiarabu lina maana ya mtu wa pwani,watu wa pwani ni waislamna kutokana na uislamu wao wamekuwa ni watu wapole na wanyenyekevu kwa makabila mengine ni wastaharabu sana na kutokana na ustaarabu wao ndio imeonekana kama ni watu waliopitwa na wakati,hawana elimu ,na wajinga wakati watu wa pwani ndo watu wa kwanza kupigania uhuru chini ya chama cha TAA na wakati huo abdulahamani skykes alikuwa kama finacier wa chama hicho huku akiwa anafanya kazi kama chief accountant kwenye shirika la reli miaka ya 1950,watu hawajui kwamba amani ya nchi yetu imetokana na watu wa pwani,sijui ingekuaje kama jiji la Dar lingekuwa la wahaya au wachaga kwani hao ndio watu wa kwanza wanawazalau watu wa pwani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...