Ubalozi wa Tanzania Nchini Ufaransa ukishirikiana na Chama cha Watanzania Ufaransa (CCWU) wanaandaa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kwa lengo la kuitangaza Tanzania, utamaduni wake na fursa za utalii na uwekezaji. 

Sherehe hizo zitaadhimishwa Jumanne tarehe 22 na Ijumaa 25 Mei 2012 mjini Paris. Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo:
  • Maonyesho (exposition) ya vifaa vya utamaduni, picha, michoro na bidhaa za kitanzania k.m. chai, kahawa, korosho, katani, n.k.
                        Mkutano (conference) kutangaza fursa za utalii na uwekezaji Tanzania. Makampuni na wafanyabiashara zaidi ya 150 kushiriki.
                        Chakula cha jioni (Gala Dinner) Jumatano Mei 23, 2012, chakula, burudani na mavazi ya wanamitindo wa kitanzania na ngoma za asili.

Maonyesho na Mkutano bure

Kiingilio kwa Watanzania: Gala Dinner: €50 (kwa watakaojiandikisha na kulipia kabla ya 31 Machi 2012) na €70 watakaojiandikisha kuanzia Aprili 1 hadi Aprili 30, 2012). Mwisho wa kujiandikisha na kulipia ni tarehe 30 April 2012.

Tumia maelezo yafuatayo kufanya malipo kwenye akaunti ya benki:


EMBASSY OF TANZANIA – PARIS
BANK DETAILS
Bank code
Agency
Account no.
RIB key
3078
00001
1049296003
77

IBAN

FR76 3047 8000 01010492 9600 377

BIC
MONTFRPPXXX

ACOUNT NAME
EMBASSY OF TANZANIA – SPECIAL ACCOUNT



Watanzania waishio Ufaransa na nje ya Ufaransa wanakaribishwa!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. 100% confidence levelMarch 17, 2012

    Mara zote tunapokuwa tunatumia rangi Nyekundu linapokuja suala la mawasiliano verbal and non verbal,tunamaanisha hali ya hatari,mfano msiba,ajali,mauaji,vita,magonjwa nk.Mwandishi wetu hiyo dhana hakuizingatia katika uwasilishaji wa ujumbe wake katika jamii.

    ReplyDelete
  2. mnasema lengo ni kutangaza nchi halafu mnaweka kiingilio??? Tna uero 50???
    kwanini msiwe wazi tu kwamba ni kama dili flani tu?
    Be serious guys!!!

    ReplyDelete
  3. Mdau Anonymous wa Sat Mar 17, 10:58:00 AM 2012

    Rangi ya Taarifa ni 'nyekundu' kumaanisha Hatari ,Dharura kwa vile sherehe imechelewa saaana miezi 6 mbele Sherehe ni ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania maadhimisho yalistahili yawe tarehe 9 Disemba 2011 sasa yanafanyika nje ya muda tarehe 22-25 Mei, 2012 !

    ReplyDelete
  4. Huu ndio Ubize wa Majuu?

    Hivi hadi Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania Ufaransa nao wanabeba Ma box?,,,inaonyesha wapo bizy sana na masuala yao binafsi kiasi cha kuahirisha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 ya Uhuru kwa miezi yote hii!

    ReplyDelete
  5. Ahhh, ahhh, ahhh,

    Hawa jamaa Ubalozi wa Tanzania Ufaransa walikuwa wapi mpaka kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru nje ya muda?

    Wanakuwa kama hawapo Duniani kama Katibu wa Jumuia ya Watanzania Ugiriki aliyekanusha shida zinazowakuta Wabongo, hadi nchi inakaribia Kuuzwa kwa Mkopo kwa Mabilionea wa Urusi yeye hana habari kabisaaa!!!

    ReplyDelete
  6. Lohh Mifaransa Ubalozini kwao hapa Tanzania nuksi kweli kweli, unaweza kulipa hela zote hizo halafu unanyimwa viza!

    SI BORA NICHANGIE WAATHIRIKA WA MAFURIKO?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...