salam,
 
Baada ya kufanikisha uundwaji wa Music Academy Tanzania chini ya usimamizi wa ASET na URBAN PULSE CREATIVE kwa mara ya kwanza wana academia walipata fursa ya kutumbuiza live stejini katika ukumbi mpya wa kisasa Dar Live uliopo mbagala siku ya  jumamosi hii.
 
Hii ilikuwa ni mojawapo ya hatua waliopiga kuonyesha vipaji vyao na kuwajengea uzoefu kutumbuiza mbele za maelfu ya mashabiki waliojitokeza kupata burudani.
 
Music Academy inaendelea kutoa mafunzo na pia kutafuta vipaji vipya katika tasnia ya muziki ikiwepo kucheza, kuimba, kutunga, kurap, kupiga vyombo mbalimbali n.k na kutoa fursa ya kujiunga katika bendi, vikundi au kuanza kama solo career/ artist mara tu wanapofuzu ili kuimarisha mziki wa kitanzania na pia kuwapa vijana ajira. Mazoezi hayo yataendela kufanyika mara tatu kila wiki kwa wiki kadhaa ndani ya ukumbi wa Baobab Kinondoni Vijana.
 Asanteni,
 ASET  na URBAN PULSE CREATIVE

 Kikosi cha wana Twanga Academy
 Komandoo Hamza Kalala akiongoza wanafunzi wake
Hapa sebene hadi wapi sijui.....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Dar Live JUUUUU!, Mbagala JUUUUU!

    Hamtoi Maoni ya kukandia sasa!

    Mabomu ya NATO kwa kutumia ndege zisizo na Marubani yamewaangukia Waosha vinywa sasa Kimyaaaaaaa!

    ReplyDelete
  2. Diamond upoooo????


    Wewe ndio uliisasambua Mbagala mwaka 2009-2010 ktk wimbo wako kwa kujali kulinganisha misitari ya Mashairi yako na kupotosha ukweli hadi watu wengi wakaamini kuwa Mbagala ni msituni nahakufai kabisa?

    Sasa kazi kwako unayo nafasi ya kuipaisha Mbagala tena baada ya kuitweza sana kipindi kile.

    -Hivi utafikiri pana demu Mbagala alikumwaga?

    -Au ulitoa barua ya posa Mbagala ukakataliwa hivyo kwa Ghadhabu ukakandia kwa kutoa single?

    Wewe Diamond ni Muungwana sijui Abdillahi vile Abdul?...na Mbagala ni msitu sio wa uchafu, ni msitu wa Mademu rudi ipaishe tukupe Demu mkaliiii!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...