Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ni muhimu zoezi la Madereva kupimwa akili mara kwa mara badala ya kukabidhiwa Leseni kuwa ndio kimoja imetoka!

    InaweZekana mtu akapewa Leseni mwezi huu lakini mwezi ujao akapata matatizo ya Ugonjwa wa Akili!

    Hivyo pana wasiwasi ktk idadi ya Madereva walio barabarani wengi wakawa sasa ni Mataahira!

    ReplyDelete
  2. Haraka yote hiyo ya huyo T558 BQZ anayetanua kulia akawa anamwahi Hawara Gesti au mgao wa Rushwa!

    ReplyDelete
  3. Nakupongeza mchangiaji wa kwanza madereva wengi kama sio mataahira basi wana magonjwa ya akili ya kurithi, mambo ya barabarani magumu sana wengi wako makini lakini wanauawa na mataahira wachache.. KAZI KWELIKWELI.

    ReplyDelete
  4. Na kuna mwehu anaendesha basi kule mbele naye ana over-take magari matatu kwa mpigo. Huyu jamaa mwenye Land Cruiser ana akili kwani hapa amefunga breki ili kumpisha mwehu mwenye Hilux aingie kwenye 'lane' asije akauawa na hilo Yutong linalokuja huko mbele.

    ReplyDelete
  5. kweli kabisa mwenye hilux ni mwehu na mwenye basi ndio zaidi kwa sababu huyo mwenye basi kwanza anaovertake kwenye kona ambayo haoni mbele ni makosa makubwa ndo maana hakuona huko mbele kama kuna hilo tanker na hizo vx na hilux, stupid drivers, maboss wao kama wataona hii picha ni tosha kabisa kuwawajibisha hao.
    Big up mdau kwa picha hii.

    ReplyDelete
  6. Unauwezekano hata mpiga picha alikuwa anaendesha GARI tehtehteh, Nchi yetu tunasema Samaki mmoja akioza wote wanaoza hii ni tabia hata kwenye njia za kona mtu huitowa gari bila kusubiri kuona kulia kwake sababu anaona hakuna atayesimama, na pia mtu anaogopa kuitowa gari anatokea mtu na gari anapinda na gari bila kuonyesha ishara ya taa wapi anaingia kushoto au kulia? Hizi ni tabia zipo utakuta foleni inaenda vizuri ila mjinga mmoja ataitowa gari akalazimishe mbele basi wengine 6 wataiga matokeo njia inaanza foleni ya kuchomekeana. Nishaona mtu hajagongwa amekoswa kuchunwa ila kakasirika kashuka ugomvi mpaka inabidi watu uvumilivu unawashinda wanaingia kwenye kupita miguu na bike. Nyerere alivyokuja kwetu Pwani nasikia alisema hataki kuona Punda wa Biashara tena mjini ila Hao Punda mie naona wamezidi mikokoteni kibao na vile vigari vyekundu havifai Kariakoo pia.

    ReplyDelete
  7. Naomba hii picha isiishie hapa jamvin, ipelekwe polisi ili mwenye gari achukuliwe hatua. Vilevile ichapishwe kwenye magazeti ili uzembe wa dereva huu utangazwe na watu wote wajue kuwa kuendesha garikizembe hivi nui kosa.

    ReplyDelete
  8. Dereva wa Toyota, kama una haraka si ungeondoka juzi!!!

    ReplyDelete
  9. tena gari lenyewe hiyo pick up pia lina tatizo stop light yake ya kushoto haiwaki.

    wajinga kama hawa wanaboa sana

    ReplyDelete
  10. t558 bqz... ngoma mpya hiyo. jamaa hajui namna yakuendesha nje ya jiji.... anadhani ktk highway unatanua pia.... naye wa basi balaaa tupu.... hata chizi huogopa kugongwa na kukwepa magari.... wote wawili wana issue zingine... kama vile kuwahi hawara gesti au rushwa

    ReplyDelete
  11. Pambano ni kali sana hapa barabarani kwani huku kuna wachezaji watatu machachari akiwemo Tanker mbele ya landcruiser VX na Midfilder Toyota pickup na kule mbele kama unavyona pasi zinavyoenda kama drafti.

    Goli lazima lipatikane hapa

    ReplyDelete
  12. Naomba niwaweke wazi kdg,ni kwamba jamaa kachua chuma kipya hivyo ndo anajaribu kukichek km kipo mwake?Madreva wa mabasi ndo staili yao ya kutumaliza.......picha nzuri sana

    ReplyDelete
  13. Mdau Tue Mar 20, 02:53:00 PM 2012 hiyo inayowaka kwenye Hilux ni indicator, sio stop light.

    ReplyDelete
  14. Mi nina mtazamo tofauti kidogo.

    1, Ni kweli wanao overtake bila kuangalia wana makosa, hilo halipingiki. Na madereva wanaoongoza kwa barabara kuu za mikoani ni madereva wa mabasi.

    2, Tatizo lililopo kwa Tanzania, (ukiachilia mbali tatizo la madereva) ni:
    a, ufinyu wa barabara. Barabara kama za mikoani zinatakiwa ziwe pana za kutosha

    b, barabara kutumika na kila mtumiaji. Barabara kuu, utakuta baiskeli humo humo, mifugo humo humo, mikokoteni nk. Hii ni hatari sana

    c, madereva polepole. Ki kawaida barabara kuu inapaswa magari kwenda kwa kasi fulani ya juu, kwani watu wanasafiri km 500+ hivyo mwendo muhimu. Sasa unaweza kukutana na mtu anaendesha gari 40km/h tena yuko kati kati ya barabara

    d, ubovu wa baadhi ya magari. Mfano hiyo picha ya gari ya mkaa hapo juu, kama haya yamejaa barabarani. Yanaenda pole pole.

    e, ukosefu wa 'by pass road', yaani barabara zinazokwepa miji. Barabara kuu zinakatiza vijiji vingi, ambavyo vina pilika za kila siku

    Sasa kwa kuwa Tanzania ni nchi inayoendelea, ni vema adhabu ya papo kwa papo ya viboko irudi. Kuwe na doria, ukikamatwa kama huyo dereva wa basi, unapata fimbo 12 unaendelea na safari. Hii ni kwa kuwa watu wengi hawaoni uchungu kutoa rushwa ama adhabu zingine, kwani haziwahusu moja kwa moja. Ila adhabu ya kudhalilisha na inayokuhusu, utafikiria mara mbili kabla ya kuvunja sheria.

    Ni hayo nakumbuka kwa sasa.
    Kama umesoma hadi hapa, shukrani.

    ReplyDelete
  15. Mdau wa hapo juu kweli wale wanaoona wenzao wamejipanga vizuri kwenye foleni halafu wao kujifanya wana haraka sana WANANIKERA KWELI KWELI.

    Na kama wanajitambua tutawaita WAJINGA. Na ndiyo hao hao wanaosababisha ajali kwa kiwango kikubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...