Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo (Machi 14 mwaka huu) limepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu uharibifu uliofanyika kutokana na vurugu za washabiki wa Yanga kwenye mechi dhidi ya Azam.

Kwa mujibu wa tathmini ya Serikali, katika vurugu hizo kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jumla ya viti 119 viliharibiwa. Gharama za uharibifu huo ni sh. milioni 5 ambazo Serikali imeagiza zilipwe mara moja.

Kwa vile washabiki wa Yanga ndiyo waliohusika na vurugu na uharibifu huo, gharama hizo zitabebwa na klabu hiyo ili Serikali iweze kufanya ukarabati haraka.

TFF inarudia tena kulaani na kukemea vurugu zinazofanywa na washabiki viwanjani na kusababisha usumbufu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa vifaa hasa kutokana na ukweli kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa burudani.

Tunapenda kuwakumbusha washabiki na klabu kuwa vitendo hivyo si vya kistaarabu, hivyo havikubaliki katika mpira wa miguu, na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa wahusika iwapo vitaendelea kutokea viwanjani.

TENGA KUZUNGUMZA NA WAANDISHI KESHO
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga kesho (Machi 15 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ofisi za TFF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Refarii naye atozwe kwa kusababisha vurugu!

    ReplyDelete
  2. Wachawi wakifungwa lazima wataleta kelele na fujo kwani wamezoea kubebwa kila kukicha. Kifo kwa Simba na Yanga. Tunataka wachezaji wenye vipaji si wachawi.

    ReplyDelete
  3. Mechi za Yanga zichezwe Kaunda;Simba Tandika mabatini. Hawana uchungu na uwanja huo

    ReplyDelete
  4. Usiibe kabla giza halijaingia ni msemo wa busara na mahusia yanayoasa mtu kutokata tamaa na hatimae kufanya mambo yasiyo kubalika au ya uvunjifu wa sheria. Ni msemo unaojenga kuwa mtu upambane hadi dakika ya mwisho. Giza linaweza kuwa na maana ya umri mkubwa n.k. Kwa wale wanaosema wachaga ni wezi miaka nenda rudi waendelee kulala na kulalama kuwa wachaga ni wezi hadi giza liingie liwakute wakilalama. Ushauri ni kuwa nendeni jela au mahabusu mfanye sensa mje na taarifa kama wako wangapi huko kulinganisha na wengine. Huo ndio utakuwa mwisho wa huo ulalamishi japo rafiki yangu mmoja aliniambia kuwa wanaiba kwa kutumia akili sana hivyo si rahisi kuwakamata. Sawa, akili!! Wanaoelewa siri ya urembo sasa wanagombea kuoa wachaga,sasa sijui kama kuna fahari gani katika kupambana kwa udi na uvumba kuoa wezi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...