Kwa niaba ya Shirikisho la michezo la vyuo Vikuu Tanzania(Tanzania University Sports Association)
Nawataarifu kuwa tulipokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya msiba wa Kiongozi mwenzetu wa TUSA, Mpendwa wetu Ndg. Andrea Lesso Hange ambaye hadi kifo chake alikuwa Katibu Mkuu Msaidizi wa TUSA na Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kifo chake Kilitokea tarehe 02/03/2012 huko Swedeni alikokuwa masomoni. Taarifa tulizonazo ni kuwa mwili wake ulikutwa chumbani kwake.
Uchunguzi wa kifo chake bado unaendelea. Taarifa tulizo nazo kama chama ni kuwa mwili utawasili hapa nchini tarehe 20/03/12 na unatarajiwa kuzikwa tarehe 21/03/12 Kwa hivi sasa Msiba upo nyumbani kwake Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Karibu na Hall One.
Tunawaomba wanachama wote wa TUSA, wanafunzi wote waliosoma Elimu kwa michezo nyakati tofauti pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wanamichezo wote na watanzania kwa ujumla tukutane wote kwa pamoja tarehe 19/03/12 ili kufanikisha shughuli hii.
Watu wote tushirikiane katika kipindi hiki kigumu kwani mwili umesubiriwa kwa muda mrefu na gharama zimekuwa kubwa. Pia unaombwa kutembelea Blog ya TUSA (http://tusadailyblog.blogspot.com/) kwa kupata taarifa nyinginezo kuhusu msiba huu.
Asante Sana kwa Ushiriakiano Wenu
NOEL KIUNSI
KATIBU MKUU TUSA
Nasikitika kusoma taarifa hii ya msiba wa kaka yetu ambye amekutwa akiwa amekufa chumbani kwake Sweden.
ReplyDeleteNawapa pole sana familia yake na wan michezo wote
Mungu atafanikisha mipango ya kurejeshwa kwa mwili wake nyumbani Bongo -Tanzania
RIP Mwalimu Hange. Alikuwa mwalimu mzuri wa Kiswahili pale Siha Secondary.
ReplyDeleteRIP Mwalimu Hange.
ReplyDeleteKumbe amekufa chumbani kwake!. Jamani tunapoenda nje tukumbuke ku beba madawa kama ya Malaria ama ugonjwa mwingine unaokusumbua(Silaumu ila nachangia kutokana na uzoefu ). Kuna wakati nilienda japani basi siku moja nilijisikia vibaya sana jioni, Lugha yao haipandi nikawa chumbani. Nikaja kuokolewa na jamaa toka Ethiopia aliyeniletea dawa alizokuja nazo toka kwao.
ReplyDeleteObserver
Ninamkumbuka Marehemu toka wakati tunasoma pamoja chuo kikuu mlimani. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
ReplyDelete