Sehemu ya raia wa Ethiopia 98 wakiwemo na Watanzania wawili wakitaremka kwenye gari la polisi katika Mahakama ya Hakim Mkazi Morogoro, kujibu mashitaka ya kuingia nchini isivyo halali.
Sehemu ya raia wa Ethiopia 98 wakiwemo na Watanzania wawili wakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro jana, wakisubiri kusomewa mashitaka likiwemo la kuingia nchini bila kibali walipokamatwa katika Kijiji cha Melela, Wilaya ya Mvomero wakati wakisafiri kuelekea Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kuvuka mpaka.Kesi hiyo iliahirishwa kwa kukosa mkalimani. Picha na mdau Juma Mtanda
hawa watu wanatia huruma, Niliwahi kwenda nchi yao once kutembea. Population yao ni kubwa sana, na wana ardhi mbaya( semi desert). Ni shida kweli. My advice kwa serikali ni kuwarudisha kwao. Kuwafunga ni kutumia resourses za serikali bila ya umuhimu. Hela watakazotumia wakiwa jela, zingeweza kusaidia tatizo la omba omba dar.
ReplyDeleteWaafrika wenzetu ruksa kuingia bila visa ili kuondoa usumbufu wa kesi zisizo na maana. Unafikiri TZ kazi gani watafanya hao?
ReplyDeleteni rahisi na kuokoa gharama kama watu hao watarudishwa nchini kwao badala ya kuwahifadhi hapa na kesi hizo hata wakishindwa ni hasara na ni kupotezeana muda.
ReplyDeleteNi wakati sasa wa kuwafunga mawakalan wao
ReplyDeleteTubadilishe sheria zetu ili watu kama hawa warudishwe kwao bila kuingia gharama za kuwatunza ktk mahabusu na magereza.
ReplyDeleteNakuunga Mkono Mkibosho Anonymous Thur Mar 08, 07:03:00 AM 2012
ReplyDeleteMjenga nchi ni Mwananchi na Mvunja nchi ni Mwananchi pia!
Wahabeshi hawana hatia wao ni wapita njia na wanahangaika na kutafuta maisha kama wafanyavyo Watanzania nchi zingine Duniani, La muhimu ni:
KUWAFUNGA MAWAKALA AMBAO NI WATANZANIA NA WAHABESHI KUWARUDISHA KWAO TUKISHIRIKIANA NA UBALOZI WAO HAPA TANZANIA WAKAFUNGWE HUKO KWAO!.
Nibora kuachana na kesi zisizo na maana hata kidogo zinazo haribu pesa za wadanganyika hawa niwaafrica wenzetu njaa ndiyo inayowasumbua tuna kesi nzito na zinazokiuka haki za kibinadamu kwenye Mahakama zetu humu nchini na zingine zimeachwa na kutelekezwa kwenye Ofisi za wanasheria wetu wa Serikali. Mheshimiwa waziri wa Home rudisha watu hawa makwao we are westing time and money that could do something beter for the TZD's. Katto
ReplyDeleteni vizuri serikali ya tanzania kuzungushia ukuta nchi nzima ili waamiaji wasingie nchini na tuweke chupa juu ya ukuta
ReplyDeleteinapendeza sana kuona watu wanatoa mawazo mazuri mno kuhusiana na hawa wageni waliokamatwa .Ni kweli kuwafunga itatugharimu mapesa kibao ambayo yangetusaidia na istoshe hawa watu pamoja na kwamba wamevunja sheria ila hawa ni watu wa njaa na si magaidi.Ni watu wanaotafuta riziki kama walivyokuwa ndugu zetu weeengi waliopo ulaya wanaojiripua ili wapate kusavaiv.
ReplyDeleteNAKUBALIANA NA WALIOTANGULIA KUWA TUSIWAFUNGE BALI TUWARUDISHE KWAO.
Kutokana na njaa iliyopo huko kwao Ethiopia jamaa tukiwafunga hapa kwa Dona na Maharage yetu wataona kama wapo MAREKANI!
ReplyDeletePANA UWEZWEKANO KIFUNGO KIKIISHA WATAKATAA KUTOKA GEREZANI!!!!!!!
Waachieni tu waishi Bongo kwani wataiweza - watarudi wenyewe!!
