Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Editha Mushi (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya sh. mil. 25, Mhandisi wa Maji Wilaya ya Geita, Daud Sweka kwa niaba ya Mkurugenzi wa wilaya hiyo za kusaidia mradi wa visima vitatu  vya maji safi na salama ya kunywa kwa wakazi wa Kijiji cha Mkolani-1 wilayani humo hivi karibuni. Katikati ni Meneja Mauzo wa TBL Geita, Issa Msuya. 
Mwenyekiti wa mtaa wa Nyamakale, Sizya Mulelemi Mashilungu akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 25 Enock Kangasa, mkandarasi anayatekeleza mradi wa visima vya maji safi na salama ya kunywa kwa ajili ya wananchi wa  kijiji cha Mkolani-1 Geita Mwanza, muda mfupi baada ya hundi hiyo kutolewa na kampuni ya Bia nchini (TBL). Kulia anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa TBL Editha Mushi. 
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBl), Editha Mushi (mwenye miwani) akipata maelezo  kutoka kwa mkandarasi, Enock Kangasa (mwenye shati jeupe la mikono mifupi ) ambaye anachimba visima vya maji  katika Kijiji cha Mkolani, Geita, kuhusu 'ring' zinazotumika katika ujenzi wa mradi wa visima vya maji uliofadhiliwa na  kampuni ya TBL  kwa sh. milioni 25. Hafla ya kukabidhi hundi ilifanyika kijijini hapo mwishoni mwa wiki. (NA MPIGAPICHA WETU)

Baadhi ya wananchi wa Nyamakale Mkolani -1  wakiwa na hundi ya sh. milioni 25 walizopewa na TBL 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hakika nchi imebinafsishwa, yaani madawati ya shule msaada kutoka PLAN kisima cha maji msaada kutoka TBL. Hivi kodi zetu zinafanyiwa nini?

    ReplyDelete
  2. Taifa la walalamishi.
    Jiulize wewe umechangia nini. Kwetu
    moshi bado tuna moyo wa kujitolea barabara, shule, madawati tunafanya kwa moyo wa harambee, kukaa kungoja serikali ni ulemavu wa kujitakia. Kama madawati yakitolewa bure huwa ni ya wahisani hivyo hayana uchungu kama tungechangia wenyewe. Kodi zitumike kulipa askari,waalimu, miundombinu, nk... Pale manzese uzuri wananchi walimkamata seremala mmoja akiiba madawati na kutengeneza samani(fanicha) akauliza kwani zenu? Hata ukikuta mtu anaiba mfuniko wa mtaro au bomba za kingo za barabara watu watatetea, anatafuta kula !!!!

    ReplyDelete
  3. Oneni aibu kutegemea misaada huku mmevalia ma wax ya kushiba. Kuomba hudhalilisha utu. Acheni hizo wabongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...