Kaimu mkurugenzi wa halmshauri ya wilaya Namtumbo Constatino Mushi kushoto akimfariji mwanafunzi wa kidato cha 3 shule ya sekondari Runa wilayani humo Abdul Ngonyani aliyevunjika mkono wake wa kulia kufuatia gari walilokuwa wakisafiria kupinduka na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja na wengine kujeruhiwa,katika ni baba mzazi Abdul Mang'inyuka,
Mwezeshaji wa mafunzo ya ukimwi kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya halmshauri ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Pees Kamugisha akitoa mada wakati wa mdahalo wa wazi juu ya maambukizi mapya ya ukimwi kwa wanafunzi wa shule ya sekondari st benedictine hanga, uliofanyika jana shuleni hapo,
Mwenyekiti wa kamati ya kudhibiti ukimwi ya halmshauri ya wilaya ya namtumbo ambaye pia ni makamu mwenyekiti wa halmshauri hiyo Kassim Ntara akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya St Benedictine Hanga wakatri wa mdahalo wa siku moja juu ya kujikinga na maambikizi mapya ya ukimwi uliofanyika jana shuleni hapo,
Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine Hanga wilayani Namtumbo,wakiiangalia chini jana wakati wa mdahalo juu ya masuala ya ugonjwa wa ukimwi ulioendeshwa na idara ya maendeleo ya jamii ya halmshauri ya wilaya ya Namtumbo kupitia mpango wake wa elimu ya ukimwi mashuleni uliofanyika shuleni hapo,
Wanafunzi wa shule ya sekondari St Benedictine Hanga wilayani Namtumbo wakimsikiliza mwezeshaji wa masuala ya ukimwi kutoka idara ya maendeleo ya jamii ya wilaya hiyo Peres Kamugisha hayupo pichani wakati wa mdahalo wa siku moja juu ya namna ya kujiepusha na maambukizi mapya ya ukimwi uliofanyika shuleni hapo jana.PICHA NA MUHIDIN AMRI
Hii kali. Hawa wanafunzi mbona wana nidhamu ya uoga sasa wanaangalia chini kama kuku walio nyeshewa mvua jamani wakati watoto wenzao mijini umri wao wamechangamka na wanajua mambo mengi mwe mambo ya mikoani sijui..........kazi kwl kwl
ReplyDeleteHizo ndio 'haya' za kike mdau, si nidhamu ya woga... Mtoto wa kike mwenye 'haya' anapendeza sana.. Sie mtoto mdogo anakukodolea macho kama mjusi kabanwa na mlango hadi unaogopa.
ReplyDeleteKwa kweli walimu wana kazi ya ziada hapo watoto Confidence ZERO, Yaani hawajiamini kabisa! Kila mmoja anaogopa camera, duh! akiambiwa asimame aelezee jambo fulani ataweza kweli??
ReplyDeleteMdau wa Tue Mar 20, 08:59:00 AM 2012, Hata mbuyu ulianza kama mchicha, hiyo pia ni process ya kuwajenga confidence maana kama watatembelewa mara mbili mara tatu na wageni basi watazoea wala si kwamba walimu wana kazi kubwa, confidnce inajengwa na uzoefu wa kujichanganya
ReplyDeleteHAWA waelimishaji naona walikuwa wanaongea mambo MAZITO SANA, watoto wa vijijini hawajui wanaogopa au anawaambia watumie kondomu wanaona ka anatukana, hayo mambo yaleteni Mjini maana hapo hata ukimwambia ajibu ataogopa kusema tttuuuuuuuuuuuu
ReplyDeletealiekwambia wanaogopa kamera nani...kalagabaho wanaguswa n amambo wanayoelezwa..safi sana mtoa mada uliwagusa kunako...maana huwa hawaambiwi kbs mambo hayo na wazazi wao
ReplyDeleteMdau ulitowa mada ya mwanzo hao watoto sio kama ni nidhamu tu bali inonekana tayari wengi wao tayari wana praktisi hayo mambo na hapo inaonesha kuna maneno yamewagusa kile wanachokifanya kama ishara ya kuhofia afya zao na maisha
ReplyDeleteMi kwa mtazamo wangu somo kama hili at least angefundisha kijana mwenzao na sio baba/mjomba wao. Nadhani ingewasidia kuuliza maswali. Imagine unafundishwa reproduction au socialization na mama/baba yako.
ReplyDeleteWAACHENI WATOTO WADOGO WATOMBANE MBELE NA NYUMA HII FURAHA YA DUNIA.
ReplyDelete