ReplyDeleteWaachieni tu waishi Bongo, wataiweza watarudi wenyewe!!
ReplyDeleteNajua sheria ni sheria lakini pia kuna ubinaadamu. Kwa nini serikali is zungumze na ubalozi wao watate tatizo hili kirafiki? Wa-Libya wali kamatwaga katika vita ya Uganda na Nyerere aliwarudisha bure kwao.
ReplyDeletenjia pekee ya Afrika kufanikiwa ni kuungana.
ReplyDeletesasa je tutafika kweli kwa mtindo huu humuhumu barani Africa?
nchi za ulaya wameungana, wako huru kuingia nchi moja hadi nyingine, sisi je?
Ni rahisi kuingia ulaya kwa mwafrika kuliko kuingia nchi nyingine barani Africa.
Nimwamini nani?, nimpende nani?, kigeugeu!, kila mtu ananigeukia!
ReplyDeleteKwa maisha ya sasa tusipendelee kuwaamini sana watu hasa Wageni kama hawa Wahabeshi mara nyingi wazamiaji hubeba vitu vya hatari sana kama Madawa, Silaha na wakati mwingine huwa tayari kufanya Uhalifu ili wasonge mbele na Safari!.
Mara zote Msafiri ni Kafiri!
Wahabeshi wana Rekodi mbaya sana Duniani ya Kuzamia wanaposafiri:
ReplyDelete1994-Michezo ya Olympic Atlanta-Marekani timu nzima ya Riadha Wachezaji, Waalimu, Makocha na Madakitari tena wa umri hadi mkubwa hakuna aliyerudi nyumbani wote walizama enzi zile kwa Bill Clinton!
2008-2009 Hivi ktk Michezo fulani hapa Tanzania nadhani CECAFA Timu ya Soka ilizama hapa Bongo hakuna aliyerudi kwao!
2010-World Cup ,Africa ya Kusini walienda kama Waalikwa na Mashabiki hakuna aliyerudi nyumbani!
Usishangae wao kuja hapa inawezekana hakuna safari ya Afrika ya Kusini wala nini,,,inaweza kuwa walipanga wakamatwe ili Walizime gari hapa au kupumua na njaa ya kwao kwa kula Dona na Maharage ya bure MAGEREZA YA TANZANIA!
Kwa Taarifa tulizozipata kwa Wadau Watanzania waliosafiri kupita huko kwao Ethiopia inasemekana Wahabeshi wanawasumbua sana Wageni kwao hasa Waafrika Wenzao!
ReplyDeleteSasa leo ni zamu yao ugenini!
Hata hivyo pana taarifa zinesema kuwa uwepo wa Ofisi za Umoja wa Afrika unampa PM wao Zenawi ku influence Utawala wa Umoja kwa sana!
Hawa Jamaa Wahabeshi ''wameua Kenge kiaina''!
ReplyDeleteNi wazi kuwa kwao kuna Njaa na pia zipo nchi zingine hata hapa jirani mfano Uganda, Burundi na Rwanda ukimshitaki mtu akiwekwa Mahabusu unamhudumia kwa chakula hadi kesi inakwisha na pia hata kama mtuakifungwa Magerereza ya nchi hizo yana njaa balaa!
Sasa Magereza ya Tanzania ni tofauti sana ingawa chakula sio kizuri sana lakini angalau pana chakula cha Bure!
Kama ni wasafiri kwa nini waje Tanzania tu, wasipitie Rwanda au Uganda?
SASA WAETHIOPIA WANAWEZA PIGA MAHESABU YA KUKAA KIFUNGONI TANZANIA ILI WADOWEE DONA NA MAHARAGE YETU BUREEE!!!
Nimetiwa moyo sana kuona kuna watu wanaangalia suala hili kwa ubinadamu. Kwa kosa la kuzamia kienyeji warudisheni kwao, kwa gharama ya ubalozi wao, hivyo ndiyo mataifa mengi yanafanya.
ReplyDeleteKama kuna mengine basi yashughulikiwe ipasavyo.
Unachomtendea mtu, huwa kinakurudia (karma).
Kana Ka Nsungu.
waacheni waishi,mbona Watanzania wengi wanaishi nje ya nchi?
ReplyDelete