Ankal, habari za kazi, hongera kwa kazi nzuri ya kuiabarisha jamii mambo muhimu yanayowahusu.

Nipo Bagamoyo kwa sasa kama mtalii wa ndani, kama ijulikanavyo Mji huu ni maharufu kwa kuwa na vivutio mbali mbali vinavyo wavutia wengi kutoka nje na ndani ya nchi kuutembelea mji huu.

Kaole ni moja ya sehemu muhimu sana kwa utalii, njia ya kwenda Kaole kutoka mjini Bagamoyo inapitia Chuo cha sanaa, lakini kwa sasa njia hiyo imefungwa baada ya mti kuanguka katikati  ya Barabara hivyo kuwazuia  waendao kwa magari, hali inayo sababisa kero kubwa sana kwa watalii. Napenda kujiuliza hivi uongozi wa Halmashauri upo wapi? Inachukuwa muda gani na shilingi ngapi kuutoa mti huo ili kulinda hesha ya mji wa Bagamoyo? Naushari uongozi wa bagamo uchukuwe hatua za haraka za kuuondoa mti huo, Kwanza hata kiusalama unapunguza kasi ya kazi hiyo maana umezuia mawasaliano kati ya Kituo cha Polini na Mji wa Bagamoyo.

Hasanteni.
Mdau Sixmund

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kwakweli huo ni uzembe mkubwa, tena kwa kuwa mji wa Bagamoyo auna Mkuu wa wilaya kwa sasa ambae anaishi mbele kidogo toka mti ulipo angukakia. Nadhani angekuwepo huo mti usinge kuwepo. Viongozi hebu utowenu basiiiii.

    ReplyDelete
  2. Wewe mpita njia au jirani, kwa nini usiuondoe

    ReplyDelete
  3. Mbona hamkujitolea kuutoa huo mti na badala yake umekimbilia kulalamika? Nafikiri watu wangejituma wala isingefikia hapo lakini kama kawaida yetu kulalamika,kama hadha ni nyie muipatayo hao Halmashauri wapo wanapumzika na familia zao.

    ReplyDelete
  4. Hao ni wapitanjia tu, tena amesha sema alikuwa kama mtalii wa ndani, ameiletea pesa bagamoyo, na wapo wengi walio iletea pesa hasa waendao Kaole, pesa hizo zinawalipa mishahara watendaji wa wilaya hiyo, kwanza ni kero hata kwa Miss Nyamizi binti maarufu huko Kaole anapo shuka mjini kununua supuzake za samaki.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...