Ubalozi wa Tanzania Nchini Ufaransa ukishirikiana na Chama cha Watanzania Ufaransa (CCWU) wanaandaa sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara kwa lengo la kuitangaza Tanzania, utamaduni wake na fursa za utalii na uwekezaji.
Sherehe hizo zitaadhimishwa Jumanne tarehe 22 na Ijumaa 25 Mei 2012 mjini Paris. Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo:
Sherehe hizo zitaadhimishwa Jumanne tarehe 22 na Ijumaa 25 Mei 2012 mjini Paris. Sherehe hizo zitajumuisha mambo yafuatayo:
- Maonyesho (exposition) ya vifaa vya utamaduni, picha, michoro na bidhaa za kitanzania k.m. chai, kahawa, korosho, katani, n.k.
Mkutano (conference) kutangaza fursa za utalii na uwekezaji Tanzania. Makampuni na wafanyabiashara zaidi ya 150 kushiriki.
Chakula cha jioni (Gala Dinner) Jumatano Mei 23, 2012, chakula, burudani na mavazi ya wanamitindo wa kitanzania na ngoma za asili.
Maonyesho na Mkutano bure
Kiingilio kwa Watanzania: Gala Dinner: €50 (kwa watakaojiandikisha na kulipia kabla ya 31 Machi 2012) na €70 watakaojiandikisha kuanzia Aprili 1 hadi Aprili 30, 2012). Mwisho wa kujiandikisha na kulipia ni tarehe 30 April 2012.
Tumia maelezo yafuatayo kufanya malipo kwenye akaunti ya benki:
EMBASSY OF TANZANIA – PARIS
BANK DETAILS
Bank code | Agency | Account no. | RIB key | ||
3078 | 00001 | 1049296003 | 77 | ||
| |||||
IBAN | FR76 3047 8000 01010492 9600 377 | ||||
| |||||
BIC | MONTFRPPXXX | ||||
| |||||
ACOUNT NAME | EMBASSY OF TANZANIA – SPECIAL ACCOUNT | ||||
| | ||||
Watanzania waishio Ufaransa na nje ya Ufaransa wanakaribishwa!
Mara zote tunapokuwa tunatumia rangi Nyekundu linapokuja suala la mawasiliano verbal and non verbal,tunamaanisha hali ya hatari,mfano msiba,ajali,mauaji,vita,magonjwa nk.Mwandishi wetu hiyo dhana hakuizingatia katika uwasilishaji wa ujumbe wake katika jamii.
ReplyDeletemnasema lengo ni kutangaza nchi halafu mnaweka kiingilio??? Tna uero 50???
ReplyDeletekwanini msiwe wazi tu kwamba ni kama dili flani tu?
Be serious guys!!!
Mdau Anonymous wa Sat Mar 17, 10:58:00 AM 2012
ReplyDeleteRangi ya Taarifa ni 'nyekundu' kumaanisha Hatari ,Dharura kwa vile sherehe imechelewa saaana miezi 6 mbele Sherehe ni ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania maadhimisho yalistahili yawe tarehe 9 Disemba 2011 sasa yanafanyika nje ya muda tarehe 22-25 Mei, 2012 !
Huu ndio Ubize wa Majuu?
ReplyDeleteHivi hadi Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania Ufaransa nao wanabeba Ma box?,,,inaonyesha wapo bizy sana na masuala yao binafsi kiasi cha kuahirisha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 50 ya Uhuru kwa miezi yote hii!
Ahhh, ahhh, ahhh,
ReplyDeleteHawa jamaa Ubalozi wa Tanzania Ufaransa walikuwa wapi mpaka kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru nje ya muda?
Wanakuwa kama hawapo Duniani kama Katibu wa Jumuia ya Watanzania Ugiriki aliyekanusha shida zinazowakuta Wabongo, hadi nchi inakaribia Kuuzwa kwa Mkopo kwa Mabilionea wa Urusi yeye hana habari kabisaaa!!!
Lohh Mifaransa Ubalozini kwao hapa Tanzania nuksi kweli kweli, unaweza kulipa hela zote hizo halafu unanyimwa viza!
ReplyDeleteSI BORA NICHANGIE WAATHIRIKA WA MAFURIKO?